Mshtuko: Mloganzila hospital hawana maji

Mshtuko: Mloganzila hospital hawana maji

sheiza

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2010
Posts
7,634
Reaction score
11,691
Hii ni hospital kubwa ya kimataifa inayohudumia watu kutoka maeneo mbalimbali nchini na duniani.

Kwa mujibu wa maelezo, ndio hospital ya mwisho ambapo mgonjwa akishindikana basi anapelekwa nje ya nchi. Maana yake inashikilia roho za wengi na ina mabingwa wa kutosha.

Ikumbukwe hii hospital iliboreshwa mno enzi za Magu na kuongezewa uwezo wa vifaa tiba na wataalam.

Lakini cha ajabu ni siku kadhaa sasa hospital haina huduma ya maji. Tahadhari ni kuwa ukienda na mgonjwa beba shuka maana hakuna mashuka, yote ni machafu.

Hali ni mbaya. Ummy hata kama unalijua hili najua linakuumiza ila yawezekana lipo nje ya uwezo wako.

Wakati huo Juma Aweso yupo Marekani anakula keki na Kikwete New York. Huku wengine wanaimba mama anaupiga mwingi.

Hivi na mvua hizi utasingizia nini sababu ya kukosa maji. Mungu anazidi kuwaumbua.

Mama nae yupo bize kugawa hela kwenye michezo. Hawa watu hawana uchungu na lolote sababu wanajua wao, watoto zao na wajukuu zao hawawezi pata huduma yoyote kwenye hizi hospital. Hizi ni za wanyonge.

Enzi za Magu aliweka utaratibu wa hawa viongozi kutibiwa pia kwenye hizi hospital.

Kwa sasa wanapishana angani kama chini moto unawaka(Benard Membe).
 
Ina maana hiyo hospitali hawana visima?

Ajabu, mgonjwa anaenda hospitali kutibiwa badala yake anatoka huko na ugonjwa mpya, sasa sijui akatibiwe wapi tena ... only in Tanzania!.
 
Maeneo mengi ya jimbo la kibamba kwa wiki sasa hayana maji na hakuna maelezo yoyote
 
Ina maana hiyo hospitali hawana visima?

Ajabu, mgonjwa anaenda hospitali kutibiwa badala yake anatoka huko na ugonjwa mpya, sasa sijui akatibiwe wapi tena ... only in Tanzania!.
Nosocomial zipo kote
 
I hate it, mada nzuri halafu mnamalizia na maujinga
Umuhimu wa viongozi kutibiwa kwenye hizi hospital utawezesha upatikanaji wa huduma bora. Huo ndio ulikuwa uelekeo. Ila kwa sasa tumerudi kule kiongozi anaenda SA kufanya check up ya mafua na kifua.

Kwa hiyo jikite kwenye ujumbe. Sio personalities.
 
Ina maana hiyo hospitali hawana visima?

Ajabu, mgonjwa anaenda hospitali kutibiwa badala yake anatoka huko na ugonjwa mpya, sasa sijui akatibiwe wapi tena ... only in Tanzania!.
Nenda hata sasa ukashuhudie hali halisi. Hii sio siasa. Ni ustawi wa watu tu.
 
Aise!!
inatisha!!!

Hospitali kubwa kama ile ambayo ni tegemeo la watanzania na hata mataifa mengine inakuwa hivyo?!!!!

Kama ni kweli basi Mkurugenzi wa hospitali hiyo anafaa aondolewa mara moja kwa kushindwa kusimamia utawala na utendaji kwa ujumla, ni kuidhalilisha hospitali ya kimataifa MLOGANZILA.

Muhimbili MLOGANZILA ni jicho la Taifa, hata watendaji kwa maana watumishi kwenye hospitali hiyo lazime wawe waadilifu na weledi.
 
Aise!!
inatisha!!!

Hospitali kubwa kama ile ambayo ni tegemeo la watanzania na hata mataifa mengine inakuwa hivyo?!!!!

Kama ni kweli basi Mkurugenzi wa hospitali hiyo anafaa aondolewa mara moja kwa kushindwa kusimamia utawala na utendaji kwa ujumla
Akasimamie utawala wa DAWASA?
 
Back
Top Bottom