Mshituko: Rafiki yangu tuliyeshibana unamuoaje Dada yangu?

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
5,154
10,809
Hili ni jambo la kushangaza sana, huyu jamaa kwao walikuwa masikini alafu nyumbani kwao ni mbali na shule, hivyo kwa kuwa tulikuwa marafiki tulioshibana na discussion tulikuwa tunafanya pamoja nikamkaribisha nyumbani kwetu akawa kama mtoto wa familia yetu kabisa.

Baba yangu alikuwa anamlipia ada, nguo za shule kuanzia form 3 mpaka form 4 amenunuliwa na baba yangu cha ajabu baada ya kumaliza chuo na kupata kazi amemuoa na kumtundika mimba Dada yangu wa mwisho kweli hii ni sawa!

Niende kwenye harusi yao au nisiende? Nimsalimie au nisimsalimie? Cha ajabu baba yangu na mama yangu wamekubali umuoe Dada eti kisa wewe ni Dr ataishi maisha mazuri!

Kwa hili rafiki yangu hufai kabisa na sijui umekula maharage ya wapi.

1620635639068.png

 
Kamtia mimba na kamuoa inakuuma..Angemkataa je.?
Yote aliyotenda baba yako ilikua sehemu ya msaada tu kama inavyotakiwa binaadamu yoyote kusaidia wengine. Kusaidia hakuhalalishi undugu wa damu hadi kuwe na miiko. Jamaa kafanya vyema kaamua kulipa fadhila kwa kuimarisha undugu daima (kama ni wakristo) mwa ndoa.
 
Happ kuna faida mbili. Kwanza atalipa fadhila kwa kuwalea na kuwasomesha wajomba zako mzigo ambao pengine mngeulea ninyi Kama familia endapo angezalia home. Pili na wewe umepata chansi ya kwenda kulala sebuleni kwa shemeji huku ukiangalia TV usiku kucha Kama wenzio wengi wanavyozililia hizo nafasi.
 
Back
Top Bottom