Unajuwa huu ukumbi si zile maskani za vijana muliowanyima elimu na kuwaongoza katika propaganda za siasa chafu, fitna na fujo. Kwanza na tumjadili mwandishi wa hii article ambae ni Mhe Mohamed Seif Khatib na namna gani yeye mwenyewe aliandika shairi juu ya muungano na then tuweze kumpa benefit of doubt kama ni mtu msema kweli na mtetezi wa kweli chama na sera butu, au ndio kama anavyosema katika shairi lake hapo chini: Shairi la Mohamed Seif Khatib kutoka kitabu chake cha Wasakatonge shairi No 4 pg 3 :
KOSA?
1. Metufunga kamba,
Za miguuni,
Za mikononi,
Za midomoni,
Na kututosa baharini !
2. Eti mnataka,
... Tuogelee,
Tujongelee,
Tujiokoe,
Hadi tufike ufukweni !
3. Kosa letu kubwa,
Kudai haki?
Yetu miliki?
Mna hamaki,
Na huku mnatukashifu !
4. Msitunyanyase,
Siyo watwana,
Watu wa mana,
Tuloungana,
Kwa heshima na taadhima!
5. Sisi tuna kwetu,
Wenye asili,
Ilo kamili,
Na serikali
Ilopatikana kwa damu !
6. Kuheshimiana,
Kwa kupendana,
Kuelewana,
Kusikizana
Hilo tutakubaliana ! Waungwana hawa ndio akina Nape na genge lao, hili shairi aliliandika Mhe Mohamed Seif Khatib katika kitabu chake kinachoitwa WASAKA TONGE ..