Mshikamano Msibani-Mbowe, Cheyo, Mrema, Mbatia-Wapo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshikamano Msibani-Mbowe, Cheyo, Mrema, Mbatia-Wapo!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Jan 20, 2012.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Nimepata nafasi kuhudhuria msiba hapa nyumbani kwa Jeremia Sumari.

  Kama ilivyo kwa Regia, hapa kwa Sumari ni vivyo hivyo, viongozi wa vyama vya upinzani wameungana na viongozi wa CCM na waombolezaji wengine kuwafariji wafiwa.

  Jioni hii, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akiongozana na Naibu Katibu Zitto Kabwe wameungana na Mwenyekiti wa UDP Mzew John Cheyo wapo kwa pamoja na mawaziri kadhaa wa serikali ya JK wakiongozwa na Mawaziri Wakuu Wastaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa!. na Fredrick Tuluway Sumaye!

  Jana rais Jakaya Kikwete na Katibu Mkuu wa Chadema Dr. Wilbrod Slaa wakifika nyumbani hapa kuwafariji wafiwa!.

  Mawaziri Wasira, Nchimbi, wabunge wakiongozwa na Katibu wa Bunge Dr Kashilila etc pia wapo!

  Ni jambo jema na la kupendeza uonapo ndugu wakikaa pamoja kwa upendo wakati wa shida na raha. Huu ni uthibitisho kuwa licha ya tofauti za kiitikadi, Watanzania tu wamoja kwa upendo na mshikamano miongoni mwetu!.

  "Mahali ni Pazuri..Ndugu Wanapokaa...

  My Take:
  Wanabodi hivi kama ushirikiano, upendo, amani na mshikamano unaofanyika misibani kama ungepelekwa mpaka Bungeni Dodoma, Jee Tanzania tungekuwa wapi?.

  Rip Jerry Solomon Sumari!.Thanks kwa Upendo, Amani, Ushirikiano na Mshikamano!

  Pasco.
  Update:
  Ratiba imetolewa.
  1. Misa kesho saa 2:00 Msasani Lutheran
  2. Saa 5 Mwili kupelekwa Karimjee
  kuagwa kitaifa.
  3. Mwili kurudi kulala nyumbani.
  4. Jumapili asubuhi kusafirishwa kwa ndege kwenda Arusha.
  5. Maziko Jumatatu.
   
 2. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #2
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,277
  Trophy Points: 280
  Mbona hujatuambia kama wamesalimiana au hawajasalimiana?
   
 3. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #3
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  hahaha.......... watu hawalali!!................. duh!!..................... haya pasco, karibu kwa maelezo zaidi...................
   
 4. m

  mitishamba JF-Expert Member

  #4
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  We! Unasema kweli!
   
 5. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #5
  Jan 20, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  safi sana tusigombane mpaka kwenye misiba
   
 6. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #6
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,576
  Likes Received: 18,546
  Trophy Points: 280
  Ratiba imetolewa.
  1. Misa kesho saa 2:00 Msasani Lutheran
  2. Saa 5 Mwili kupelekwa Karimjee
  kuagwa kitaifa.
  3. Mwili kurudi kulala nyumbani.
  4. Jumapili asubuhi kusafirishwa kwa ndege kwenda Arusha.
  5. Maziko Jumatatu.
   
 7. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #7
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Vipi kuhusu kusalimiana nani hajamsalimu mwingine...!
   
 8. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #8
  Jan 20, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huyu (Wasira) yuko kikazi tu! Siyo muombolezaji. Anafanya tu kazi aliyopangiwa na JK kwa ufanisi mkubwa.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nisahihishe kidogo Walutheri hawana 'misa' wana ibada.
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Jan 20, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Misa ndo 'mass' eeh?
   
 11. m

  mitishamba JF-Expert Member

  #11
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huwa nachanganyikiwa sana:
  1. Misa, Ibada, Huduma....
  2. Tumsifu Yesu Kristu, Bwana Yesu asifiwe
  n.k.
  Hivi nia ni kujitofautisha na mwingine au..!?
   
 12. m

  mitishamba JF-Expert Member

  #12
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaa.
  Na ibada inaitwaje?
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Jan 20, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,410
  Trophy Points: 280
  Church service? Maybe...
   
 14. m

  mitishamba JF-Expert Member

  #14
  Jan 20, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 697
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa mbona kuna baadhi ya madhehebu huwa yanasema tunaenda kwenye huduma badala ya misa au ibada.
   
 15. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #15
  Jan 20, 2012
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Pasco kule "mjengoni" ni lazima kuwe na migongano ya kiitikadi na kimawazo. Ukitaka huo "umoja" unaouona misibani uende hadi bungeni utakua unatuombea "tuliwe" mithili ya simba amlavyo swala, na watawala.Achana na mawazo ya namna hiyo.
   
 16. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Lowasa siyo waziri mkuu mstaafu.
  Bunge litusaidie kufafanua hili suala, marupurupu yake yafafanuliwe uhalali wake pia.
  Samahani pasco, just noticed.
   
 17. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hiyo imeachwa mahsusi kwa ajili ya magazeti kama mwananchi. Yatie chumvi ndipo wauze magazeti yao.
   
 18. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,631
  Likes Received: 904
  Trophy Points: 280
  Watanzania wameamka, ni upuuzi kusalimiana, muda wa kusalimiana upo au tuna muda wa kufanya kazi kukabiliana na mfumuko wa bei, Ajira kwa Vijana hakuna, KILIMO kwanza imekuwa kilio kwanza, wawekezaji uchwara wanapewa ardhi
   
 19. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Wakuu mnaonaje JF itoe tuzo kwa JK kutokana na mahudhurio na michango yake ktk misiba, sherehe na sikukuu? Naomba mnisaidie kusuggest jina la tuzo hii
   
 20. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2012
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  huo "mshikamano" mnaouita (hasa hao viongozi wa serikali na bunge).................. ndo kodi zetu zinatafunwa hivyo..................... kila uliyemtaja hapo ana "fungu" na pia atakamata "fungu" jingine atajkapohudhuria mazishi arusha.................... nyie mnaomboleza na kuzika wenzenu wanajiimarisha kuichumi...................... kwa kodi zetu........................ kweli kufa kufaana!!...................

  i hope na mh, pasco hakosi bahasha za hapa na pale hapo msibani..................... teh teh...................... nchi hii bana, .................. taaaaamu kwlikweli......................
   
Loading...