Mshahara wa mwezi Septemba kwa Watumishi wa Umma...

Pole mkuu umeandika kwa uchungu sana
 

Pole sana mtumishi mwenzangu naona umeandika ukiwa na uchungu kweli,ukweli tatizo linaanzia kwetu watumishi kwa kukubali kuburuzwa na muajiri wetu (serikali) na tumekaa tukitazama tu bila kujua kesho yetu.
Watumishi tukikosea mara zote muajiri anatuadhibu bila kusita ila yeye anakosea kwa miaka miwili sasa ila sisi tunaishia kutoa lawama kwenye mitandao ya kijamii tu,nilishawahi kusema hili kua tulipofikia tusijifanye WAZALENDO kwa Taifa hili ni uwendawazimu kujitoa na kufanya kazi kwa bidii kama hakuna anaejali maslahi yetu nawakumbusha kua tuna familia zinatutegemea tukiendekeza uzalendo tutawaacha masikini ni wakati sasa wa kumuwajibisha muajiri kwa vitendo sio maneno TUFANYE KAZI KADRI TUNAVYOLIPWA tusiwe waoga na hapo ulipo muibie tu muajiri hata MUDA tu inatosha maana anavyotuburuza alafu anapata matokeo chanya hashtuki ila anajisifia kua inawezekana uku kwetu nashukuru hata wale waliokua wanoko wamenyooka sasa tumekua kitu kimoja na tunapambana na adui yetu pamoja honestly sioni maumivu ya udhalimu wa muajiri kwa kua najua wapi nafidia.
 
aise kiukweli inauma sana ,kuona watumishi wanavyoteseka namna hii.
hela kwa mheshimiwa imekuwa ngum kutoka sijui kwanini!?
 
Watanzania daini katiba mpya vinginevyo mtapata tabu sana. Kuna kakikundi ka watu ndo kameifanya Tanzania yakwao.Wananeemeka na kila kitu.
Katiba si suluhisho pekee la matatizo ya watanzania, bado kuna kundi kubwa la watanzania wasiojitambua (elimu-less) na hawa ndio mtaji wa watawala, hufanya wanayojiskia wao huku wakiwa na uhakika wa kurudi madarakani bila kukataliwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…