Kila mtu anajua thamani yake. Wewe unajijua thamani yako kulingana na qualifications zako na uzoefu.
Ukiulizwa unataka kiasi gani taja unachoona ndio thamani yako kwa uzoefu na qualifications zako. Usiogope, kama wakiwa wapo chini mta negotiate.
Kusitasita kutaja na kujiumauma kunakupotezea points maana mwajiri anakuona kabisa hujui thamani yako.
Kwa hao waliosema kuwa umetaja kiasi kikubwa na wewe unaona ndio thamani yako na inaendana na vigezo nilivyotaja hapo juu unaweza ku negotiate kiasi ambacho utaona bado kina maslahi kwako lakini waambie baada ya muda fulani labda six months kuwe na increments kulingana na performance yako.