Wasalaam wanabodi.
Weekend iko safi kabisa wakati tukijiandaa kuuanza mwezi wa 12, mwezi ambao una mambo mengi ya kimaisha ambayo yote hukutana kwa wakati mmoja.
Mshahara wa mwezi Desemba huwa ni shida sana kuugawa.
Mshahara utaingia kati ya tarehe 22 mpaka 23 Disemba 2019.
Tarehe 25 Disemba ni sikukuu ya Christmas (kwa sisi wa upande wetu), siku hii hujawa na shamra shamra sana za kufufuka Bwana Yesu. Sherehe hutamalaki kila kona ya dunia. Yote haya huhitaji pesa.
Wiki moja baadae, January 1, 2020 ni sherehe ya mwaka mpya. Hii nayo ni kubwa sana kwa watu wa dini zote. Mbwembwe zote ni mwaka mpya. Hii sherehe inataka uwe na pesa.
Wiki moja baada ya mwaka mpya shule zinaanza kufunguliwa, ada kama zote. Maandalizi madogo madogo ya vitendea kazi vya shule vyote hutaka pesa.
Kuna kodi za nyumba, kodi za frame za biashara, leseni za biashara, fuel, michepuko na kadha wa kadha.
Kasungura kadogo mambo mia kidogo.