Mshahara wa Desemba: Christmas, mwaka mpya, ada na kodi

Mshahara wa Desemba: Christmas, mwaka mpya, ada na kodi

Hivi punde

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2017
Posts
2,554
Reaction score
8,627
Wasalaam wanabodi.

Weekend iko safi kabisa wakati tukijiandaa kuuanza mwezi wa 12, mwezi ambao una mambo mengi ya kimaisha ambayo yote hukutana kwa wakati mmoja.

Mshahara wa mwezi Desemba huwa ni shida sana kuugawa.

Mshahara utaingia kati ya tarehe 22 mpaka 23 Disemba 2019.

Tarehe 25 Disemba ni sikukuu ya Christmas (kwa sisi wa upande wetu), siku hii hujawa na shamra shamra sana za kufufuka Bwana Yesu. Sherehe hutamalaki kila kona ya dunia. Yote haya huhitaji pesa.

Wiki moja baadae, January 1, 2020 ni sherehe ya mwaka mpya. Hii nayo ni kubwa sana kwa watu wa dini zote. Mbwembwe zote ni mwaka mpya. Hii sherehe inataka uwe na pesa.

Wiki moja baada ya mwaka mpya shule zinaanza kufunguliwa, ada kama zote. Maandalizi madogo madogo ya vitendea kazi vya shule vyote hutaka pesa.

Kuna kodi za nyumba, kodi za frame za biashara, leseni za biashara, fuel, michepuko na kadha wa kadha.

Kasungura kadogo mambo mia kidogo.
 
Naunga mkono hoja.
Alafu pia una mwaka mzima kwanini usitenge kibubu cha akiba kidogokidogo kwa ajili ya hizo sikukuu.
Akili kinkichwa.

Jamii imeifanya km xmas km siku ya kuvaa nguo mpya na kula vyakula kibao..eish mm hata huwa sina kbs wazo hilo..bora ucelebrate new yr!
Kuna watu wazima kbs bila kutinga kiwalo kipya xmas haelewi kbs siju huwa ni nn jaman!
 
Naunga mkono hoja.
Alafu pia una mwaka mzima kwanini usitenge kibubu cha akiba kidogokidogo kwa ajili ya hizo sikukuu.
Akili kinkichwa.


Pia kutenga kibubu hili ni somo gumu sana kwetu hasa nchi za kimaskini kama Tz!.. Misiba, harusi, majanga !changamoto nyingi mnoo...sema ni kuishi uwezavyo sio wapendavyo!
 
Tarehe 25 Disemba ni sikukuu ya Xmas (kwa sisi wa upande wetu)...siku hii hujawa na shamrashamra sana za kufufuka Bwana Yesu..sherehe hutamalaki kila kona ya Dunia. Yote haya huhitaji pesa..

mkuu ni kuzaliwa kwa Bwana Yesu
 
Tarehe 25 Disemba ni sikukuu ya Xmas (kwa sisi wa upande wetu)...siku hii hujawa na shamrashamra sana za kufufuka Bwana Yesu..sherehe hutamalaki kila kona ya Dunia. Yote haya huhitaji pesa..

mkuu ni kuzaliwa kwa Bwana Yesu


Alafu wabobezi wa Bible wanasema Massiah hakuzaliwa dec..alizaliwa around july!
 
Tuwe na tabia ya kutenga fedha kwaajili ya mapumziko na sherehe kama hizo, vingenevyo january itabaki kuwa mwezi mgumu.
 
Back
Top Bottom