Mshahara wa Dereva wa Mbunge usipitie kwa Wabunge, baadhi wanawanyonya, hawawalipi inavyotakiwa

Mshahara wa Dereva wa Mbunge usipitie kwa Wabunge, baadhi wanawanyonya, hawawalipi inavyotakiwa

BungeLetu

New Member
Joined
Feb 4, 2026
Posts
3
Reaction score
6
Kuna tetesi kuwa baadhi ya Wabunge wetu huwa wana kawaida ya kuwanyonya madereva wao kwenye suala la mishahara kwa kuwa inapitia kwao Wabunge.

Nashauri kama inawezekana mshahara wa dereva upite moja kwa moja kutoka Bungeni uingie kwenye account ya dereva.

Ipo hivi mshahara na posho ya dereva wa Mbunge unapitia kwenye account ya Mbunge mwenyewe, hivyo sasa kima kilichopangwa na Bunge ili dereva apewe, kinachotokea wao Wabunge baadhi hawatoi kile kima, wanatoa kima cha chini sana.
 
Wabunge wa mbogamboga hawajawahi kutosheka na ukubwa wa vitambi vyao.
 
Kama hili linaukweli basi tupo kwenye nchi ya ajabu sana!
 
Unapokea milioni 18 kwa mwezi ,maposho ya kamati kama yote ,mapesa ya ziara kama yote ,mapesa ya warsha ,makongamano ,mapesa ya uchawa kuchangia bajeti kama yote lakini bado hawatosheki ,wanashindwa kumlipa milioni moja na laki 5 Dereva? Haiwezekani Dereva wa Mbunge awe na njaa ni hatari kwa Mbunge.
 
Huu ndio utofauti wa mtu mwenye akili timamu na mjinga, hivi dereva unapo mpunja mshahara hawaoni kuwa wanarisk maisha yao?
 
Huu ndio utofauti wa mtu mwenye akili timamu na mjinga, hivi dereva unapo mpunja mshahara hawaoni kuwa wanarisk maisha yao?
Kuna watu unatakiwa wasiwe wanahudhika hata kidogo ,wasaidizi wako inabidi wawe happy kwa kuwalipa vizuri ,ukiwalipa vibaya ni hatari kukuumiza either kukuibia/kukupiga au kula njama na wabaya wako na kukumaliza/kukudhuru maana huna faida.
 
Back
Top Bottom