Mshahara vipi wafanyakazi wa serikali??

kaeso

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
551
96
Dah!! madeni yamenizonga na sasa tumeanza mwezi mwingine. Kuna yeyote ana taarifa kwa nini tumecheleweshewa mshahara?? Nasikia wengine wamepata ila sisi hata dalili hakuna, kila unayemuuliza anakuwa mkali...
 
Nasikia mtalipwa January mkuu kwa mshahara wa Mwezi wa Novemba na December. Mnakopwa ili kulipia sherehe za miaka 50 ya uhuru na kulipia maposho ya wabunge na viongozi wakuu serikalini na safari zao za mamtoni vumilia au karibu sekta ya binafsi.
 
Du ina maana wakina muraaaa hawajalipwa? Wafanyakazi wa wizarani hawajalipwa? Acheni kazi muje sector binafsi mambo hayo hakunaga kwasababu yanajiendesha kibiashara zaidi huko kwenu mnajiendesha kisiasa nendeni mkakope tena CRDB au Stanbic,mara elfu niende kulima kijijini kuliko kufanya kazi sirikalini,mtoto wa msoga kaaribu kila kitu kipindi cha mkapa kila mtu alitaka kufanya kazi sirikalini:::poleni sisi tushapokea tangia tar 24
 
Umeshatoka nmb labda ninyi wa crdb nk ndo mtaendelea kusota kwa siku mbili
 
Zikiingia mtaniambia, mimi bado natumia posho niliyodaka kwenye semina ya siku nne tu.
 
serikali inaelekea pabaya suala la kutolipa mshara wa wafanyakazi ni kuwafanya waishi maisha magumu
 
Piga moyo konde kuna mzigo umeingizwa leo wameamua kuchapisha noti ulaya
CCM Oyeeeeeeeee!
 
Serikali ina fedha bwana, kama hujapata basi ni compyuter tu ndo iliyokorofisha. Jana watu kama aslimia 70% kutoka halmashauri yetu walipata, ile 30% waliambiwa wasubiri kidogo na watalipiwa dirishani. Fedha ipo, tena nyingi msiwe na wasi wasi
 
Mlipoambiwa wakati wa kampeni 2010 kuchagua magamba ni janga, hamkuamini. Na huo ni mwanzo, makubwa mtayaona tuendako. Wenzenu sasa hivi wanavuana magamba utafikiri hayo magamba matatu ndio yameifikisha hii nchi hapa tulipo.
 
Hiyo ndiyo CCM Mzalendo jitahidi,kama unalipwa 7,000/=kwa siku ondoka kazini kabla ya muda nenda kasake 7000/=ingine.Serikari haina shukrani utakufa ukasifiwe mazishini.
 
Watumishi wa umma ndiyo wanatumiwa kuichakachua nchi.Onjeni joto kidogo ili tuungane kusaka Tanganyika(haki) yetu
 
Wafanyakazi wa "Serikali" huwa mnafanya "kazi" gani? Vikao, Semina, Safari, e.t.c - hamstaili kulipwa!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom