Msemakweli amzidi kete DPP;

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,443
18,453
Mahojiano ya awali yaliyokuwa yakifanywa na kikosi kazi kinachoundwa na maofisa kutoka vyombo vitatu vya dola dhidi ya Mwanasheria na Mwanaharakati maarufu nchini, Kainerugaba Msemakweli, kuhusu sakata la Kampuni ya Kagoda Agriculture Limited kukwapua Sh. bilioni 40 za Epa, yamefikia tamati, huku mwanaharakati huyo akigoma kutoa ushahidi wa nyaraka za serikali na kumuomba Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP) ampe kinga.
Msemakweli, ambaye mwaka jana aliwataja baadhi ya mawaziri na wabunge kuwa ni mafisadi wa elimu kutokana na kudanganya elimu zao, alikuwa akihojiwa na kikosi kazi hicho kuhusu ushahidi alioibuka nao wa kuipeleka mahakamani kampuni ya Kagoda.
Kagoda inatuhumiwa kukwapua Sh. bilioni 40 kati ya Sh. bilioni 133 zilizoibwa na kampuni nyingine 22 katika Akaunti ya Madeni ya Nje (Epa) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Kikosi kazi kilichomhoji Msemakweli kinaundwa na maofisa waandamizi kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru), Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Jeshi la Polisi.

Mahojiano hayo yaliyoanza rasmi Septemba 7, yaliendelea juzi kwa saa tano na kuhitimishwa jana, baada ya kikosi kazi hicho kufanya mahojiano ya utangulizi na Msemakweli kuhusu ushahidi huo, Septemba 3, mwaka huu.

Habari za uhakika ambazo NIPASHE ilizipata zilithibitisha kufanyika kwa mahojaino hayo kuanzia juzi hadi jana.

Akizungumza na NIPASHE jana, Msemakweli, alisema aligoma kutoa nyaraka hizo kwa kikosi kazi hicho jana ili kukwepa mambo yasije kumgeukia baadaye na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki nyaraka za serikali, kinyume cha sheria.

Hata hivyo, alisema baadhi ya nyaraka alizitoa kwa kikosi kazi hicho ukiwa sehemu ya ushahidi wa kuipeleka Kagoda mahakamani.

“Mahojiano ya awali yamemalizika leo (jana), yamekwenda vizuri. Ila kuna tatizo limejitokeza. Nimegoma kutoa nyaraka za serikali zisije zikanigeukia nikashtakiwa nimezipata wapi,” alisema Msemakweli.

Aliongeza: “Nimewaambia (kikosi kazi) nitakuwa tayari kutoa nyaraka hizo mpaka nitakapohakikishiwa kwa maandishi kwamba sitashtakiwa. Kwa hiyo, document (nyaraka) muhimu bado ninazo.”

Kutokana na hali hiyo, alisema leo atamwandikia Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) barua kumtaka amthibitishie kwa maandishi kwamba, hatashtakiwa iwapo atatoa nyaraka hizo kwa kikosi kazi hicho.

Alisema atachukua hatua hiyo kwa kuzingatia Sheria ya Usalama wa Taifa sura ya 104, ambayo inatoa utaratibu wa jinsi ya kutoa nyaraka za serikali.

Miongoni mwa mambo aliyokieleza kikosi kazi hicho katika mahojiano hayo yalihusu kwamba analijua suala la Kagoda kwa kina na anao ushahidi wa kuipeleka mahakamani na kwamba, yuko tayari kuupeleka ushahidi huo mbele yao (kikosi kazi).

Hatua hiyo ilichukuliwa na vyombo vya dola, siku chache, baada ya Msemakweli, kuwasilisha ushahidi huo kwa Ofisi ya DPP.

Yalifanyika saa chache, baada ya Msemakweli kukutana na DPP, Elizer Feleshi na Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Manumba, ofisini kwa DPP siku hiyo.

Kwa mujibu wa Msemakweli, alikwenda siku hiyo kwa DPP baada ya kuitwa na Feleshi kwa ajili ya mazungumzo kuhusu ushahidi aliouwasilisha ofisini kwake.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Mrakibu Msaidizi (ASP) Advera Senso, alithibitisha wiki iliyopita kuwa uchunguzi kuhusu ushahidi alioibuka nao Msemakweli unaendelea.

Mahojiano hayo yalikuwa yakifanyika katika Ofisi za Kikosi Kazi (TFO) zilizoko Mikocheni, jijini Dar es Salaam.

Septemba 2, mwaka huu, Msemakweli, alikutana na waandishi wa habari na kuwaeleza kuwa amefanya uchunguzi na kupata ushahidi unaoweza kuipeleka Kagoda mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi zinazoikabili.

Msemakweli alisema ushahidi huo aliuwasilisha kwa DPP.

Alisema katika ushahidi wake huo kwa DPP, amewataja wamiliki saba halali wa kampuni hiyo, wakiwamo wafanyabiashara Yusufu Manji na aliyekuwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz.

Msemakweli alisema pia aliwasilisha kwa DPP baadhi ya vielelezo vinavyoonyesha kwamba wahusika hao saba waliratibu na kuiba dola za Marekani milioni 30.7 kutoka Epa.

Alidai amefanikiwa kukusanya na kufahamu ushahidi unaowaunganisha moja kwa moja Rostam, Manji, Gulam Chakaar, Bahram Chakaar, John Kato, Barati Goda na Tabu Omary, kuwa ni wahusika wakuu katika wizi huo.
CHANZO: NIPASHE
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,443
18,453
Shule nzuri sana unapojua ulifanya nini tukonyuma ako msemakweli hata wakikupeleka keko tutakuletea mihogo huko huko mwaya mungu akutangulie uwe na hekima kujjuua jinsi ya kuwapatia hizo data
 

Shine

JF-Expert Member
Feb 5, 2011
11,483
1,360
Nia ya hiyo timu kazi ni nini? Kuwatetea watuhumiwa au kujua undani wa suala hilo kabla yakuwapeleka mahamani?
 

Ndoano

Senior Member
Aug 9, 2011
192
31
Msemakweli, Mungu akupe nguvu na hekima ya kutetea maslahi ya taifa kwa manufaa ya vizazi vijavyo
 

luckman

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,211
371
we sio PDIDY, nilidhani utasema, wakikupeleka huko tutapambana kukutoa kumbe kumpelekea mihogo! miafrika ndivyo ilivyo!
 

Emanuel Makofia

JF-Expert Member
Jan 5, 2010
3,839
628
chonde chonde mskweli
usije kubali kupoozwa na vijisenti kisha mambo haya yakaisha!
tuko nyuma yako,
 

Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,159
4,435
Kweli nchi hii inaongozwa kisanii, Sitaki kuamini kwamba jeshi la Polisi linatumia mamilioni ya shilingi kila siku, lakini linashindwa kazi ya kusaka ushahidi na Msemakweli. Kama msemakweli anaweza kusubutu kutafuta ushahidi kwa kutumia visenti vyake wanashindwaje Polisi kutumia pesa ya walipakodi kutafuta ushaihidi?
 

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
48,443
18,453
we sio PDIDY, nilidhani utasema, wakikupeleka huko tutapambana kukutoa kumbe kumpelekea mihogo! miafrika ndivyo ilivyo!

unajua wanasheria atuwapagi majibu mapema unaweza kutangza kumtoa mwenzio anakazia hukumu so unatakiwa kuangalia hali yake ya afya kwanza akiwa gerezani huku njia za kumtoa zikifanyika kwa siri..else utamwaga maji hadharani mpwa
pole
 
Aug 19, 2011
53
4
komamaa kama kawa wadosi tumewakalibisha balazani wameingia mpaka chumbani unategemea nini?manji anasema anatumia pesa za babu yake kumbe babu yake ni selikari??? MWISHO INATOSHA KAMATA MWIZI MEN!
 

Rweye

JF-Expert Member
Mar 16, 2011
16,891
7,390
Nchi hii ni zaidi ya maigizo yaani ndani ya miezi michache matukio ya kufa mtu,ni tukio juu ya tukio

Tuyaangalie jamani; kujivua gamba (ccm), madiwani kupigwa chini (arusha),Rostam ni gamba (Nec-ccm),bunge ni kama zecomedy (Jairo),mafuta kupanda bei (baraza la mawaziri),kuhonga bunge (wizara ya nishati),kushushwa bei za mafuta (Nec-ccm),Jairo kurudishwa kazini kwa vigelegele (Luhanjo),Rostam kusaidia kampeni Igunga (ccm),spika kukalia hoja mahususi (bunge),Mgao wa umeme kupungua kuanzia sept (Ngeleja),Jairo kuondolewa kazini tena (Ikulu),kurudishwa kazini madiwani-arusha (Mkuchika),siku ya 5 ni giza (arusha-sept),ajali ya meli,maombolezo kitaifa siku3 (Rais),miss voda Tanzania (siku ya maombolezo kitaifa),maombolezo siku3 ni visiwani tu (TBC)....nahisi kizunguzungu jamani endeleeni
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom