Msemaji wa Serikali Dk. Abbasi atunukiwa Cheti cha Uprofesa nchini China

Hongera sana Dr Abbas Msemaji wa serikali kipaji kilichoibuliwa kipindi cha awamu ya Tano
 
Mnaoponda humu ndani hata certificate wengine hawana .....this is bong land of idiots


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
China ndiko vitokako vyote vilivyo fake, hata Baba Prince alipewa lakini haivumi
 
Walishatujua sisi ni walevi wa PhD na Profesorioism, wao hata wakiwa nazo huoni wakijiita vile hadharani lakini kwetu ni utukufu na fahari hata kama haina tija fahari ndiyo satisfaction
 
Kwanini wasimtunuku cheti cha Uprofesa wa Fotoshop
Maana alitudanganya kwa kutuwekea SGR ya Kenya na kutuaminisha kuwa ni ya Magufuli.
 
View attachment 912118
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi, ametunukiwa cheti cha Uprofesa wa Muda (Part Time and Research Professor) katika Kitivo cha Lugha na Utamaduni wa Kigeni katika Chuo Kikuu cha Mawasiliano na Habari cha China (China Communication University). Tuzo hiyo imetolewa na Mkuu wa Kitivo hicho kwa kutambua mchango wa Dkt. Abbasi katika tasnia ya habari, utafiti na lugha ya Kiswahili.

Akizungumza wakati wa hotuba yake chuoni hapo kuhusu hali ya sekta ya habari nchini Tanzania, Dkt. Abbasi amesema kuwa vyombo vya habari vina wajibu wa kusaidia maendeleo ya nchi na kuwa chachu ya amani na si vurugu. "Sisi kama wanahabari au vyombo vya habari tunapaswa kuwa na weledi na wajibu wetu mkuu ni kusaidia maendeleo ya nchi na si kuzigawa jamii au kuzitofautisha. Waandishi wa habari wa hapa China ni mfano mzuri wa kile ninachokiita uandishi wa habari za kimaendeleo na si za kimapokeo " amefafanua Dk. Abbasi.

Aidha, Dkt. Abbasi ameshauri vyombo vya habari nchini Tanzania kutobaki na mfumo mmoja wa utoaji taarifa bali kujiimarisha katika mifumo mingine ya kidigitali kwani dunia imehama kutoka analojia kwenda digitali.
Kumbe china niridhani ni nchi
Inayoangalia uhakisia sio fursa.

Kwa huyo jamaa hamna kitu hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom