GE2025 Msemaji wa Polisi: Hakuna tishio lolote la kiusalama lililobainika hadi sasa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime, amethibitisha kuwa hali ya usalama nchini ni shwari na salama, akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vyao vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba.

Akizungumza leo, Oktoba 29, 2025, kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, Misime alisema hakuna tishio lolote la kiusalama lililobainika hadi sasa.

“Niendelee kutoa wito kwa wananchi wajitokeze bila hofu katika vituo vyao. Askari wapo kimsingi katika vituo vyote kuhakikisha usalama wa kutosha. Tutahakikisha kazi hii inafanywa kwa weledi, busara na haki kubwa ili wananchi watekeleze haki yao ya kupiga kura,” alisema Misime.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limeandaa mikakati madhubuti kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu kote nchini.

huu ni uhodari wa hali ya juu kwa jeshi letu wallah

wazalendo wako salama huku wakitimiza haki yao kikatiba kazi na utu ndio msingi wa taifa
 
Tatizo uchaguzi umesha kufa KIBUDU ...sasa hivi ccm itaanza kutafuta wanaccm kwenye mabasi
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime, amethibitisha kuwa hali ya usalama nchini ni shwari na salama, akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vyao vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba.

Akizungumza leo, Oktoba 29, 2025, kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, Misime alisema hakuna tishio lolote la kiusalama lililobainika hadi sasa.

“Niendelee kutoa wito kwa wananchi wajitokeze bila hofu katika vituo vyao. Askari wapo kimsingi katika vituo vyote kuhakikisha usalama wa kutosha. Tutahakikisha kazi hii inafanywa kwa weledi, busara na haki kubwa ili wananchi watekeleze haki yao ya kupiga kura,” alisema Misime.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limeandaa mikakati madhubuti kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu kote nchini.

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, David Misime, amethibitisha kuwa hali ya usalama nchini ni shwari na salama, akiwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika vituo vyao vya kupigia kura ili kutimiza haki yao ya kikatiba.

Akizungumza leo, Oktoba 29, 2025, kwenye kipindi cha Jambo Tanzania cha TBC1, Misime alisema hakuna tishio lolote la kiusalama lililobainika hadi sasa.

“Niendelee kutoa wito kwa wananchi wajitokeze bila hofu katika vituo vyao. Askari wapo kimsingi katika vituo vyote kuhakikisha usalama wa kutosha. Tutahakikisha kazi hii inafanywa kwa weledi, busara na haki kubwa ili wananchi watekeleze haki yao ya kupiga kura,” alisema Misime.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi limeandaa mikakati madhubuti kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu kote nchini.

Kwahiyo TISS waliwaingiza chaka.
 
Imenikumbusha Comical Ali

1000152719.jpg
 
Back
Top Bottom