Johnny Sack
JF-Expert Member
- Jan 21, 2017
- 8,984
- 19,287
Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Emmanueli Eligaisha amesema wafanyakazi 134 waliiondolewa Muhimbili hawajaleta madhara yoyote kwa wagonjwa kwa kuondolewa kwao kwa kuwa walikuwa wamejipanga kutoa huduma kwa dharura.
Sababu iliyowarahisishia kukava nafasi zao ni kuwa wametoka katika maeneo mblimbali na sio eneo moja.
Kati ya 134 madaktari ni 2, wauguzi ni 68, maabara 10, famasia 2, kumbukumbu wagonjwa 11, wahudumu wa afya 19 na kada nyingine watu 22.
Pia amesema kuwepo kwa watumishi hao hakujawahi kuzorotesha huduma ya matibabu na anayedai hakupewa huduma bora aende na ushahidi.