Msemaji wa muhimbili hajui wajibu wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msemaji wa muhimbili hajui wajibu wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by meningitis, Jul 8, 2012.

 1. meningitis

  meningitis JF-Expert Member

  #1
  Jul 8, 2012
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 8,020
  Likes Received: 911
  Trophy Points: 280
  [h=6]
  Irene Mark Tanzania daima


  KAMUSI ya Kiswahili Sanifu inaeleza maana ya neno ‘Mjinga’ kuwa ni mtu asiyefahamu kitu au jambo fulani; ****, jura, gulagula, bozi, mpumbavu au ****, nami napenda kumpachika neno hilo msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

  Nimelazimika kuanza na tafasiri ya neno mjinga nililolitumia hapo juu nikiamini kwamba ujumbe huu utamfikia mhusika na wakubwa wake ili waone namna ya kurekebisha utaratibu wa mambo.

  Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inacho kitengo cha habari ambacho kwa sasa kinaongozwa na Aminieli Bubelwa Eligaesha. Huyu ni mtumishi wa umma ambaye kwa mtazamo wangu hajui majukumu yake wala kazi muhimu za kitengo alichopo.

  Ninasema hivyo kwa sababu tangu Juni 23 mwaka huu, Jumuiya ya Madaktari Tanzania ilipotangaza mgomo kwa madai ya kuishinikiza serikali iwaboreshee mazingira ya kazi, vifaatiba, mashine za kisasa, nyongeza ya posho na mishahara madaktari hapa nchini waandishi wa habari nao wamekumbana na urasimu wa watendaji wa Hospitali ya Muhimbili.

  Kutangazwa kwa mgomo huo kuliyumbisha huduma hospitalini hapo licha ya ukweli kwamba si madaktari wote waliogoma lakini kwa sababu wengi wao wameungana na wenzao kwenye mgomo huduma za tiba zilitetereka.

  Kutokana na unyeti wa huduma zinazotolewa kwenye hospitali hiyo ya taifa ilimpasa ofisa habari huyo mwandamizi kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu kuyumba kwa huduma za tiba hospitalini hapo badala ya kuendeleza propaganda za kisiasa zisizo na tija kwa jamii.

  Aminieli anadiriki kuandika taarifa kwa vyombo vya habari jioni ya saa 12 na kuituma kwenye vyomba hivyo akiwataka wananchi kufika hospitalini hapo kupata tiba kwa kuwa hakuna mgomo, ni jambo la hatari kitaaluma.

  Ni uongo wa mchana aliotaka kuuficha kwa kuwahadaa wahariri ambao hawakufika eneo la tukio, kwangu alichokifanya ofisa huyo ni kuwachochea waandishi walioshinda MHN na kuzungumza na madaktari, wagonjwa, wauguzi na madaktari wanafunzi ambao walikiri kuwapo kwa mgomo hospitalini hapo.

  Ni uongo wa kitoto alioufanya Aminieli wa kuandika taarifa akieleza kwamba hakuna mgomo. Jambo hilo ni kinyume cha maadili ya uandishi.

  Aminieli ni ofisa habari mjinga ndiyo maana hataki kuulizwa swali na waandishi wa habari, anachojua ni kuandika taarifa zisizo na ukweli na kuzipeleka kwa wahariri wa vyombo vya habari ili kumridhisha bosi wake.

  Si kazi ya ofisa habari kukaidi kueleza ukweli, ndiyo maana yupo hapo na kwa kufanya hivyo anaua taswira njema ya taasisi nyeti kama hospitali hiyo ya taifa.

  Hakuna asiyefahamu kwamba taifa lenye maendeleo lazima liwe na watu wenye afya njema, sina hakika kama Aminieli analifahamu suala hili au kwa sababu wagonjwa wanaomhusu wanatibiwa nje ya hospitali hiyo wakati wa mgomo ndiyo maana anawahadaa Watanzania waendelee kujazana MNH wakati hakuna huduma?

  Kila nikimtafakari ofisa huyu anakaidi agizo la Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fenela Mukangara, alilolitoa hivi karibuni wakati akiwafunda maofisa habari wa umma, alipowazuia kuacha kukalia taarifa kwa masilahi ya umma.

  Aina hii ya maofisa habari hawastahili kuendelea kuwapo kwenye nafasi zao kwa sababu wanawasumbua wananchi pasipo sababu za msingi na kuwafanya wananchi wasiviamini vyombo vya habari.

  Waandishi wa habari hupata ushirikiano na taarifa sahihi kutoka kwa Jezza Waziri, ambaye kwa sasa hana uwezo wa kuzungumza kwa kuwa Eligaeshi ni kiongozi wa ofisi hiyo.

  Nashindwa kuelewa kwa nini ofisa huyu aliyekosa hekima asiige mfano wa Ofisa Habari wa Kitengo cha Mifupa hospitalini hapo (MOI), Almas Jumaa, ambaye yupo tayari kuwapeleka wodini waandishi ili wajionee hali halisi ya utendaji wa ofisi hiyo!

  Ninaamini kwamba ofisa habari bora ni yule aliyewahi kufanya kazi kwenye chombo chochote cha habari, kwa sababu wanajua umuhimu kazi hiyo kwa jamii, wanaelewa athari za kupotosha jamii.

  Ninaushauri uongozi wa MNH kufanya mabadiliko ya kitengo hicho ili kuboresha taswira ya hospitali hiyo ya taifa.

  imarkmeero@yahoo.com 0784 19 00 66
  [/h]
   
Loading...