Msemaji Serikali ya Israel: Mwili wa Mtanzania Joshua unashikiliwa na Hamas

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,639
15,970
Habari wana jukwaa la kimataifa. Hii ndio habari iliyotangazwa leo saa 2 usiku katika taarifa ya habari Azam. Msemaji wa serikali ya israeli ameutangazia umma wa watanzania kuwa mwili wa Joshua mollel aliyetekwa na kundi la Hamas tarehe 7.10.2023 huko Israeli ulichukuliwa mateka na kundi hilo na kwamba kwa sasa eti mwili huo upo Gaza mikononi mwa Hamas.

Nina maswali machache sana ya kuuliza kwasasa.

1. Hamas waliwazaje kuuteka mwili wa mtu ambaye tayari wameshamuua ndani ya israeli na kumpeleka Gaza huyu mtu ana umuhimu gani sana kwenye hii vita? Tuzingatie waliuliwa 1400 siku hiyo

2. Tunavyofahamu mpaka sasa Gaza hakuna umeme , hospitali zimebomolewa je Hamas watakua wameuweka wapi mwili wa ndugu yetu ikizingatiwa leo ni siku zaidi ya 70 tangu auwawe? Je mwili bado upo?

3.kwanini Hamas katika taarifa zao za mateka waliokufa wakishikiliwa hawajamtaja Joshua?

Jamani naomba ndugu zangu nauliza haya maswali kwa nia njema tu sijaleta vita.najua watanzania hatupendi kuulizwa maswali lakini tujitahidi kufikiria mambo kwa kina hasa tunapokuwa ni watu wa kupokea taarifa kutoka nje.

Karibuni kwa mjadala wa kistaarabu. Moderators na Maxence Melo mkuu naomba wasifute uzi wangu tujadili tu mbona sijavunja sheria yeyote?

Ahsante.
 
Haya mambo yanafikirisha, mkiona mpaka mzazi wa marehemu kaamua kwenda kupambania mwenyewe kuhusiana na kifo cha mwanaye huku serikali iliyoapa kulinda raia wake ikikaa kimya kama vile hamna kilichotokea au ni kuku kapoteza maisha basi mjue kuna shida kubwa sana kwenye utawala wa hii nchi
 
Msemaji wa Hamas aliweka wazi mauaji ya raia wa nchi zingine waliowateka ni Salam kwao kwamba kumpeleka raia wao Israel ni hatari. Na wao wapo vitani na Kila mshirika wa Israel.

Sasa kama walimteka na amafariki wakiwa nae, unataka Israel waseme Wana mwili wake?

Kumbuka kama alikua ameenda Israel Kwa kufuata taratibu zote, serikali yetu itataka kujua Nini kimejiri na mwili wake uko wapi. Lazima Israel watolee ufafanuzi.

Wewe unachopinga ni kipi, kwamba hajatekwa na Hamas, hajauwawa na Hamas au mwili wake haupo mikononi mwa Hamas?
 
Soma tena mkuu hilo bandiko hapo juu naona hujaelewa vzuri
 
Wameenda kusoma kilimo?
paslaingoodstar_1703102325348428.jpg

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Utawala wa nchi si upo pamoja na palestina na wapalestina si pamoja na Hamas sisi wananchi tusemeje sasa.

Japo hiyo video ya Jo inafikirisha lakini waislamu baadhi kufurahia kifo cha Joshua Mollel inafikirisha zaidi

Ni watu wanamna gani hawa waislamu kati lbgtq na waislamu ni kundi gani hatari zaidi kwa binadamu wengine

Maana kama Jo angetekwa na mashoga yawezekana angekuwa hai mpaka wakati huu
Lakini katekwa na watu wa allah akbar wakammiminia risasi hadharani na sasa wanakuja na propaganda kuwa yule mkulima alikuwa mwanajeshi wa Israel.
 
Habari wana jukwaa la kimataifa. Hii ndio habari iliyotangazwa leo saa 2 usiku katika taarifa ya habari Azam. Msemaji wa serikali ya israeli ameutangazia umma wa watanzania kuwa mwili wa Joshua mollel aliyetekwa kundi Hamas tarehe 7.10.2013 huko Israeli ulichukuliwa mateka na kundi hilo na kwamba kwa sasa eti mwili huo upo Gaza mikononi mwa Hamas.

Nina maswali machache sana ya kuuliza kwasasa.

1. Hamas waliwazaje kuuteka mwili wa mtu ambaye tayari wameshamuua ndani ya israeli na kumpeleka Gaza huyu mtu ana umuhimu gani sana kwenye hii vita?

2. Tunavyofahamu mpaka sasa Gaza hakuna umeme , hospitali zimebomolewa je Hamas watakua wameuweka wapi mwili wa ndugu yetu ikizingatiwa leo ni siku zaidi ya 70 tangu auwawe? Je mwili bado upo?

3.kwanini Hamas katika taarifa zao za mateka waliokufa wakishikiliwa hawajamtaja Joshua?

Jamani naomba ndugu zangu nauliza haya maswali kwa nia njema tu sijaleta vita.najua watanzania hatupendi kuulizwa maswali lakini tujitahidi kufikiria mambo kwa kina hasa tunapokuwa ni watu wa kupokea taarifa kutoka nje.

Karibuni kwa mjadala wa kistaarabu. Moderators na Maxence Melo mkuu naomba wasifute uzi wangu tujadili tu mbona sijavunja sheria yeyote?

Ahsante.
unafikiri walienda pale kwa mguu? mbona akili yako ndogo sana.
 
Pia ndugu mpenda haki mwenzangu tujiulize, huu mwili wa mtanzania mwenzetu unashikiliwa sehemu gani haswa ndani ya Gaza wakakati tunaambiwa Gaza yote kwa sasa ipo chini ya jeshi la Israel?

Hatuoni kwamba ni maigizo yaleyale ya serkali dhalimu ya Israel kwamba ndugu yetu Joshua mollel aliuawa na Hamas kumbe aliuawa na wayahudi wenyewe ili kutafuta attention duniani?

Tafakari
 
Nashukuru mungu mwakani natimiza miaka 5 ya kuwa raia wa kudumu ndani ya taifa hili la fursa.
Naukana uraia wangu kwa maslahi mapana ya watoto wangu na familia yangu ya baadae.
Serekali ya hii nchi ipo serious juu ya raia wake, na hili limenivutia kubadili uraia.
Motherland tutaiheshimu daima na tutarudi baadae kuipigania.
Poleni waTanzania wote na familia ya wafiwa.
 
Nimeamini Tanzania kuna magaidi mengi sana, na mengi pia yapo humu jf. imagine watu wanaweka sura ya mtu mwingine kabisa na kusema ni sura ya Joshua Molel na Clement Mtenga waliouawa Israel, ili tu awasafishe Hamas waonekane walifanya sahihi kuwauwa. cha muhimu mmekubali hamas waliwauwa na sio israel, kilichobaki hangaikeni kutafuta picha ili kuwasafisha kwenye mitandao, ila kule israel wanakamatwa, wanaogeshwa na kupakwa mafuta, na kuvalishwa nguo mpya.
 
Back
Top Bottom