Msemaji Mkuu .... si Spika ...

klf

Member
Jun 12, 2009
58
95
Kwa kweli hatua ya kumchagua Anna Makinda hivi (hongera sana) karibuni yanikumbusha namna hadhi ya Bunge na ya lugha ya kitaifa kitakavyokuwa kitaboreka ikiwa tungeachilia mbali desturi ya kutumia neno hiki la "Spika". Mbona hatufanyi maamuzi mahali pake pachukukliwe na "Msemaji Mkuu"?
Wabunge wengine wajulikane kila mmojaa kama "Msemaji" lakini cheo cha juu kipewe heshima ya kuitwa "Msemaji Mkuu". Kwa njia hii, mimi nafikiri wadhifa ya cheo hicho itapewa heshima inayostahiki. Ilibidi kuondoa mabaki ya kizamani ikiwa istilahi ya kisiasa ya asili ya kileo yanapatikana kwa urahisi.
 

MKUNGA

JF-Expert Member
Dec 10, 2009
441
195
Kuitwa spika ni sahihi kwani duniani hamna lugha iliyojitosheleza. Hata hicho Kiingereza kimekopa maneno mengi kutoka katika lugha nyingine. ni sahihi kuendelra kuitwa spika.
 

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,398
1,250
Neno 'Speaker' katika kiingereza ni mojawapo katika yale ambayo yana maana zaidi ya moja. Maana (tafsiri) mojawapo ni 'mzungumzaji' (na sio msemaji, 'spokesperson/spokesman'), na nyingine ndiyo hiyo ya mratibu wa mijadala ya bunge.
 

klf

Member
Jun 12, 2009
58
95
Si vigumu sana kutofautisha baina ya "msemaji" na "mzungumzaji" na matumizi mengine mengi yenye uhusiano na utumiaji wa maneno. Ufunguo ndio muktadha yenyewe.
Tungalitumia "msemaji mkuu" kutoka mwanzo hatungekuwa na swali hili sasa. Utohozi wa maneno afadhali tuepukane hadi raslimali (hazina) za asili za lugha mama zepekuliwe kwa kina.
Pamoja na yote, mara nyingi tabia ya kuazima maneno katika lugha geni huashiria uzembe sio ukosefu wa malighafi la kilugha la kiasili.
Awali ya yote, tuchimbe kwenye migodi ya kitaifa kuliko kuingiza kutoka nje. Kama tukishindwa basi huu ndio wakati wa kuazima maneno yahusikanayo na utamaduni mwingine.
Labda hatuna budi kuzingatia hekima ya methali "Usiache mbaachao kwa mswala upitaao".....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom