Hapa CCM wamelamba dume, wamecheza! Naona wameamua kuwa serious kidogo. Uzuri kwetu na ubaya kwao ni kwamba huyu mzee siasa za majukwaani haziwezi kabisa, akina Mnyika watamnyanyasa sana. He is more of an intellectual than a politician. Sanasana atawasaidia kuwaandikia ccm mashairi lakini sio kukomboa majimbo kama mzee Malecela!
Kitila,
Kwa wakati huu, CCM walikuwa wanahitaji kiongozi makini, sio mpiga Debe, wananchi siku hizo wanayaona na kuyasikia wenyewe kwenye vyombo vya Habari, hawahitaji mpiga debe mwingine...
Nadhani pia CCM itafaidika kutoka kwa Msekwa kwa kuweza kudumisha demokrasia ndani ya chama chao,,, maana mtu ambaye amekuwa bungeni kwa miaka yote,,, nadhani hatapenda majungu sana...
Lakini la muhimu tunahitaji demokrasia idumu vizuri pia kwenye vyama vingine vya siasa sidhani huyu mzee atakuwa mtu mbaya...
Kwangu mimi naona ni BEST kutoka kwa wote waliotajwa... ingawa JF inaweza kuja na kashifa zake,,, lakini at least hatukuzisikia kashifa hizo tangu aastaahafu...
Dalili ni kwamba baada ya mkutano mkuu,,, pia katibu mkuu atakuwa mtu mzuri,,, maana Mwenyekiti,na Makamu wake wawili ndio hao watakao pendekeza katibu mkuu!!!