Msekwa angoja nini kujivua gamba? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msekwa angoja nini kujivua gamba?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Aug 23, 2011.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Kufuatia wabunge kumtaja wazi wazi Makamu Mwenyekiti wa CCM kuwa anahusika na udalali wa viwanja vya kujenga mahoteli katika njia za kupita wanyama ndani ya hifadhi ya Ngorongoro akiwa kama Mwenyekiti wa Bodi ya asasi inayosimamia hifadhi hiyo. Ni kwani naye asijivue gamba kwa kujiuzul nyadhifa zote ndani ndani ya chama kama maazimio ya vikao vya chama hicho yanavyohitaji? Naomba kuasilisha
   
 2. G

  Gwesepo Senior Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nani asiye jua kuwa msekwa ni fisadi na mwanamagamba mzoefu?ana gamba la kinyoga huwezi kugundua kirahisi Pole sana Taznania Kila kona wame jaa wanamagamba sijui tukimbilie wapi tufwile nyambala
   
 3. Bishop Hiluka

  Bishop Hiluka Verified User

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 4,100
  Likes Received: 1,424
  Trophy Points: 280
  Nchi hii kiongozi huwa anajiuzulu mwenyewe bila shinikizo?
  Ikitokea hivyo basi jua litachomozea Magharibi!
   
 4. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  what if anayemtuhu yuko wrong thats why kuna chance ya kukanusha na ameitumia...sasa ni wajibu wa vyombo husika ufuatilia tuhuma na kuchukua hatua endapo kuna ukweli...but sio kila unapotuhumiwa unapaswa kuwajibika...tukumbuke kuna tuhuma za kusingiziana watawajibika wangapi?

   
 5. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Huyu mzee kila sehemu anaboronga, ila nafikri kosa ni la JK kumteua kuwa mwenyekiti wa boad ya Tanapa. Mzee ameshachoka huyu anatakiwa apunzike. Sasa anafanya mambo ya ajabu halafu anajitetea bila aibu mbele ya vyombo vya habari
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mashirika yote ya umma ambayo mwenyekiti wa Board ni mstaafu, wenyeviti wake wana tabia zinazofanana. Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tanesco hakuwa na ofisi wakati siyo full time employee? Huyu wa Ngorongo amepewa gari na nyumba ya kuishi wakati siyo full time employee.

  We have long way to go before a true corporate governance practice in our government owned corporations
  .
   
 7. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #7
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  sidhani kama tuna utamaduni wa kujiuzuru kila tukituhumiwa
   
 8. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #8
  Aug 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Huyu ndiye alipokuwa mwenyekiti wa Vodacom aliingia mgogoro na "mkewe" (Anna Abdalah akiwa UWT) kwa kuwambia wanaosema yeye kuwa spika na wakati huohuo kuongoza VTL kutamshinda akasema wanaosema hayo wana wivuwa kike sijui leo atamsemaje Mhe. Ole Telele. Yeye mzee apumzike tu kashatumikia taifa hili sana BABU VUA GAMBA au njoo nawe na msemo wako wakuondokea
   
 9. sajosojo

  sajosojo JF-Expert Member

  #9
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 14, 2010
  Messages: 815
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  What if anayemtuhu yuko wrong thats why kuna chance ya kukanusha na ameitumia...sasa ni wajibu wa vyombo husika ufuatilia tuhuma na kuchukua hatua endapo kuna ukweli...but sio kila unapotuhumiwa unapaswa kuwajibika...tukumbuke kuna tuhuma za kusingiziana watawajibika wangapi?
   
 10. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #10
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Msekwa: Nimetupiwa fitina inayoitwa usongombwingo [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 22 August 2011 22:03 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Neville Meena, Dodoma
  MAKAMU Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa amemshambulia Mbunge wa Ngorongoro (CCM), Kaika Saning'o Ole Telele akisema kwamba kauli alizotoa bungeni dhidi yake ni fitina yenye uongo ndani yake.

  Kauli hiyo ya Msekwa imekuja wiki moja bada ya kulipuliwa bungeni na wabunge wa chama chake huku wale wa kambi ya upinzani wakimtuhumu kuingilia mamlaka ya kiutendaji ya Bonde la Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), wakati si mtendaji.

  Baada ya kukaa kimya tangu kutolewa kwa madai hayo Agosti 18, mwaka huu, jana Msekwa ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Hifadhi hiyo aliibuka mjini hapa kwa kuitisha mkutano na waandishi kwenye Ofisi za Makao Makuu ya CCM kufafanua tuhuma moja baada ya nyingine huku akiita maneno ya Telele kwamba: "Ni aina ya uongo unaoitwa usongombwingo".

  Msekwa alifafanua maana ya usongombwingo kuwa ni maneno ya uwongo yenye fitina ndani yake. Yaani siyo uongo wa kawaida, bali wenye lengo la kumfitini aliyetajwa."

  "Maneno yaliyonukuliwa na magazeti kwamba yalisemwa bungeni na Mheshimiwa Telele yalikuwa na lengo la kuchafua jina langu mbele ya umma. Yalikuwa ni maneno ya kashfa dhidi yangu, yaliyojikita katika kuchafua historia ya muda mrefu ya uadilifu wangu katika kutekeleza kazi za umma nilizopangiwa katika nyakati mbalimbali na marais wangu, kuanzia Rais Nyerere (Julius) hadi Rais Kikwete (Jakaya)."

  Alipoulizwa kwa nini amemzungumzia Telele peke yake wakati suala hilo lilisemwa na wabunge wengine, Msekwa alijibu: "Kwa sababu yeye ndiye aliyelianzisha, wengine walidakia na kuendeleza."

  Kutohudhuria mjadala wizara
  Kuhusu kutokuwapo kwake kwenye mjadala wa hotuba ya Wizara ya Maliasili na Utalii, Msekwa alisema bila shaka hoja hiyo inatokana na dhana mpya iliyojengeka ya kukusanya watu wengi Dodoma kwa gharama kubwa wakati wa mikutano ya Bunge la bajeti bila sababu za msingi.

  Alisema kwa kuwa tayari alikuwa amekutana na Kamati ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii, hakuona umuhimu wa kuwapo Dodoma na badala yake alipanga ratiba ya shughuli nyingine zinazohusiana na uenyekiti wake wa bodi.

  Alisema kazi hizo ni pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa hoteli za kitalii ndani ya Hifadhi ya Ngorongoro na siyo kugawa viwanja kwa wawekezaji pamoja na miradi mingine inayotekelezwa kwa fedha za NCAA ikiwamo Shule ya Sekondari ya Nainokanoka ambayo imekuwa ikijengwa kwa muda mrefu bila kukamilika.

  "Hii ni kazi muhimu zaidi kuliko kukaa tu kwenye Gallery ya Bunge na kulipwa posho za kusikiliza hoja mbalimbali za wabunge zinazoelekezwa kwa Waziri!," alisema Msekwa na kuongeza kuwa taarifa ya kazi zake hizo itawasilishwa kwenye kikao cha Bodi ya NCAA.

  Msekwa alisema kimsingi bajeti ya wizara ni sehemu ya Bajeti Kuu ya Serikali ambayo tayari ilishapitishwa na kwamba kazi wanayofanywa wabunge hivi sasa kwa mujibu wa Ibara ya 63 (3) (b) cha Katiba ya nchi ni kujadili utekelezaji wa kila wizara.

  "Kwa hiyo hakuna kazi inayohitajika ya mwenyekiti kusaidia kuhakikisha kuwa bajeti ya wizara inapitishwa vizuri na Bunge, kwa sababu bajeti ya wizara inakuwa tayari imepitishwa wakati Bunge linapopitisha bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Fedha," alisema.

  Alisema alipokutana na Kamati ya Bunge, alijibu hoja zote alizoulizwa na kamati hiyo na kwamba tuhuma zilizotolewa na Telele hazikujitokeza wakati huo na kwamba madai ya Telele kwamba alikwenda Ngorongoro kugawa maeneo ni lugha ya kuudhi ambayo inakatazwa na Bunge.

  Wakati Telele akichangia alisema wakati wenyeviti wenzake (Msekwa) wote wako Dodoma yeye alikwenda kutafuta maeneo ya kujenga hoteli... "Mwenyekiti wa Tanapa yuko hapa. Yeye hayumo humu, labda alijua kwamba tutazungumza huku. Lakini kule aliko anatusikia."
  Jina la Rais

  Tuhuma nyingine ambayo Msekwa aliikanusha ni madai kwamba alitumia jina la Rais Kikwete kuhalalisha utoaji wa maeneo ambayo ni mapitio ya wanyama kujengwa hoteli.

  Alisema Desemba 28, 2006 alikutana na Rais Kikwete pamoja na Mhifadhi Mkuu wa NCAA, Bernard Murunya wakati huo akikaimu nafasi hiyo na kiongozi huyo wa nchi aliwapa maagizo ambayo yaliwasilishwa kwenye mkutano wa bodi kwa waraka maalumu.

  "Katika waraka huo, maelekezo ya Rais kuhusu haja ya kuongeza idadi ya vitanda katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro yameainishwa waziwazi," alisema Msekwa na kuongeza kuwa madai kwamba anatumia jina la Rais vibaya pia si ya kweli.

  Alisema maombi ya kujenga hoteli kwenye mapitio ya wanyama yaliwahi kutolewa na Bodi iliyokuwapo wakati huo kukubali, lakini utekelezaji wa mradi huo haukufanyika kutokana na katazo la Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC).

  "Tunaendelea kutekeleza uamuzi wa NEMC kwa kutoruhusu hoteli yoyote nyingine kujengwa katika mapitio ya wanyama. Ndiyo sababu katika orodha ya viwanja vilivyogawiwa na Bodi katika mkutano wake wa 87 wa Oktoba,2007, hakuna kiwanja chochote kilichopo kwenye mapitio ya wanyama kama Mheshimiwa Telele anavyodai," alibainisha Msekwa.

  Kujifanya Mtendaji
  Msekwa alisema hajawahi kufanya kazi za watendaji na kwamba tuhuma hizo si za leo kwani zilianza muda mfupi tu baada ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi.

  Alisema baada ya siku 100 tangu kuteuliwa kwake, alimwandikia waraka Waziri husika ambaye wakati huo alikuwa Anthony Diallo akimweleza jinsi atakavyofanya kazi na kwamba amekuwa na utaratibu wa kutoa taarifa ya bodi yake kila baada ya muda fulani kwa waziri.

  Mwenyekiti huyo wa NCAA alisema tuhuma hizo ziliendelea hata baada ya Waziri Jumanne Maghembe kuhamishiwa katika wizara hiyo na kwamba waziri huyo alifanya uchunguzi na kubaini kuwa hazina ukweli wowote.

  Msekwa aliongeza kuwa hata kikao cha bodi kilichojadili tuhuma hizo kilizitupilia mbali na kwamba anamshangaa Telele ambaye wakati huo alikuwa mjumbe kuziibua upya hali akifahamu kwamba zilikuwa zimeshawekwa kando.

  Alisema Ngorongoro haiwezi kufia mikononi mwake kwani tangu alipochukua uenyekiti wa chombo hicho ameongeza uwezo wa ukusanyaji wa mapato kutoka Sh17.79 bilioni mwaka 2005/06 hadi Sh48.7 katika mwaka wa fedha unaoishia Juni, 2011.

  Msekwa alisema hasira dhidi yake zinazoonyeshwa na Telele huenda zinatokana na kutoteuliwa kuwa mjumbe wa bodi katika kipindi cha pili hivyo kuamua kuwashambulia watu ambao kimsingi hawahusiki na uteuzi huo.

  Kuhusu ombi la kuvunjwa kwa bodi hiyo Msekwa alisema: "Ni vyema (Telele) hilo ni jambo ambalo halitekelezeki kisheria," na kwamba labda utumike ubabe kutokana na Sheria ya Mamlaka ya Ngorongoro kutompa Waziri uwezo wa kuivunja.

  Kilichosemwa Agosti 18
  Akichangia hotuba ya Bajeti ya Maliasili na Utalii, Telele alisema Msekwa amekuwa akiingilia kazi za watendaji wa Ngorongoro kiasi cha kutoa ofa za ujenzi wa hoteli kwa wafanyabiashara katika Bonde la Ngorongoro na kwamba maeneo ambayo yanatolewa ni mapito ya wanyama aina ya faru.

  "Kwanza nadhani jambo hili aangalie tunaheshimu sana Chama cha Mapinduzi ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi na maombi yanavyokuja ya kujenga hoteli wanasema Rais amesema, Rais gani anasema kwamba tujenge hoteli aende kinyume na taratibu zilizowekwa na wahifadhi na watalaamu wa hifadhi?"

  Msemaji wa Kambi ya Upinzani Bungeni kwa Wizara ya Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa alisema: "Haiwezekani Mwenyekiti wa Bodi ya Ngorongoro ambaye moja ya majukumu yake ni kukagua hali halisi ya hifadhi hiyo, ajiingize pia katika shughuli za utendaji tena zilizo nyeti kama hizo."[​IMG]Makamu Mwenyekiti wa CCM (Tanzania Bara), Pius Msekwa  Aliitaka Serikali kuchukua hatua kali dhidi ya Msekwa kwa kukiuka mipaka ya majukumu yake na kwamba kambi ya upinzani ipo tayari kuipa Serikali ushirikiano kuhusiana na tuhuma hizo.

  Pia mbunge wa Simanjiro (CCM), Christopher Ole Sendeka akichangia hotuba hiyo alisema bodi hiyo ifumuliwe ili iundwe upya kwa maelezo kwamba ilikuwa imekiuka ushauri wa Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kuruhusu ujenzi kwenye njia za faru.


  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 11. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #11
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  #46 mikolo mileki mingi 2011-08-23 19:52 Msekwa ni mmoja wa wazee waliosoma sana Tanznaia, lakini hana cha kukumbukwa kizuri alichokifanyia Taifa. Muda huu anpaswa kustaafu siasa na kukaa pembeni akiwa mshauri wa mambo ya sheria ya jamaii. Nilitegemea muda muu angekuwa ametunga kitabu cha dira za chama au uongozi bora, lakini kauchuna na kujiingiza katiba Ubody members ya mashilika ya Rostam Azizizizizizi! Msekwa wewe sasa neda kalime kwenu ukerewe! Mimi nikiwaonaga msekwa na malecela wakijifanya kutoa ushauri, nacheka sana.
  Quote

  +2 #45 Manuel 2011-08-23 16:59 To you Mr.Msekwa...Make love,not war,DUDE!
  Quote

  +2 #44 Beano 2011-08-23 16:25 Hizi ni sura za wazee wasiotaka kustaafu wakiwa na heshima zao. Ulafi na kujilimbikizia kwa mtu ambaye maisha yake hapa duniani yanakaribia kuisha ni mtindio wa ubongo
  Quote

  +1 #43 ahmed00 2011-08-23 16:00 Msekwa, Luhanjo, Jairo, Rutabanzibwa,Ad amu Malima almost serikali yote ya JK na JK mwenyewe ni wasanii.
  Pamoja na vielelezo vyote Jairo hana hatia na amepata kibarua chake. HUU NI USANII
  Quote

  +1 #42 sitaki tena 2011-08-23 15:35 sasa hivi tunakuja na nyingine! tunataka kuuza Mlima K! mpaka tujue kama kweli nyie watz uvumilivu ni sifa yenu ya kuzaliwa au mnajifanyisha tuu
  Quote

  +2 #41 majmaj 2011-08-23 15:20 Msemakweli longa hoja za uongozi na si za maisha ya mtu na mkewe. Hoja kwa ufisadi wa Msekwa, yes, does hold water while any focus to his marital affairs dilutes what you want to share with readers. Msekwa hakupata nyadhifa zake kutokana na maisha yake na mke wake. Suala la kushindwa au kuweza maisha ya ndoa ni so private na halina maslahi yoyote kwa umma. Tunahitaji kiongozi makini, asiye fisadi, mchapakazi na anayejali maslahi ya watanzania. Aoe wake sabini au asioe hiyo ni shauri yake. We do have strong leaders who have demonstrated excellentleader ship the world over but we do not venture into their troubled marriages eg Mandela, Nkurumah, Belursconi, Moi, Mkapa, Schwazinegger, nk are one of those. Biblically we have the likes of mfalme Sulemani, Samson, Daudi, Mzee Ibrahim nk nk. So who si Msekwa?

  Msekwa asemwe kwa ufisadi wake na si kwa masuala yake ya ndoa. Ndoa nyingi zimeshindikana si kwa viongozi, wafanyabiashara , watu wa kawaida, viongozi wa dini, superstars nk au kwa waafrika, wazungu, waarabu, wachina nk achilia mbali na wakerewe, wayao, wachaga, wakwere nk bali kwa watu wote possibly inclluding you. Isitoshe ndoa ni urafiki (mapatano), unaweza kutengenezwa na kuvunjika wakati wowote iwapo wahusika wanakubaliana hivyo.

  Quoting MSEMAKWELI:
  Pius Msekwa nyazifa zote ulizowahi kushika zilikushinda,um akamu wa ccm umekushinda na hata ndoa yako ilikushinda,ing awa ili la ndoa limewashinda Wakerewe wengi ninaowajua.
  Watu kama Msekwa ndiyo wanaozidi kukipeleka shimoni chama cha mapinduzi.
  Walk Up Kikwete.​
  Quote

  +2 #40 Adam 2011-08-23 14:11 Msekwa kama siyo fisadi aeleza ni kiasi gani alilipwa na waliojenga ukumbi mpya wa Bunge kwa sababu mwenye akili yeyote atajiuliza ni kweli watanzania walihitaji ukumbi mwingine wa bunge na ule wa zamani unaitwa Msekwa white elephant?
  Quote

  +1 #39 MSEMAKWELI 2011-08-23 13:57 Pius Msekwa nyazifa zote ulizowahi kushika zilikushinda,um akamu wa ccm umekushinda na hata ndoa yako ilikushinda,ing awa ili la ndoa limewashinda Wakerewe wengi ninaowajua.
  Watu kama Msekwa ndiyo wanaozidi kukipeleka shimoni chama cha mapinduzi.
  Walk Up Kikwete.
  Quote

  +1 #38 MSEMAKWELI 2011-08-23 13:55 Msekwa nyazifa zote ulizowahi kushika zilikushinda,um akamu wa ccm umekushinda na hata ndoa yako ilikushinda,ing awa ili la ndoa limewashinda Wakerewe wengi ninaowajua.
  Watu kama Msekwa ndiyo wanaozidi kukipeleka shimoni chama cha mapinduzi.
  Walk Up Kikwete.
  Quote

  +2 #37 Makiri Unguluma 2011-08-23 12:59 Quoting rutashubanyuma:
  swali langu kwa Msekwa ni kuwa kwa nini ni mkabila kupita kiasi yaani havumiliki kabisa. Alipokuwa Mwenyekiti wa Bodi ya CDA akampachika mkabila mwenzie Dr. George Mlingwa kuwa Director General..................alipokuwa Mweka Dr. Manyanza...........Ngorongoro Bernard Mrunya Mkerewe mwenzie na ambaye hata vyeti hana na Msekwa kamshauri vibaya Murunya akaongezewa muda wa miaka miwili baada ya kufikisha umri wa kustaafu..................this old man is the most corrpupt guy in CC ya CCM today......​
  MLINGWA NI MSU[NENO BAYA] JAMANI ALIYOKOSA YAMETOSHA HAKUNA HAJA YA KUMUONGEZEA BABU WA WATU. HAWAWEZI KUSTAAFU MAANA WANAYAFANYA MAISHA YA KAWAIDA KUWA MAGUMU, UMEME, MAJI, NA MAFUTA HAVIJULIKANI BEI HALAFU USTAAFU BORA KUFIA HUMOHUMO
  Quote

  +1 #36 mcso 2011-08-23 12:49 Mh mbunge ndugu Selele anapokea maoni yenu hapa tathmini.com/.../telele-saning'o-kaika kuhusu utendaji wake wa kazi. Msimuangushe ndugu wananchi
  Quote

  +1 #35 kuku 2011-08-23 12:43 Tatizo la Tanzania Viongozi wetu wanataka kula sasa hguyo mbugnge anaona mtu mwingine anakula jimboni mwake.Tufanye nini wananchi mmeuza wanyama mwishoe na mbuga mtaziuza.Wananchi challenge kwetu viongozi tunaowachagua wanatuumiza wenyewe
  Quote

  +2 #34 Jo 2011-08-23 12:35 Hivi lini hawa wazee watatoka na ku2achia nafac na cc, inamaanisha aelewi yakuwa ni yeye aliyejipa tender ya kutengeneza barabara za Bonde hili??!! Hii ni aibu 2pu anatakiwa kukaa kimya ili mambo yapite, na kam ingekuwa uwezo wangu ningemuondoa mara moja kwenye bodi hii maana tangu ameingia ni uwizi na kupeana ma-tender ya ahjabu ajabu, yaani we caha 2??!! Lakini hivi huyu 2naemuita Le President, yupo kweli au ni kucheka-cheka 2 na kufukuzana na sketi?? Nisaididieni maana ingekuwa ni uwezo wangu ningeaanza kuandamana kama ukanda wa waarabu!!
  Quote

  +2 #33 kanyau 2011-08-23 12:34 Tuache kutafuna maneno na viswahili vya ukerewe. Tunawaheshimu wazee wetu na kuthamini michango yao kwa nchi hii. Lakini kama wamekengeuka sasa ktk nyakati za mwisho mwisho za utumishi wao wanakula bila kunawa tena kwa mikono yote miwili lazima waambiwe ukweli bila kutafuna mamneno. Wanapoanza kufikiri kwa kutumia matumbo na makalio yao, hapo ndipo ugomvi wao na kizazi kipya unapoanzia. Taarifa zilizopo ni kwamba, si Msekwa peke yake anayehomoa uhondo kwenye hifadhi, wapo wazee wengi nchini wenye majina na Historia ya nchi hii ambao wanafaidi kiharamu raslimali za Taifa katika hifadhi za Serengeti, Manyara, Mikumi nk. Naamini Mkuu wa Kaya anajua hili pamoja na viona mbali wake. Kwa nini hakuna hatua zilizochukuliwa ? Muulize Mkuu wa nchi na Mkuu wa Idara ya kuona mbali. Msekwa aache kujibu kwa kisanii, kama anaona kakashifiwa tena mbele ya Bunge na umma wote ukiona, amevuliwa nguo hadharani. Ili ajisafishe, aende Mahakamani. Hapo tutamwelewa, zaidi ya hapo, message sent and delivered. Tusubiri hukumu ya wananchi.
  Quote

  +2 #32 Rwihura Mutatina 2011-08-23 12:08 Tatizo ni CCM kuonyesha kwamba Tanzania hatuna watu wengine wa kuwa viongozi. Viongozi wale wale miaka nenda wakati vijana wanamaliza vyuo na bado hawana kazi eti wazee bado wamo. Waandishi wa mwananchhi fanya utafiti mtuletee viongozi ambao wame madarakani tangia miaka ya sitini. Nchi bado iko nyuma pamoja na utajiri lakini viongozi wale wale. Ujio wa chadema hata wasipochukua madaraka umefanya CCM iamke kidogo bado wanahitaji kuamka zaidi. Siyo lazima chama kiwe kwenye madaraka bali kuleta changamoto ili chama kinachotawala kisilale usingizi kwam ilivyo kuw CCM n watanzania hata siku moja tusikubali ukiritimba wa chama chochote iwe Chadema, CCM, TLP, CUF etc. Ukiritimba ni hatari sana hata TANESCO tatizo lao kubw ni Ukiritimba. Nina wahakikishia watanzania kama TTCL ingebakia kampuni pekee ya simu sasa hivi bei simu ingekuwa haikamatiki lakini sasa hawafikirii hata kuongeza bei hata kidogo.
  Rwihura
  Quote


  1234
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h] 1234  +3 #31 kokel 2011-08-23 11:32 Kama nafsi yake iko hai,basi itamshtaki..maana Mzee huyu ni fashisti.Anataja mafanikio ya fedha(48.7 billion)..SAWA ila mbona wenyeji wa eneo hili wanalia njaa tena kali..Fedha hizo zinakusanywa kwa manufaa ya nani?Ni msafiri tena zaidi na mwamuzi asiyekubali kuhojiwa/kushauriwa.
  Quote

  0 #30 Neutral Observer 2011-08-23 11:16 Wataalam mnaojua mambo haya tafadhali nisaidieni kujibu maswali yafuatayo:

  1. Utaratibu wa utoaji vibali kama hivi ukoje? Ni nani mwenye Mamlaka ya kuidhinisha na kutoa vibali vya ujenzi kwenye mbuga za wanyama? Waziri husika, Mkurugenzi wa Mamlaka, Mwenyekiti wa Bodi, Bodi nzima kupitia vikao, Wizara ya ardhi, Baraza la Mawaziri?

  2. Waheshimiwa Wabunge walitoa vielelezo vya uthibitisho wa madai yao? Kama hakuna vielelezo je hii hatuwezi kuiita fitina au uzushi?

  3.Je Msekwa ametoa majibu ya tuhuma dhidi yake kwa vielelezo vya uthibitisho?

  3. Hizo za 5 stars zinazojengwa ni zipi na zinajengwa au zinatarajiwa kujengwa maeneo gani Ngorongoro?

  4.Wakati wa harakati za ujenzi wa hoteli za 5 star Serengeti za Kempinski Bilila Lodge na Grumeti Lodge taarifa zake zilikuwa zinajulikana wazi kwa umma, ina maana kwa ngorongoro 5 star zinajengwa kwa siri hata NEMC na wanaharakati wa mazingira wamezibwa mdomo hawajatoa maoni yao? Hii kweli inawezekana kufanyika bila kujulikana katika generation hii ya kuscan na kuattach? Hata JF?

  5. Je NEMC na wanaharakati wameshatoa kauli yoyote kuhusu jambo hili?

  Ukiangalia mwelekeo wa maoni mengi hapa ni ule wa ushambulizi wa uzee na U-CCM wa Msekwa na siyo uchambuzi wa hoja alizotoa. Kwa kweli chuki dhidi ya CCM na serikali yake zimetufunika macho mpaka chochote kinachozungumzw a kutoka mdomoni mwa watu wao kinaonekana ni kama kinyesi tu wala hatujali kufanya uchambuzi wa kina. Tabia hii pia ipo kwa wapenzi wa CCM dhdi ya wapinzani. Wengi wetu tuna hulka ya kuchagua tu maneno tusiyoyapenda kutoka jedwali zima na kuyashikia bango kwa mashambulizi binafsi kwa mtoa hoja mradi tu ana mtizamo tofauti wa kisiasa. Huu ni ugonjwa mkubwa kwa watanzania ambao nafikiri unasababishwa na ubinafsi mkubwa uliyojaa kwenye nyoyo za baadhi ya jamii yetu. Inabidi tujitafakari kwa kina la sivyo hata mabadiliko ya uongozi wa Jamii hayatazaa matunda mazuri ya muda mrefu.

  Wote hatupendi kinachoendelea lakini linapotokea jambo kama hili ni muhimu kuweka hisia zetu za kibinafsi na kisiasa pembeni na kujaribu kupata uthibitisho wa ukweli wa madai ya pande zote ili kupata taarifa sahihi za mgogoro huu vinginevyo tukiri kuwa tutakuwa tuneaendekeza majungu na fitina. "Trust but verify".

  Hapa inaonekana mashambulizi mengi yanaelekezwa zaidi kwa mtoa hoja kuliko uchambuzi wa hoja zake. Huu ndiyo udahifu wetu wa kawaida.

  Sisi vijana sasa hivi tupo katika harakati za kupokea hatma ya nchi yetu kutoka kwa hawa wazee wetu, tumeona makosa mengi yanafanyika na tunataka mwelekeo mpya lakini tujiulize kama miongoni mwa tabia zetu ni kuamini haraka taarifa au hoja zinazotolewa bila kuzitafutia uthibitisho na kujikita kwenye kushambulia watoa hoja kwa hisia binafsi na siyo kujadili hoja, Je sisi tutakapokuwa viongozi kesho hatutaendeleza tabia hii kwa wanaotoa hoja dhidi yetu?

  Nitashukuru sana kama kama kuna mtu ataweza kusaida kujibu maswali haya kwa hoja na siyo kwa mashambulizi binafsi.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA.
  Quote

  +1 #29 John Maganga 2011-08-23 10:57 Nimesikitishwa sana na kitendo cha Pius Msekwa cha kujiingiza katika kuhujumu maliasili za Tanzania. Hata kama akiita waandishi kwa lengo la kutaka kujisafisha, lazima aelewe watanzania wana akili timamu na wana uwezo wa kuchuja na kupambanua.Msekwa uliheshimika sana miongoni mwa watanzania kutokana na nyazifa ulizoshika katika utumishi, lakini siamini kama unamaliza kwa AIBU KUBWA.
  Quote

  +4 #28 janet 2011-08-23 10:53 jamani naomba mnisaidie! kustaafu kazi serikalini unatikiwa uwe na umri gani!?
  Quote

  +4 #27 ahmed00 2011-08-23 10:29 Wakati mwingine kukaa kimia ni busara kuliko kuongea U JI NGA ambapo anajidhalilisha zaidi
  Quote

  +4 #26 mgongofimbo 2011-08-23 10:23 we babu we ni gamba hata ujitetee kwa mipasho we ni gamba tu
  Quote

  +2 #25 loma 2011-08-23 10:20 Wamekula yambuzi wameota mapembe na pembe zenyewe bd wanataka kujitetea eti hawana na kawaida ya pembe zikitoka zinaonekana,kwl huyu mzee nae ameamu kuuza hifadhi na bila aibu anajitetea,ina mana hana hata aibu ajinyamazie tu akale hizo alizochukua mana nafkiri ameshawawekea mpaka wajukuu wake ili ss ambao ndg zetu hawana vyeo serikalini tufe,kwl hawa jamaa wametudharau vyakutosha ila naamini tunakusanya matukio ili siku tikiingia mitaani mtambue kuwa tumechoka na wezi.
  Quote

  +3 #24 Felista 2011-08-23 10:06 MZEE MSEKWA PUMZIKA TU SASA MAANA HATA UJITETEE VIPI HAKUNA WA KUKUAMINI LABDA MKEO AMBAYE NAYE NI HAO HAO MAGAMBA.
  Quote

  +2 #23 neema mghen 2011-08-23 09:39 hivi kwann hawa viongozi wanapenda wasiambiwe ukweli?maana Richmond walidai wamefedheheshwa ,ilipokuja ishu ya Sumaye akawabana waandishi kuwa atawafikisha mahakamani watakaomwandika katika shutuma yoyote,leo hii mh Telele anawapigania wanyonge kwa kueleza ukweli khs huyu mh bado anakuja juu.Tunamlaumu Kikwete sababu hana maamuzi na hii ni kutokana na mfumo wa kibepari,katika chama chake na ili serikali yake iimarike tunamwomba Kikwete aache kuchagua viongozi kiurafiki na azingatie maoni ya upinzani na hawa wazee wapumzike.
  Quote

  +5 #22 Beano 2011-08-23 09:27 Mtu mnafiki siku zote hawezi kukaa kimya anapoambiwa ukweli. Huu ni umri wa kustaafu, lkn hivi vibabu vinakazana kujaa maofisini wakati vimechoka ubongo hadi mwili. Nia ni kuendelea kuiba na kulamba marupurupu. Mwenzao Mheshimiwa sana Mandela anamalizia maisha yake ya hapa duniani akiwa na amani na watu wanampenda na kumlilia. Hivi vya hapa kwetu vinakomaza kichwa utafikiri havitaki amani. NAKUKUMBUKA SANA KAMARADA RASHID MFAUME KAWAWA, muaminifu daima. Mungu ailaze roho ya mzee yule mahali pema peponi, Amen!
  Quote

  +4 #21 Beano 2011-08-23 09:22 Quoting ajuaye:
  Tatizo ni kwamba wazee hawa wamezoea starehe za mwili kwa muda mrefu. Sasa wakijiuliza ni wapi tena watazipata wakiwa nje ya ofisi wanachanganyiki wa. Vinginevyo mzee kama huyu alitakiwa kuwa ameshajipumziki a siku nyingiiiii. Sasa ona anavyojiadhiri mwenyewe kwa mipasho ya taarabu!​

  Kaka wee, ni kukosa ubongo ndio kunawafanya waishi kwa siasa. Ukiwakuta majukwaani wakiwaasa vijana wajiajiri bila mitaji utadhani sio wao wenye mitaji lkn wanashindwa kuwa ma-bakhresa wapya. AKILI NZURI UKIWA NAYO
  Quote

  +4 #20 Hariti 2011-08-23 09:19 Kwa kweli sasa nimejua ni kwa nini Watanzania wengi bado ni maskini.kumbe ni ufinyu wa mawazo wa viongozi wetu.yaani vitu wanavyoviongea hata mtoto wa form one pale st.marians hawezi kuongea utumbo kama huo.
  Hoja hapa ni kwamba,Bwana msekwa unafanya kazi za kiutendaji ambazo kimsingi si kazi zako,sasa wengi tulitegemea ujibu kwa vithibitisho halali kuonyesha tuhuma hizo ni za uongo,lakini cha ajabu mzee wewe unakuja na mipasho.
  halafu hata hawa waandishi wa habari nao sijui ni vipi,wanapewa fursa ya maswali wanauliza maswali ya mteremko mno.ati kwa nini hukukataa uenyekiti wa bodi wakati wewe pia ni makamu mwenyekiti wa ccm? hivi hili ni swali la msingi kwa mkutano huo? au huwa mnanunuliwa?
  Quote

  +2 #19 Manyoya 2011-08-23 09:16 Msekwa aondoke haraka maana anachafua hewa
  Quote

  +4 #18 Göttingen 2011-08-23 09:10 You can fool people for sometime, but you can't fool them all the time.....
  Quote

  +5 #17 A. M.Hamisi 2011-08-23 09:08 Nyinyi wazee kwanini mnakuwa wagumu kuachia ngazi mnapokubwa na makashfa mazito mazito kama haya, msekwa achia ngazi kwa heshima usitake wakufulumushe, au ndio mnaona ujiko?
  Quote
   
 13. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #13
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  [h=4]Comments [/h] 1234  +6 #16 ajuaye 2011-08-23 09:04 Tatizo ni kwamba wazee hawa wamezoea starehe za mwili kwa muda mrefu. Sasa wakijiuliza ni wapi tena watazipata wakiwa nje ya ofisi wanachanganyiki wa. Vinginevyo mzee kama huyu alitakiwa kuwa ameshajipumziki a siku nyingiiiii. Sasa ona anavyojiadhiri mwenyewe kwa mipasho ya taarabu!
  Quote

  +3 #15 Lilian 2011-08-23 09:01 Jamani hiki chama chetu sasa kinatia kichefu chefu. Hivi vizee vipumzike sasa Msekwa hata macho hayaoni vizuri mboni zimejaa minyama uzembe anapewa kuongoza bodi ya taasisi nyeti kama Ngorongoro Conservation? Mh. Kikwete nakupa ushauri wa buuuure usipokuwa makini CCM inafia mikononi mwako hii awamu yako ya mwisho safisha hawa wakongwe wapumzike kuna wasomi wengi sana wataalamu kibao mbona hamuwapi nafasi? Nchi hii ni yetu sote jamani pisheni wengine nao walisukume hili gurudumu. Msing'ang'anie madaraka. Kama mafisadi wanatakiwa kujivua magamba basi Msekwa awe miongoni mwao. Msinyooshee vidole wachache CCM inaonekana kama ni maficho ya mafisadi.
  Quote

  0 #14 meku 2011-08-23 08:59 Mzeee.!!!!!!! Utasema sana lakini wataibua yale ya kule PARIS mwaka JUZI.
  Kazi kwako.......let them toknow how clean you are. Asante BABANGU'
  Quote

  +4 #13 big 2011-08-23 08:29 jamani mimi inatosha tuitoe hiki chma kimeoza hakistahili kusimama tena Kwanini tusikitoe madarakani I hate discussing about ufisadi while we can kick it out if we want changes, lets decide now to let it go,enough is enough Wapi chadema maanadamano wanayotaka kuunda sheria ya kuyaondoa ndio njia pekee ya kuitoa CCM madarakani believe me or not mpaka uchaguzi ujao waTZ tutakuwa tumechoka vibaya sana Chaema washa moto wananchi wamechoka tupo pamoja kudai haki na uadilifu kwa ustawi wa nchi yetu
  Quote

  +3 #12 bushman 2011-08-23 08:24 MSEKWA KASHFA HII INAKUTAFUNA INABIDI UJIVUE GAMBA MZEE,UTAJIELEZA SANA LAKINI UADILIFU WAKO HAUPO CCM NI KICHAKA CHA WANYANG'ANYI WA NCHI HII
  Quote

  +4 #11 Asante Mungu 2011-08-23 08:07 Msekwa ni mojawapo ya Magamba yaliyobaki CCM je yeye anasubiri nini asiondoke? Hii nchi sio ya kwake ni ya watanzania wote. Kwa kashfa nzito kama hii ni vema angejiuzulu ili kupisha uchunguzi zaidi.
  Quote

  +8 #10 rutashubanyuma 2011-08-23 06:59 hoja za msekwa hazina mashiko hawezi kusema sheria inampa madaraka waziri kuteua bodi lakini hana uwezo wa kuivunja kama imejaa wezi na wabadhirifu kama msekwa..................

  vile vile msekwa aelezee umma wa watanzania tangia awe mwenyekiti wa bodi mahoteli mangapi yamejengwa ngorongoro na maeneo gani?

  Na alikuta mahoteli mangapi ndani ya hifadhi hiyo ukizingatia ya kuwa zaidi ya asilimia 80 ya nahoteli yote ngorongoro yamejengwa wakati wa miaka 4 ya uenyekiti wake......................na yeye anahisa kwenye hoteli 3 ndani ya hoteli mpya........

  suala la kudai Telele ana chuki binafsi ni kufilisika kisiasa....................msekwa jibu hoja na kama hii serikali ya kifisadi iko makini hii bodi ni ya kuivunja na kuteua nyingine.............
  Quote

  +8 #9 Vipaji 2011-08-23 06:57 Wee Kibabu Msekwa heri ungekaa kimya. Kuliko kuongea utumbo kujitangaza jinsi ulivyomwongo . Pumzika mzee kule Pensheni mud a wake wa kutafuta umekwisha mwongo mkubwa
  Quote

  +8 #8 rutashubanyuma 2011-08-23 06:54 swali langu kwa Msekwa ni kuwa kwa nini ni mkabila kupita kiasi yaani havumiliki kabisa. Alipokuwa Mwenyekiti wa Bodi ya CDA akampachika mkabila mwenzie Dr. George Mlingwa kuwa Director General..................alipokuwa Mweka Dr. Manyanza...........Ngorongoro Bernard Mrunya Mkerewe mwenzie na ambaye hata vyeti hana na Msekwa kamshauri vibaya Murunya akaongezewa muda wa miaka miwili baada ya kufikisha umri wa kustaafu..................this old man is the most corrpupt guy in CC ya CCM today......
  Quote

  +6 #7 mwanaweja 2011-08-23 03:37 hawezi toa vidhibitisho maana huo ndio ukweli serikali yetu wengi wanafanya kazi amabzo sio zao bali kwa uchu wa kujipatia fedha ndio unaofanya kung'ang'ania mpaka wafie wakiwa madarakani wakati mwingine wastaafu iliwakae kwa amani wanjiaibisha sana.
  Quote

  +6 #6 Bundi 2011-08-23 03:32 Halafu hii mizee ina pesa lakini bado inapenda kung'ang'ani tu,wewe unastahili kupumzika,hivi bw Pius unadhani taifa hili halina viongozi? umezoea propaganda za CCM sasa umeshtukiwa unajikosha,nani atakubali propaganda zako,ondoka kampumzike,shug hulikia mambo ya CCM huko msaidie JK,badala ya kubuni miradi ya kuendesha CCM bado mnashindwa ubunifu na kukimbilia kuwaweka watu wenu kwenye zabuni,leo unatafuta njia ya kukana,wadangan ye vijana wa CCM wasiokwenda shule,tumeng;at uka,na wewe acha usongombingo wa kuita waandishi,tema tongo ulilolimeza
  Quote

  +10 #5 Dume la Nyani 2011-08-23 03:27 wee mzee nakuheshimu sana huendani na kauli zako,mfikishe mahakamani kama unaona kauli za Telele ni Usongombingo,hi vi ulichoambiwa ni kwamba umekuwa mwenyekiti mtendaji kwanza kanusha kama si mwenyekiti mtendaji,unafan ya kazi ya katibu halafu yeye afanye nini? je,Telele unadhani ni mtu wa kukurupuka? anao ushahidi sasa tunaona mkutano na waandishi kama vile unajiosha lakini,ridhika, jua lenyewe limezama bado unakaba mpka penalti,vitukuu waje kurithi nini?
  Quote

  +11 #4 hamis 2011-08-23 03:19 MSEKWA SI MKWELI KWANI KAMA MWENZAKE KINGUNGE NA WENGINEO ANAJARIBU KUWAHI MATUNDA YA HARAKA HARAKA KABLA HAJASTAHAFU KWANI UMRI WAKE NDIO HIVYO UMEKWENDA HATA HAPO ALIPO HAKUSTAHILI KUSTAHILI KUFANYA KAZI HIZI KWANI KWA HIVI SASA TUNAHITAJI DAMU MPYA NA WATU WENYE MAWAZO MAPYA NA SIYO TENA WAKINA MSEKWA WALIOPITWA NA WAKATI. KASHFA NI NZITO NA MAJIBU YAKE YAKO SO SHALLOW KWA KUONYESHA KUWA ANAHUSIKA KWANI ALICHOPASWA KUKIFANYA KTK HII PRESS CONFERENCE NI KUONYESHA BARUA ZA BODI NA KUONYESHA NI AKINA NANI HASA WALISAINI KUPITISHA KUUZWA KWA VIWANJA HIVYO NA ILIBIDI PIA MKURGENZI WA WANYAPORI NAYE AKANUSHE LAKINI AMEKAA KIMYA KWAHIYO HAPO LAZIMA KUNA KITU MSEKWA AMEFANYA.
  Quote

  +6 #3 Göttingen 2011-08-23 03:11 Tunahitaji hoja kujibu shutuma na si misamiati mipya.
  Quote

  +8 #2 Kishena, V. 2011-08-23 03:01 Muheshimiwa, usituletee misamiati mipya ya kupotezea. Mvua magamba wenzia na yeye uvuliwa. Msituyeyushe kwa matatizo mnayoendelea kutusababishia. Ushauri wangu wa bure: "Salama yenu mvunje chama hicho muanze upya......"
  Quote  1234
  Refresh comments list
   
 14. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #14
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  1234  +11 #1 Bakari 2011-08-23 02:19 Siku hizi CCM ina chuo cha kufundisha mipasho... eti USONGOMBWINGO! Sikutegemea mzee Msekwa (ambaye amewahi kuwa VC wa UDSM) angeita press kisha aongee maneno ya mtaani.

  Alitakiwa atoe vithibitisho kuonesha hakuna kibali alichotoa katika kipindi cha uenyekiti wake. Athibitishe kuwa kama kuna hotel inalalamikiwa basi ilijengwa kwa baraka za watu wengine.
  Quote  1234
  Refresh comments list
   
 15. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #15
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  nimepitia maoni haya yote kwenye magazeti mbalimbali na nimebaini ya kuwa huyu babu wananchi kweli wamemchoka...........he is a face of official graft inside the ruling clique na wao kumteua kusimamia zoezi la kujivua gamba ama kwa uhakika ulikuwa ni unafiki usio na kifani kabisa............
   
 16. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #16
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,014
  Likes Received: 417,338
  Trophy Points: 280
  unapoona mzee mzima amejitundika kwenye kichaka cha misamiati mizito mizito na kujificha humo basi ujue amebanwa mbavu na hana pa kupumulia kabisa........
   
 17. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #17
  Aug 23, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  ajivue kirahisi rahisi?
   
Loading...