G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,767
- 36,625
Huku serikali ikitenga bilioni mia moja kwaajili ya kuviboresha viwanda vyake vya ndani, viwanda vya kuzalisha dawa za binadamu vilivyopo nchini havitafanya kazi na serikali katika kipindi cha miaka miwili ijayo, imefahamika.
Bohari kuu ya dawa nchini MSD imeingia ubia na viwanda vya China pamoja na India ili visambaze dawa za binadamu nchini kupitia Bohari hiyo kwa asilimia mia moja miaka miwili mfululizo kuanzia mwaka ujao wa serikali unaoanza mwezi wa tano. Hiyo ni kwa mujibu wa tenda iliyofanyika hivi karibuni ambapo viwanda vya ndani havikutakiwa kushiriki.
Kwa maana hiyo sioni haja ya serikali kujikwamua hadi kuwaza kuviboresha viwanda vyake huku ikishindwa kuvitumia ili vijiendeshe.