Bila Shaka Mkuu
Nimekuelewa , wewe unaongela data science kama course content na mimi naongelea kama big world....
Kwa dunia zilizoendelea sio lazima uwe umesomea technical based subjects kama inavyochukuliwa na dunia ya tatu.
Na kama umesomea pia ni advantage, kwa hiyo ukisomea data science na kuwa data scientist narudia tena sio lazima uwe umesomea masomo ya sayansi,
Dunia ya juu, labda sio Africa kila kitu kinaendeshwa na data, iwe unafanya shopping online, unatap kadi yako iwe ya treni , au na ya benki, kununua vitu sokoni au madukani, kila unachoaangalia kwenye mitandao ya jamii, kuna watu nyuma hii process ambao kazi yao kama data scientist kazi yao ni kutengeneza algorithm kufuatilia trend zako ili kukutumia matangazo ya biashara kwenye email yako au simu yako kutokana na maisha yako , kukutumia habari na mihemko inayofanana na ufuatiliaji wako wa mitandao na tovuti....yaani kama unapenda kustream movies, unapenda kula pizaa , unatumia sana usafiri wa umma, unapenda habari za daimondi......hizi utakuwa kila ukifungu mtandao ndio habari za kwanza unaziona kwenye simu yako au kompyuta....
Ni neno lenye maana kubwa sana tena sana kwa dunia ya leo, au labda wewe unaangalia hili neno kama module ya course fulani...
Amazon amekamata dunia kwa data driven business, ukiwa unajua data science Amazon wanakuhitaji sana tena sana..na fecibuku wanakutafuta, na sasa na hii korona ndio kila serikali za dunia hii zimejua zinahitaji data scientist kuchakachua R number ya covid.... pia kufuatilia mienendo ya wananchi na tabia zao yaani serikali zimekuwa BIG BROTHER kinyemela....
Kwahiyo kwa siku za usoni, huyo mwanafunzi aelewe tu kuwa data science kiujumla ndio habari ya mjini..........