Aisee,,,
Bora hata ungekaa kimya
Data ni kitu kidogo eheee....
Ohhh samahani unamaanisha kibongobongo data hazina umuhimu eheee...
Na hizo fesibuku na insta na kadhalika na hii Jf akaunti yako hujui kuwa hizo na hii ni data....
Samahani nitakuwa nimeenda mbali na uelewo wako wa neno data.....
kama hujui dunia ya leo, inaendeshwa na data, iwe data kununua mboga sokoni, kuchungulia simu yako kila saa unavyobonyeza bonyeza, kutumia kadi ya benki , kulogi kwenye mitandao , mzunguko wa pesa, yaani ni ache tu imetosha....
Hii ndio course content ya hiyo data science.
1. Research Methods in science,
hizi research methods huwa zipo covered hata kwenye masomo mengine
2. Problem Driven Group Project
3. Programming in Python and MATLAB, hivi ni vitu vidogo kujifunza na karibia course za science na engineering wanavicover siku hizi.
4. Statistical Methods for Data Science, kidogo hapa utakua mgeni kidogo, ila haitakua tofauti na ile statistical method ya science ya kawaida.
5. Machine Learning Algorithms, hapa ni hesabu sasa, utajifunza algorithim zinazotumika kwenye machine learning, kwa mtu anayezijua hesabu ni vitu vidogo hivi.
6. Data Analysis, Visualization and Use
7. Big Data Analytics,
neno big data lisikuchanganye mkuu, vyote hivi ni vitu vidogo, hapo anamaanisha jinsi ya kuanalyse data nyingi. Unakuta mfano una millions of data, how do you analyse, unaitaka data ya laki tano unafanyaje ili kuichukua ndani ya muda mfupi na mambo mengine yanayohusu data analysis.
Mimi kwa ulewa wangu ukiisoma hii content hapa, unaweza kuicover kwenye masters ya masomo mengine kama ukifanya option ya somo la data science.
Mimi sihitaji kuandika mambo mengi, nina mambo mengi kidogo.
Ila usichukulie neno
Data Science kama data Science, jaribu kuangalia course content na kuona kama vitu vilivyomo humo ndio unavihitaji au la.
Nasema hivyo kwasababu mtu wa mathematics, computer science, statistics na engineering mfano petroleum engineering anaweza kufanya kazi za data science. Kwasababu probably ukiweza kucode kwenye python na Matlab kwa ufasaha then ukailewa na hiyo machine learning na AI kwa ufasaha utakua umeicover hiyo data science kwa 50 percent.