Msanii Wema Sepetu arejea CCM, aitosa CHADEMA

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,503
2,000
874951de442443338470145dde33ce1e.jpg

Wema Sepetu: Siwezi Kuendelea kuishi kwenye Nyumba inayo nikosesha amani... Peace of mind is everything for me... Natangaza Rasmi kuondoka Chadema na Kurudi Nyumbani....

Feels good to be Back...

==========
Siku moja kabla, aliweka post hii:

a8afa8c40b01d5729006c54314084f78.jpg


==========

Mapema mwaka huu (Februari), msanii huyo alihamia chama cha CHADEMA akidai ameenda kupigania demokrasi ambayo alidai ilikuwa inafifia nchini.

"Kuanzia sasa mimi siyo tena mwanachama wa CCM, na muda mfupi ujao nitachukua kadi yangu ya CHADEMA... Nimeamua kuingia CHADEMA kwa sababu nataka kupigania demokrasia, laiti ningejua, ningeingia zamani sana, najua nimewahi kusema kuwa nitakufa nikiwa CCM, lakini sikujua kama itakuwa hivi, laiti ningejua mapema basi nisingesema vile na ningejiunga CHADEMA muda mrefu sana, kwa sasa I am a proud member of CHADEMA" alinukuliwa Wema Sepetu mara baada ya kuhamia upinzani.

Aidha, msanii huyo anakabiliwa na shtaka la kutumia dawa za kulevya wakili wake akiwa ndg. Alberto Msando ambaye naye katimkia CCM toka ACT-Wazalendo.

Aidha, vipodozi vya msanii huyo (Kiss) vimepigwa marufuku na Serikali kuwa havifai kwa matumizi ya binadamu.
 

craq

JF-Expert Member
Mar 22, 2017
835
1,000
85495122e56fbe2243c2e7161d3a9b94.jpg9187ea0befd304e821ed792797829cf0.jpg270ff89506f80db52a241558a2507109.jpgIlikuwa rahisi sana kumuamini fisi na kumuachia bucha kuliko kuamini wema atakuwa chadema kwa muda ,nilikuwa nacheka kuona mbowe akizunguka na wema kila mahala wakienda uwanja wa taifa kuangalia mpira pamoja ,wakienda mahakamani


Kesi ya wema ilivyoisha aliongozana na kibatala huku wakishikana mikono mithili ya wapenzi .

Wema mbayaaaa tena mbayaa balaa ameshawatumia chadema Sasa anawatupa kama vile tissue

Ilihitaji moyo wa ujasiri kama wema angekuwa mwanachadema


Nakumbuka Vijana wa chadema walikuwa wanamtetea mpaka wanatokwa na fahamu walikuwa wanamsafisha saizi nategemea kejeli matusi na mashambulizi dhidi ya wema kuona


Kamanda wema ,wema mbayuwayu tokea kwenye sanaa yake makamanda walimuamini haha


Siasa tamu sana
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom