Leo hii Wema Sepetu wa kumuita Makonda "Le Brother"?

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,929
Kweli Siasa hazina adabu baada ya Wema Kurudi CCM na kusema yupo nyumbani amuita RC wa Dar Le Brother. Kasahau yale yote ya nyuma Kesi za Madawa na kila kitu.

Maneno yote aliyoyasema wakati anatoka CCM na kuenda Chadema Kasahau,

Wema:
Kwa jina naitwa Wema Sepeti Isack Abraham⁠⁠⁠⁠, Naomba mnisamehe kwa kufika kwa kuchelewa. Sitakuwa na mengi ya kuongea, nataka kutoa tamko moja kutoka kwa Wema mwenyewe. Nimewaiteni hapa kuja kutamka rasmi kwamba hivi sasa nmehamia CHADEMA kutoka CCM
⁠⁠⁠⁠
⁠⁠⁠⁠⁠⁠⁠Wema: ⁠⁠⁠Sio kwa tuhuma zinazonikabili bali nmefanya maamuzi kama mtu mwingine yoyote. Nyote mnajua nlikuwa kada wa CCM na nmepigania chama kwa uwezo wangu wote. 2015 niligombea ubunge viti maalum Singida na kura hazikutosha na sikufa moyo. Marehemu baba yangu alikuwa kada nguli wa CCM na alipata kuwa hadi mshauri wa rais Zanzibar, Waziri na Balozi wa Urusi. Amekufa akiwa CCM

Wema:
Nimetuhumiwa hivi karibuni, wakati najitoa kwa hali na mali ndani ya CCM na niliamini hawatanitupa na haina maana kwamba nilitaka kubebwa hapana. Kilichotokea kwangu kilikuwa ni uonevu. Nimetafakari sana kwanini hili limetokea. Kama mwanachama kimenivunja moyo. Tenda wema uende zako usingoje shukurani. Mimi naamin katika demokrasia. Nimefanya reseach yangu na hata wakati wa kampeni CHADEMA ilitupa tabu. CHADEMA inapigania demokrasia na mimi nataka uhuru wa watu
⁠⁠⁠⁠
Wema: ⁠⁠⁠Ningejua mapema ningenijiunga CHADEMA zamani. Najilaumu sana kuchelewa kujiunga CHADEMA. Bado sijachelewa kufanya maamuzi. Na hii najua nimeingia kwenye vita na naamini watu wengi wapo wananiunga mkono. Dola ifanye kazi zake na kifuata sheria kama dola. Ila wazingatie haki za binadamu. Naamini ndani ya CHADEMA tunaweza kuleta mabadiliko nchini. Kwa kupitia nguvu ya CHADEMA tunaweza pata ule uhuru tunaoupigania.

Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu na mama yake wahamia CHADEMA kutoka CCM

WhatsApp Image 2017-12-10 at 14.22.26.jpeg


Kwani ni lazima Msanii Kuwa na chama?
 
Siyo lazima kila msanii kuwa na mahaba na chama flani cha siasa
 
Wema ni msanii, msanii kazi yake ni sanaa. Sanaa ni maigizo.

Mimi nilishangaa zaidi pale professional lawyer alipogeuza maneno kusema eti EL hakuwa fisadi bali mfumo ndo chanzo.
 
Back
Top Bottom