Msanii wa filamu Wastara Juma aomba kusaidiwa pesa ya matibabu na Rais Magufuli

e2n

JF-Expert Member
Dec 24, 2015
636
790
"RAIS MHE MAGUFULI
MAKAMO MHE SAMIA SULUHU
WAZIRI MKUU MHE KASIM MAJAALIWA
MKU WA MKOA MHE POUL MAKONDA
WATANZANIA WENZANGU

Mim Wastara juma muigizaji wa filamu tanzania naandika ujumbe huu mfupi sina budi sina jinsi nahitajika kurudi hosptal india Sifael hosptal tokea tal 12/02/2017 ambapo nilitakiwa nifanye matibabu kwa mda wa miaka 2 chini ya uwangilizi wa hosptal hiyo kabla ya kufanya maamuzi ya kufanyiwa operetion ya mgongo hivyo kila tal 12/ 2 natakiwa kurudi hosptal nimejitahidi kupambana peke yangu kutafuta pesa ya kunirudisha hosptal nimeshindwa

Mwezi 1 wachina wenye kampun ya simu ya KZG wamenikimbia nikiwadai milion 80 mwezi wa 2 muzambiq nimepoteza mzigo wa milon 19 kwenye vurugu la kufukuzwa watanzania
Mwezi wa 3 nimeenda nchini sweden kufanya filamu nimerudi mikono mitupu mwezi wa 4 nimedai pesa yangu steps tumeishia kwenda mahakamani bila kulipwa nilivyokuwa natarajia tokea hapo chchote ninachofanya kinachohusu pesa lazima tuishie polis au mahakamani silipwi vile tunavyokubalian na baya zaidi ninaofanya nao kazi awajui kuwa tokea nimerudi nchini toka sweden ninahaha kutafuta pesa ya matibabu,,

silali kwa maumivu makali ya mgongo na ninazimia kila mda hii imetokana na kuchelewa kurudi hosptal kufanya tiba ya mgongo na kubadilisha soberly skoner inayowekwa kwenye mguu kama tiba kuu ya kurudisha mgongo wangu ukae sawa matokeo yake mguu unavimba na kuchanika kila mara mgongo unauma kitu ambacho kinanikosesha raha kabisa na kuona sasa naathirika kiakili kwa maumivu sababu mda mwingi nakunywa dawa za maumivu bila kujua kama nimemeza dawa mara ngapi kwa siku hii sio nzuri kiafya

Kikubwa ninachoomba kutoka kwenu ni mim nirudi kwenye apointment yangu ya hospital sababu siwezi kurudisha mguu wangu kama zamani lakini ninaweza kuyakwepa maumivu kutokana na tiba ninayoweza kupata kupitia tatizo langu

Sihitaji msaada wa mtu nikiwa mahututi nikiwa siwezi kuandika sms kupokea sim au kumtambua mtu nahitaji sasa ninayo nguvu kidogo ya kuelewa hta nataka kutibiwa nin staki nisaidiwe kwa mtu kunisemea matatizo yangu wakati huo mim nimeshashindwa hta kuongea tena please watanzania wenzangu mficha uchi hazai sio mim mwenye matatizo pekee wapo wengi ila wanaona aibu najua mtajiuliza kiasiku wastara anauza nguo why?

anataka msaada sio kweli kuwa biashara ya mtandao inakidhi mahitaji yetu nimekuwa nikipost bidhaa kwa fujo bila kupost hta picha zangu nikiamini nitauza sana ili nirudi hosptal lakini sio kweli kabisa watu wanataka kuniona mim mitandaoni na sio mashati na magauni ninayouza ndio maana sifanyi vizuri upande huo ninaumia sana kuona mashabiki nawanyima haki ya kuniona lakini ninayo shida nahitaji niwe na afya njema nitembee vizuri nifurahi na watoto wangu na mashabiki zangu

afya yangu mim inauzwa tena kuanzia dollar 18000 pia mtajuliza why sioni aibu kusema shida zangu au kuomba msaada wakati mimi ni msanii na tafsir ya walio wengi wasanii ni watu wenye pesa sana sio kweli sanaaa yetu ndio kwanza inakuwa nimechoka kupost nikilalamika naumwa huku kesho mtu ananiona mzima nacheza mziki kumbe najilazimisha tu kuficha mateso yangu staki tena kuficha maumivu yangu natembea nanenepa huku nina maumivu makali

natamani nimmpe mtu huu mwili na ili jina ili niwe huru kwenye mateso ya kujificha huku naumia
nimejaribu sana kuongea na marafiki zangu wa karibu wanajua natania ninavyosema naumwa nahitaji msaada mtu aamini hata nikimwambia nichangie elfu 50 anaona nina pesa nyingi sana nadanganya No kabla haujafa haujaumbuka

nikiuza nyumba gari na chchote nilichonacho alafu nikafa watoto wangu wataishi wapi nin kitawasaidia mpka wapate pesa za kujikimu?? Jibu hakuna japo nimejaribu kunadi kilakitu nilichonacho ili mladi nipate pesa nirudi hosptal lakin mda umepita sana na naendelea kuumia mwili na kiakili pia sijafanikiwa please usinitafsir vibaya wala kunikejili wakati huna uwezo wa kunisaidia mim nimeamua kuwa muwazi kuwa nahitaji msaada ili niendelee na majukumu yangu watoto na watanzania waendelee kuniona

Pili ninaomba serikali inisaidie nipate pesa ninazowadai wachina mpka sasa zaidi ya milion 400 maana nilisain mkataba wa miaka miwili mpka leo ni mwaka 1 na miezi 2 na awajasitisha huo mkataba mpka leo kitu kinachoniuzia mim kufanya kazi na kampuny nyingine ya kuuza sim mpka mkataba wao uishe na awajanipa hta shilingi mia mpka sasa....

please wamenitoroka sina mkono mrefu wa kuwakamata zaidi ya huruma yenu na wanacho kiwanda kikubwa tu uko kwao china cha KZG kwasasa ninachohitaji kuliko chochote ni afya yangu kwanza
Ukiguswa kwa chchote nipo na unanipata kwa no hii.
0768666113
0768666113"
 

Msanii wa filamu Wastara Juma amepaza sauti yake ya kutaka kusaidiwa pesa ya matibabu na Rais John Pombe Magufuli baada ya kutapeliwa na kampuni moja ya simu ambayo ilimteua kama balozi wa bidhaa zao.

Huyu mhanga anaomba msaada halafu amevaa gold chain, mbona kama akili haijiongezi? Fikiria unayemwomba msaada hata shanga za 2000 hana hivi atakuonea huruma kweli? Kwanini asijiweke katika mwonekano wa kutia huruma kuliko hivi alivyo kweli ni vigumu sana kumwonea huruma kwa mwonekano huo.

Hebu huyu dada ajifikirie halafu atoke kivingine na namtakia kheri katika hiyo harakati yake ya kuomba msaada kweli Mungu anaweza kumsaidia ila aangalie sana huo mkufu wa dhahabu aliovaa hauendani na tukio.
 
Sasa amevaa dhahabu inahusiana nini na deni analodai??kwahiyo awe mchafu mchafu kisa anapmba msaada kwa haki yake!!!!!
Kali ya mwaka
Unaomba msaada usaidiwe halafu uko kwenye gari la nguvu ambalo wa kukupa msaada hanalo hivi anaweza kukuonea huruma kweli? Elewa hapa anatakiwa kuonewa huruma si akae kihuruma huruma pia? Halafu na wewe haujiongezi kama yeye.
 
Unaomba msaada usaidiwe halafu uko kwenye gari la nguvu ambalo wa kukupa msaada hanalo hivi anaweza kukuonea huruma kweli? Elewa hapa anatakiwa kuonewa huruma si akae kihuruma huruma pia? Halafu na wewe haujiongezi kama yeye.
Hilo unalitaka wewe sasa,na yeye ndio hayupo hivo. Kwahiyo kila anaedai na kuomba msaada akivaa vizuri asisaidiwe kisa kavaa vizuri? Au asaidiwe kisa kuvaa ovyo!??faking situation na mazingira??? Jiongeze wewe hapo,hata hujiongezi kwamba Hiyo picha imetoleea katika mitandao ndio ikaambatanishwa na habari??
Zuzu
 
Hilo unalitaka wewe sasa,na yeye ndio hayupo hivo. Kwahiyo kila anaedai na kuomba msaada akivaa vizuri asisaidiwe kisa kavaa vizuri? Au asaidiwe kisa kuvaa ovyo!??faking situation na mazingira??? Jiongeze wewe hapo,hata hujiongezi kwamba Hiyo picha imetoleea katika mitandao ndio ikaambatanishwa na habari??
Zuzu
Povu lote la nini bidada?
Kama yuko sahihi futa povu then mpe msaada...
 
Amekosa maarifa, serikali haina pesa kuna watu wanajitokeza hadharani kuwa wana pesa ......haendi huko ila anakomaa na magu.

Angeenda kuchungulia zile fomu za kuonyesha mali za viongozi. Fomu yenye salio kubwa bank ndio angemfuata ili ampatie msaada...hahahaa!
 
Back
Top Bottom