GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 60,426
- 120,778
Nilidhani tu kuwa UNYANYASAJI uko tu nchi za Wenzetu lakini katika hali ya KUSHANGAZA na ya KUSIKITISHA kumbe hata hapa Tanzania kwetu hali ni ile ile na yawezekana ikawa pia imezidi japo haizungumzwi.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kabisa na ambayo binafsi nimeishuhudia leo asubuhi maeneo ya Bahari Beach ambapo Kijana wa Kazi ( Shamba Boy ) alikuwa akikata Michongoma katika nyumba ya Bosi wake ambapo mara zote alikuwa akiimba nyimbo ya Msanii Rich Mavoko yenye kipande kisemacho " Wazee wa zamani walisema UKIWA MJANJA KUCHAPIWA NI SIRI YA NDANI....roho yangu mie.....roho yangu mie....".
Inasemekana ni kwamba jambo ambalo lililomkwaza Bosi wake hadi kumfukuza Kazi huyu SHAMBA BOY wake ni kitendo chake cha kuimba kipande hicho kwa sauti ya juu kila akimwona Bosi wake huyo au wakipishana nae hali ambayo ilimfanya huyo Bosi ahisi pengine huyo Shamba Boy anatembea na Mkewe au kuna jambo nyeti analijua.
Alipohojiwa mara baada ya kufukuzwa Kazi rasmi leo asubuhi kwamba kwanini na yeye alikuwa akiimba hicho kipande cha huo wimbo wa Rich Mavoko kwa sauti ya juu kila Bosi wake akitokea alijibu kwamba namnukuu " Kusema ukweli Mimi nilikuwa nafanya vile makusudi ili ajue kuwa naweza / najua kuimba na anisaidie kukiendeleza Kipaji changu na wala kusema ukweli hakuna jambo lolote baya nalifanya au anafanyiwa ".
Baada ya hali hii kumtokea huyu Shamba Boy aliponiona napita njia akanikimbilia kuniomba ushauri wa Kisheria ya nini cha kufanya kwani anaona AMEONEWA na pia kufukuzwa kwake Kazi ni kama vile AMEDHALILISHWA halafu isitoshe hana pa kwenda hapa na hapa Dar hana Ndugu.
Wanasheria mliopo humu TAFADHALI nisaidieni na USHAURI wenu ili nami niweze kumsaidia huyu SHAMBA BOY kwani kiukweli kwa mazingira ya KUFUKUZWA Kwake Kazi si kitendo cha HAKI kabisa na Kaka wa Watu anatia hadi HURUMA.