Msanii Kajala katupwa rumande

Msanii Kajala katupwa rumande

Fidel80

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2008
Posts
21,945
Reaction score
4,499
Kajala.jpg


Msanii wa Bongo Movie, Kajala Masanja amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashitaka matatu yakiwamo ya kutakatisha fedha haramu kosa ambalo halina dhamana kisheria na hivyo kurudishwa lupango.
Katika kesi hiyo, Kajala anashitakiwa pamoja na mumewe Faraji Mchambo ambapo makosa mengine ni kula njama na kubadilisha umiliki wa nyumba.
Wakili wa serikali Leonard Shayo mbele ya Hakimu Mkazi Sundi Fimbo alidai kuwa Kajala na mumewe wameshitakiwa kwa kosa la kwanza la kula njama kinyume na kifungu cha 34 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007 ambapo washtakiwa wote walitenda kosa hilo la kuhamisha umiliki wa nyumba iliyopo Kunduchi Salasala jijini Dar es Salaam.
Shtaka la pili walidaiwa kuwa mnamo Aprili 14 2010 walihamisha umiliki wa nyumba hiyo kinyume na kifungu cha 34(2)A(3) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2007.
Ambapo shtaka la tatu walidaiwa Aprili 14 2010 huku wakijua ni kinyume na sheria walifanya kosa la kutakatisha fedha haram ambapo ni kosa lisilo na dhamana kisheria .
Chambo hakuwepo mahakamani kwasababu yupo gerezani mahabusu kwa makosa mengine ambayo hayana dhamana yanayomkabili ya utakatishaji fedha.
Kajala alikana mashtaka hayo na kurudishwa rumande kwa uchungu mkubwa huku akilia pamoja na ndugu zake akiwamo mama yake aliyekuwepo mahakamani hapo.
hakimu Fimbo aliarisha kesi hiyo mpaka Aprili 20 mwaka huu ili kesi ije kwaajili ya kutajwa na pia kutolea maamuzi,maombi yaliyotolewa na wakili wa Alex Mgongolwa anayemtetea kajala.

Source: Kutoka mahakamani Kisutu
 
Pole yake.


Na wewe siku hizi umekuwa mwandishi wa tbc?.. Manake hukaukiwi habari.
 
ooh okie dokie smokie

Halafu sasa, ukiwa na kosa lisilodhaminika huruhusiwi kuja mahakamani?

Interesting...
 
tamaa mbaya tamaaa mbaya... wimbo asilimaine 20%..
 
1+%282%29.JPG


Akiwa mbele ya pirato hapa
 
"kutakatisha fedha" ndio kufanya nini?
 
"kutakatisha" = "laundering" ...! Kiswahili kina upungufu mkubwa wa maneno sorry "vocabulary"
 
Asante sana. Lakini wamezitakatisha kutoka wapi kwenda wapi?

Hapa alilizungumzia hili sakata lake ....take a listen

Ngoja tusubiri ushahidi upande wa mashtaka utasema wamezitakatisha pesa zipi za kiwanja au zilitoka nje ya nchi
 
Utajiju babu weeeeeee na kijiba cha wivu, dume zima una wivu wa kike

weeeee rekebisha kauli yako kabla sijakushushia kipondo cha 'kike' hadharani ebo...
 
Ndo ma sista du wakome kupapatikia ma pedejhee,ambao hawajui vyanzo vyao vya mapato! Pole we!
 
weeeee rekebisha kauli yako kabla sijakushushia kipondo cha 'kike' hadharani ebo...

Madume kama hayo dawa ya ndogo jamaa lina wivu wa kike
 
Fidel80 kumbe wewe ni mwandishi wa habari wa kujitegemea lol sasa ndo nimeamini
 
Fidel80 kumbe wewe ni mwandishi wa habari wa kujitegemea lol sasa ndo nimeamini

hujamtmjua Fide matron, hapo mwangalie huyo mlimbwende kisha ujipe majibu...chezeiya Fide weweee !!!
 
Huyu dada nae mume wake ana moyo, P-Funk amempiga tattoo mwabwepande, mferejimaringo kote ni signature ya majani, sijui kila akimvulia na akiona hayo matattoo sijui anamtathimini vipi mpenzi wake?
 
Back
Top Bottom