Msanii Chid Benz akamatwa tena na dawa za kulevya

Wampe kifungo cha mwaka mmoja jela,akitoka atakuwa ameshasahau hayo madawa
 
Sheria zikoje?

Au labda Mimi ushamba bado unanisumbua!

Nijuavyo Mimi ni kwamba, huwezi kukaa Kituo cha Polisi zaidi ya masaa Ishirini na Manne (24).

Ni kwamba mpaka Masaa Ishirini na Manne (24) yakishapita bila wewe kufunguliwa Mashitaka, basi hapo hamna Kesi tena.

Kinachotakiwa ni kwamba ndani ya Masaa Ishirini na Manne (24) uwe umeshapandishwa Mahakamani, na kama kuna Upelelezi wowote unatakiwa uwekwe Mahabusu huku ukiwa tayari umeshapanda Mahakamani.

Sasa hii ya kuwekana Kituoni Siku tatu na Mtu bado hajapandishwa Mahakamani imekaaje?
Wanatafuta ushaidi,Hapo siasa itakuwa imeshaingia
 
Cc: Rodrigo Duterte
philippines-duterte.jpg
 
Huyo mtu ni janga kwa familia na taifa kwa ujumla,ukichukulia kuwa yeye ni kioo cha jamii.
 
Ndiyo maana, China wanawapa zawadi ya bomba kumbe wao wanaelewa kabisa kuwa hawa jamaa huwa hawaachi hii kazi.

An way, RIP wote waliouliwa kwa dawa hizo, na pole sana kwa wote wanaotesaka kwa sababu ya hizi mambo za hawa punda.
 
Sijui ni kwa nini watu wengi hawakupenda ile kasi ya Mheshimiwa Makonda ambayo kwa upande wangu ilitoa picha halisi juu ya kiwango cha biashara hii haramu ya madawa ya kulevya na ukubwa wa madhara kwa nguvu kazi ya taifa hili! Sijui!!!
Ila ninachofahamu, ni juu ya jinsi gani jamii inavyoweza kuondolewa kwenye hoja za msingi kwa kuelekezwa kujadili watu!
Mbali na huyu kijana Chid Benz, ambaye nyota yake inaonesha kutoweka, kunao wengi ambao tunawaona kwa dhahiri wanavyoangamia kwa sababu tu hatukutaka kumuunga mkono Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa ambao ni lango kuu la kuingizia madawa haya nchini.
Tujutafakari!
 
Sasa hata sielewi tena hii issue ya madawa. Nilidhani imekwisha hasa baada ya zile jitihada za Makonda na Mh. Raisi. Kumbe mambo yapo hadharani kama kawa.... Sasa inamaana zile jitihata zimefeli?
 
Unaweza kuwa na tatizo dogo lakini vile unalitatua lisikupe matokeo chanya au matokeo ya kuonekanika.Roho ii radhi lakini mwili u dhaifu. Kuna vitu vingine wakuna nafsi ndo inayougua sasa ukimpeleka magereza sana sana utamzika huyu mtu. Kuitibu nafsi lazima ujue alianzaje kuna stori ndefu. Kati ya haya mawili hakuna mwenye nia ya dhati ya kumsaidia huyu kijana au wote wanaojaribu kumsaidia hawajui jinsi ya kumsaidia.
 
Tatizo la Chid Benz ni moja tu. Anashindwa kujizuia emotions zake hasa akipata hela.

Ukijaribu kuangalia hii histori ya Chid kurudia Madawa ndio unapata picha.

1. Baada ya kupelekwa Rehab na Bab Tale. Alipotoka alitoa ngoma ya Chuma ft Rayvan. Akaanza kushika hela. Emotions za madawa zikamshinda nguvu. Akadondoka.

2.Alipelekwa Rehab ya Siri na Mdau mmoja hivi ambae hakutaka ajulikane. Alipotoka tena akatoa Ngoma ya MUDA ft QChillah. Akaanza kushika hela. Emotions za Madawa zikamshinda.
Akaanguka.

Kwahii picha naona Hatima ya Chid inatakiwa asishike hela mwenyewe. Awe anapewa Mahitaji yake kwa uangalizi maaluma mpaka muda flani upite.
Na hichi kitu Chid Mwenyewe hapendi ndio kisa cha Kugombana na Babu Tale.

sent by Samson Cyper
Chidi kwa imani yangu kinachoumwa ni spirit being, nafsi yake iko mateka iko kifungoni ni spiritual zaidi, ukimfungia hata ufanye nini atarudia kwa sababu kinachomshikilia bado hakijaachia. Kama alivyosema Mshana jr vitu vingi vinaanzia ulimwengu wa roho ndo tunapata matokeo ulimwengu wa nyama na damu. Binadamu tunavitu viwili , tuna nafsi(roho) na mwili. Chakufanya kwanza ayakatae matendo ya mwili yaliyoleta madhara ya nafsi yake baada ya hapo kuingia kiroho kupambana ili nafsi yake iachiliwe ndipo tutaona matokeo chanya. Hakuna jambo linalomshinda Mungu. Tuliambiwa msinililie mimi zililieni nafsi zenu .....
 
Back
Top Bottom