Msanii afufuka huko Bondeni baada ya kufariki miaka2

lutayega

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
1,288
552




Mtu huyo anasema yeye ni Khulekani "Mgqumeni" Khumalo - mwanamuziki wa nyimbo za kiasili za Kizulu ambaye alifariki mwaka 2009. Hata hivyo alizuka katika nyumba ya familia yake wiki iliyopita akidai kuwa alikuwa ametekwa na mizuka.
Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi wamesema atashtakiwa kwa udanganyifu iwapo vipimo vya DNA vitaonesha anadanganya.


Familia yake wakiwemo wake zake wawili, wanasema anaonekana kuwa ndio mwenyewe - lakini polisi
Mwandishi wa BBC mjini Johannesburg, Nomsa Maseko amesema polisi wanatarajia kupata majibu ya vipimo vya DNA baadaye wiki hii - na mpaka wakati huo mtu huyo atasalia kizuizini. Kesi hiyo imezua kizazaa nchini Afrika Kusini - na siku ya Jumapili iliyopita, maelfu ya mashabiki walikwenda Kwazulu-Natal kushuhudia "kutolewa" rasmi kwa mtu huyo.

Akitumia kisemeo, aliwaambia mashabiki wake kuwa hakuwa amekufa - lakini alipotea baada ya kuchukuliwa na wachawi. Amesema alifungiwa katika pango na mizimu kwa miaka miwili, na alilazimishwa kuimba na kulazimika kula matope ili asife kwa njaa. "Nimepoteza uzito mwingi lakini ni mimi," alisema. Mtu huyo, alitaja majina ya ukoo wake.

Polisi wa Afrika Kusini wamesema wanashughulikia mkasa huo kwa kufanya upelelezi wa kesi ya uhalifu.


 
hii ni habari ya sikunyingi sana. Vipimo vilionyesha kuwa sio yeye na ana kesi ya kujibu mahakamani.
 
Habari hii ni ya siku nyingi sana,na ilishathibitika kuwa walikuwa wanafanana tu!
 
Back
Top Bottom