Msanii Selementally ambaye ameachia kazi yake mpya inayoitwa 'Nataka kununua Dar' aliyomshirikisha msanii Belle 9, amesema anakusudia kulinunua jiji la Dar es Salaam ili arekebisha baadhi ya vitu ambavyo anaona haviko sawa.
Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Selementally amesema anakerwa na tabia ya watu kuamini kila kitu kipo Dar es Salaam peke yake na kukimbilia huko, huku wakiacha fursa kwenye mikoa wanayotoka.
"Dar es Salaam imetengenezwa kuwa kila kitu lakini nataka kufanya mageuzi, nataka watu wote wahamiaji warudi walikotoka, unaweza ukawa na kipaji ukatoboa hata kama ukiwa Mbeya, nataka kuinunua Dar es Salaam nirekebishe baadhi ya mambo ambayo naona hayako sawa, nimechoka kusikia kila kitu Dar, Mbunge wa Mbeya vijijini anakaa Mikocheni na ilibidi wabunge wakae majimboni, watu wanawekeza sana Dar es Saalam wanakosa fursa mikoani", amesema Selementally.
Selementally ambaye watu walianza kumfuatilia kwa ukaribu zaidi baada ya kufanya vizuri kwenye Dakika 10 za Maangamizi kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, amesema wazo hilo ndio lililomfanya aandike wimbo wake wa 'Nataka kuinunua Dar'.
Itazame hapa kazi yake mpya akiwa na Belle 9.