Msando vipi tena | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msando vipi tena

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by superfisadi, Feb 15, 2011.

 1. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Msando amburuza kortini Mwanasheria Mkuu wa serikali


  na Grace Macha, Moshi


  [​IMG]
  DIWANI wa kata ya Mabogini, Albert Msando (CHADEMA), amemfikisha mahakamani Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi akipinga taratibu zilizotumika kumchagua mwenyekiti wa halmashauri hiyo.
  Kesi hiyo namba moja ya mwaka 2011 ilifikishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya Moshi, Simon Kobelo, ambapo diwani huyo anapinga utaratibu uliotumika wakati wa mkutano wa halmashauri hiyo uliofanyika Desemba 17, 2010 aliodai ulikiuka sheria na kanuni za uchaguzi wa mwenyekiti wa Halmashauri ya Moshi.
  Msando ambaye ni wakili machachari wa kujitegemea alidai kuwa katika uchaguzi huo kulikuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu na sheria kwani madiwani waliapishwa na mwanasheria wa halmashauri badala ya hakimu mkazi au wa wilaya inavyotakiwa kisheri.
  Aliieleza mahakama hiyo kuwa dosari nyingine katika uchaguzi huo ni kitendo cha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Anna Mwahalende, kujiteua kuwa msimamizi wa uchaguzi wa mwenyekiti na makamu wakati sheria inataka madiwani kumchagua mwenyekiti wa muda miongoni mwao ili aendeshe zoezi la uchaguzi.
  Hivyo aliiomba mahakama kutengua matokeo ya uchaguzi huo ili kuruhusu madiwani wa halmashauri hiyo kuapishwa na hakimu mkazi pamoja na uchaguzi huo kurudiwa. Kwa upande wake wakili wa serikali, Abdalah Chavulla, aliwasilisha mahakamani hapo hati ya kisheria akipinga madai hayo na kuiomba mahakama hiyo kuisikiliza kesi ya msingi kwa njia ya maandishi jambo ambalo lilipingwa na diwani Msando ambapo hakimu Kobelo alikubali pingamizi hilo hivyo kesi hiyo itaendelea kusikilizwa kwa njia ya kuongea jambo ambalo litasaidia kupunguza muda wa kusikilizwa kwa kesi hiyo. Katika uchaguzi huo diwani wa kata ya Okaoni, Moris Makoye (CCM), alichaguliwa kuwa mwenyekiti na Meja Jesse Makundi wa TLP alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti ambapo Msando alikuwa ni mgombea wa nafasi ya uenyekiti kupitia CHADEMA.

  My take
  kumbe wanajf ni wabishi mpaka uraiani?:msela:

  [​IMG]
   
 2. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyo jamaa namfahamu. Ni balaa!
   
 3. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,085
  Likes Received: 4,032
  Trophy Points: 280
  safii sheria ni msumeno!
   
 4. Rwamuhuru

  Rwamuhuru Member

  #4
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu sio swala la ubishi. swala ni sheria na taratibu kukiukwa. ule wkt wa kuitika hata kama hujaitwa kisa hofu umepita
   
 5. c

  carefree JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  hivi ukiwa wakili kumbe waweza kujitetea mwenyewe mahakamani?
   
 6. s

  superfisadi JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 552
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nadhani inakubalika vinginevyo hapo asingekubaliwa
   
 7. c

  carefree JF-Expert Member

  #7
  Feb 15, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  sf sikutaka unijibu wewe nimemuona msando mwenyewe yumo jukwaani nikataka anipe ufafanuzi wa kisheria
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri, kudai haki kila kona
   
 9. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naruhusiwa kulalamika hata kama ni mwanasheria. Kwa sababu mimi ni mlalamikaji (Petitioner) nina haki ya kujieleza mbele ya mahakama (sio kujitetea).

  Kesi hiyo (without prejudice) ni kupinga kitendo cha Mkurugenzi kumtumia mwanasheria wa halmashauri kuapisha madiwani kabla ya Mkutano wa Kwanza wa Kawaida na kabla ya kushika Wadhifa. Kitendo hicho kimesaidia kubaini kuwa Halmashauri ya Moshi kwa miaka zaidi ya kumi imekuwa ikiendeshwa bila kanuni huku Mkurugenzi akiendelea kuandika barua na kunukuu kanuni ambazo hazipo.

  Baada ya kuhoji ni kanuni ipi anatumia ndipo alipokiri kwamba kanuni hazijawahi kupitishwa wala kusainiwa na Waziri husika!!

  Jambo la msingi ni kuonyesha jinsi gani uzembe unaweza kushamiri na kutusababishia hasara za mabilioni kama Dowans nk.

  Ukiniuliza inawezekanaje Halmashauri ikaendeshwa kwa muda wote huo bila kuwa na kanuni za kuendesha mambo yake na inawezekanaje Mkurugenzi akaruhusu Mwanasheria wa Halmashauri akaapisha madiwani wakati kuna Mgombea wa CDM Mbeya aliapishwa kwa wakili akaenguliwa kugombea ubunge!!

  Mahakama itaamua usahihi wa jambo hilo!
   
 10. jino kwa jino

  jino kwa jino JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 769
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mkuu mbona hapa jf tuliambiwa halimashauri ya Moshi inaongozwa na chadema ilikuwaje? na mnamadiwani wangapi?dhidi ya ccm na tlp naomba ufafanuzi mkuu
   
 11. Taluma

  Taluma Senior Member

  #11
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 159
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  watabana wataachia tu, wamekalia kuti bovu......!
   
 12. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Usichanganye kati ya halmashauri ya moshi mjini na halmashauri ya moshi vijijini mkuu
   
 13. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Msando weka Avatar ya picha yako original kama kina Regia bwana!
   
 14. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Paulo sitaki utani na wewe. Na kama unataka kunidhalilisha jiandae kupanda kizimbani! Uwezo wa kufanya hilo sio wa kila mtu ndugu yangu. Matumizi ya computer yamekuja ukubwani!! Email address nimefungua mwaka 2002! Nitupie private msg kama kweli unania njema na mimi ukinipa maelekezo nifanyeje kuweka! La sivyo utaniadhiri mbele ya kadamnasi.

  Ila sina tatizo na hilo, nikielimika jinsi ya kuweka nitafanya kamanda! Nashukuru kwa angalizo!
   
 15. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona ni simple tu mkuu! Ngoja nikutengenezee video clip ya jinsi ya kuweka picha yako fasta. Nipe dk chache tu, provided power will not go off as we are now using generator and the time to switch it off is almost up!
   
 16. Paulo

  Paulo JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 350
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Mbona ni simple tu mkuu! Ngoja nikutengenezee video clip ya jinsi ya kuweka picha yako fasta. Nipe dk chache tu, provided power will not go off as we are now using generator and the time to switch it off is almost up!
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  BERRTOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO KIJANA ANANIKUMBUsha MBALI SANA THOSE DAYS NA mwili wake mdog kijana wangu LAKINI MPIRA ANAOPIGA UTASEMA MHAMED HUSSEIN...ANYWAY SION CHA KUJIBU MAANA MWANDISHI UMEJIULIZA ALAFU UMEJIJIBU TAYARI..SUBIRI MATOKEO KOMAA NAO KAKA NAFIKIRI UMEFIKA WAKATI WA KUDAI HAKI YAKO KIVYAKO NA HIKI NDICHO KIOJA WALICHOCHEMSHA CCM WAMEINGIA CHOO CHA KIKE KABLA YA KUJUA MLANGO AWAJAFUNGA
  HIGHhhhhhhhhhhhhhhhh one time!!
   
 18. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pdidy hunitendei haki kamanda! The old good days!! Sasa kwa hili jina am left to guess who this is!

  Ila the use of 'Berto' inanikumbusha kipindi ambacho life was really good, lots of footballing, laughing and fun. Hopes were high about this country! Look at us now!
   
 19. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  msando usiweke wengine wako kazini humu kaka kila la kheri mkuu natamani ningekuwa lawyer wako maana hapo si simba wala yanga unashinda unazivuta mwenyewe haya ggodday kaka
   
 20. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Madiwani wa TLP na Chadema pamoja na Mbunge 1 jumla tuko 23. CCM madiwani na Wabunge 2 jumla wako 22! Kura ikapigwa wakapata kura 23! Msimamizi Mkurugenzi!!

  TLP walishirikiana nasi na wameendelea na ushirikiano huo. Mh. Lyatonga Mrema alisaini hati ya Ushirikiano pamoja na Mh. Mbowe kama wenyeviti wa Taifa.

  Bado tunashirikiana na TLP. Mpaka sasa umekuwa ni ushirikiano wenye manufaa kwa sababu tunaweza kupinga jambo na kuhoji na itakapokuja kura ya kunyanyua vidole tunaweza kuzuia kwa wingi wetu.
   
Loading...