Msami afunguka ishu ya kutokuwa na Nandy kimapenzi

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,515

Msanii wa Bongo Flava, Msamii amesema si kweli kwamba ameshawahi kutoka kimapenzi na Nandy.

Muimbaji huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma katika mahojiano na Bongo5 amesema Nandy ni kama dada yake hivyo hawezi kufanya hivyo.

“Nandy sijawahi kupita naye ni kama mdogo wangu, dada yangu, kwa hiyo kwa sasa hivi mimi na Nandy ni kaka na dada, let say mimi ni mtu ambaye nimetoka kwenye familia ya THT Nandy pia kwenye familia hiyo hiyo, tupo familia moja” amesema Msami.

Msami anaungana na rapper Bill Nass ambaye amekuwa akidaiwa kuwa na mahusiano na Nandy kitu ambacho amekuwa akikikanusha kila mara.


Muungwana
 
nandy si ney kasema kamrithi ruby bas ruge,bdozen,mchomvu,kipanya,na soudy wanapita
 
Sijawah sikiliza wimbo wa nandy mpak mwisho...naona aapigiwa promo sana na clouds ila ni wa kawaida sana..wapo weng wasanii wa kike wenye uwezo ila machine ni Maua sama...huyu dada next level aisee
 
Sijawah sikiliza wimbo wa nandy mpak mwisho...naona aapigiwa promo sana na clouds ila ni wa kawaida sana..wapo weng wasanii wa kike wenye uwezo ila machine ni Maua sama...huyu dada next level aisee
ila mkuu, sikatai kuwa promo ni kitu muhimu sabb inasaidia kuitangaza bidhaa husika, ila muziki ni tofauti na michezo (basketball,tennis,soccer etc.) muziki huwa hauna formula.
Pia ktk muziki huwa kila mtu ana kitu chake kinachomvutia ktk wimbo, na watu hatuwezi kuwa sawa ktk upenzi wa vitu.. Mfano, wewe unaweza kuuona wimbo "A" ni mzuri sana na unakubamba vilivyo, ila wimbo huo huo "A" kwa mtu mwngne akaona mbona ni wimbo wa kawaida tu.
ila kweny michezo (soccer, basketball,tennis etc.) mara nyngi hakunaga hizo, maana unawezakuwa humkubali mwanamichezo flani lakin unajkuta unasema, "jamaa flani silikubali lakini linajua".(Maana linafanya vitu na vinaonekana sabb ni rahisi kuonekana kulko ktk muziki)
ila kwny muziki ngumu sana kupima vitu maana km ingekuw ni uwezo wa kuimba tu pekee ndo unakufanya uwe juuu ya wasanii wenzio basi kuna wasanii wengi sana wa kwny "mainstream music" wasngekuwa walipo, maana kuna watu wana sauti balaa na hawana mafanikio kimuziki, maana muziki una mambo mengi sana na huwa hakunaga formula ktk kutengeneza hit-song.
(Mtu "A" mwnye bonge la vocal anaweza kupata promo ya kutosha na bado asiwe anakubalika kivileeeee kw nymbo zake kitaani,
Afu upande mwngne mtu "B" mwnye vocal ya kawaida anaweza akapata promo na akajkuta anakubalika kitaa)
 
Back
Top Bottom