Msamaha kwa mafisadi na mwaka mpya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msamaha kwa mafisadi na mwaka mpya.

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Keynes, Dec 31, 2010.

 1. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Ndugu wana JF.
  Kwa muda mrefu tumekua tukipiga makelele ya ufisadi bila kutoa muafaka au solution.
  Kutokana na uongozi wa nchi kuonekana kua umeshindwa kurudisha maliasili zilizoibiwa na mafisadi na kufichwa nje ya nchi kwa mantiki kwamba katika kila dili la ufisadi ni viongozi wengi wa serikali wameshiriki kiasi kwamba wanashindwa kujiwajibisha wenyewe.

  Ukiangalia swala la EPA kama ni kuwajibishwa viongozi ingebidi mpaka rais ajiuzulu maana serikali nayo imeshiriki direct kupitia kagoda na meremeta. Je tunaweza kushinikiza serikali yote ijiuzulu? Jibu ni hapana maana wakijiuzulu wote nani atampeleka mwezake mahakamani? Na je ikijiuzulu hizo hela walizoficha nje ya nchi tutazipataje? Maana kuna viongozi wengi wenye fedha nyingi nje lakini hakuna ushahidi kua walizipataje au waliziiba wapi!!

  MY POINT
  Kwa sababu mafisadi wamekua wakiiba fedha na kuficha nje ya nchi ambapo uchumi wa tanzania umezidi kuzorota kutokana na capital flights wakati nchi za nje ambazo ni matajiri kama Uswiss wananchi wao wanakopa hizo hela walizoficha mafisadi huko na kuzitumia kama mitaji.
  Je mwaonaje serikali ikitangaza msamaha kwa mafisadi wote walioficha hela nje ya nchi na kuwataka waje kuwekeza tanzania then tukaanza upya??

  Pili usalama wa taifa ungefanya utafiti wa akiba zilizopo nje na wenye hela zote nje zirudishwe kwenye mabank ya tz na wahusika waruhusiwe ku invest ndani ya nchi ili kukuza ajira.
  Angalieni mfano mdogo wa ile bilion mzee wa vijisent aliyoficha nje kule inafaidisha wengine wakati tz watu hawana mitaji.

  Tatu baada ya hayo yote kufanyika sheria ya takukuru iimarishwe ili rushwa na kujilimbikizia mali kwa viongozi kusijirudie tena.
  TUKI KOMAA NAO SANA KUWAFUNGA HATUWEZI NA HELA ZINAZIDI KUPOTEA
  Yangu ni hayo karibuni!!
   
 2. Keynes

  Keynes JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Tumeshapuliza filimbi ya vita dhidi ya ufisadi siku nyingi ili wale wasio na dhambi juu ya mali za umma wachukue mawe wawaponde hawa mafisadi lakini hakuna aliyethubutu.
  Hii inamaanisha serikali yote imeoza!!!!!!!!
   
 3. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,088
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  mapinduzi tu yawe ya kiraia au ya kijeshi ndio suluhisho then tuanze mwanzo. Hakuna kuwachekea hawa nyani tutavuna mabuwa.
   
 4. C

  Chagula Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MAFISADI Tanzania walianza tangu siku ile Mwinyi alipotangaza OPEN MARKET, maana hata mbwa alianzisha business na kununua shea mabalimbali katika makampuni mbalimbali. Matokeo yake, nani atamfunga mwenzie, mahakama ni mafisadi, polisi ni mafisadi. Nchi nzima imejaa mafisadi, toka rais hadi wafagia barabara.

  Suala la kuwasamehe halitoshi. Kama kuna mtu mwenye uwezo na busara, hizo pesa walizowekesha nchi za nje ziwe frozen kama walivyomfanyia Malima na vijisenti vyake alivyokuwa amewekeza Uingereza, matokeo yake alipokwenda huko ili atumia, mwanae akamwambia "baba hela zimezuliwa", akazirai na kufariki.

  Wakati umefika wa kuirudishia Tanzania TAIFA lake, TAIFA limekufa tangu siku ile Mwinyi atangaze, iliyobaki ni NCHI tu. najua Rais Kikwete hawezi kufanya lolote maana naye ana chake somewhere, isitoshe hawa MAFISADI wana uwezo mkubwa kwa kutumia hizo pesa za kuweka mawakili shujaa, kiasi kwamba Rais anaogopa kuwafungulia mashitaka maana itaigharimu serikalo pesa nyingi sana, na hasa ukizingatia kuwa Wafadhili wameanza kushtuka kutoa misaada kwa vile tunakula tu bila kujali kujenga Taifa.

  Watanzania wakati wa vitendo umefika, tuache kuogopana tuseme ukweli na ikiwezekana hawa mafisadi ambao tuna ushahidi nao wafikishwe mbele ya sheria siyo kuunda tume ya kuwachunguza na kuwapeleleza na kuandika makaratasi chungu nzima, then hamna kinachofanyika.

  Watafutwe Polisi waaminifu na Mahakimu waaminifu, kesi zifunguliwe na ziendeshwe KISHERIA, kam haiwezekani, basi zipelekwe kwenye BARAZA la kimataifa kama Rais anaogopa kuwashtaki wakati anajua wana pesa zetu na bado wanatamba.

  WAKATI NI HUU TUSINGOJE KESHO.
   
Loading...