Msalato International Airport kwenye mpango

Msalato International Airport kwenye mpango

GwaB

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2014
Posts
5,210
Reaction score
7,052
Nimekutana na huu muundo wa uwanja wa ndege wa kimataifa unaotarajiwa kujengwa Dodoma na kushawishika kuunga mkono pale ambapo huo muundo utatumika. Tujikumbushe, huko nyuma wakati T3 ya Dar es salaam ikiwa kwenye mipango, tuliwahi kuona miundo kadhaa ya kuvutia ambayo haikuwahi kutumika wala haifanani na kile kilichojengwa pale Kiwalani.

Kule Mwanza Mbeya vile vile, kuna majengo ya abiria yanajengwa ambayo kwa jinsi nilivyoona muundo wake na hadhi na hasa ule wa Mwanza kibiashara ni vitu viwili tofauti!. Natarajia kuona uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato utakaolingana na hadhi ya makao makuu ya nchi iliyoko kwa sasa kwenye kundi la MIC- nchi zilizo na uchumi wa kati.

Mungu Ibariki Tanzania.🙌
Screenshot_2020-07-07 Gilbert Alfred Bigil ( GBigil) Twitter.png
 
Back
Top Bottom