Msalaba unapovunjika

Msalaba unapovunjika

BabM

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
1,166
Reaction score
956
Japo nı muda mrefu umepita lakini nimeoma nishee nanyi mkasa huu. Jirani yetu ambaye alikuwa na watoto watano wakike watatu na wakiume wawili. Hata hivyo baba akawa na uhusiano mbovu na mzaliwa wake wa kwanza wa kiume. Inasemekana alikuwa akimpendelea na kumsapoti huyo mtoto mwingine wa kiume. Huyo mtoto wa kwanza akaoa lakini baba hakumsapoti zaidi ya kumpatia banda kwa ajili ya kuishi. Kijana alipoone ametengwa akaamua kujinyonga. Nakumbuka tulienda kuchungulia dirishani baada ya tukio, marehemu alikuwa amejinyonga na kama ya manila na ilikuwa imejivuta kiasi kwamba alikuwa anaonekana amekaa chini mkono mmoja ukiwa kitandani. Kila mtu alikuwa anasema lake na wengine wakidai baba kamloga. Kutokana na kujiua padri hakuja na alizikwa bila sala zaidi watu waliruhusiwa kumuangalia. Mtoto wa baba mkubwa wa marehemu alikuwa akiongea wazi kwamba baba mzazi wa mtoto ndio kamloga. Wakati wa kuzika huyo kaka wa marehemu alikuwa amelewa sana na alikuwa akiimba wimbo wa kamanda. Bada ya kuzika jambo la ajabu lilitokea. Baba alitakiwa akaweke msalaba kaburini. Wakati akaiushindilia msalaba ukavunjika vipande viwili. Hapo tena butwaa ikawapiga watu na sasa ndio watu tena wakona marehemu kaukataa msalaba kutokana na dhulma za baba au uchawi. Kwa kweli huyo baba alibaki ameduwaa mpaka mtu akamwambia aulaze tu juu ya kaburi.

ni tukio la ajabu na siwezi lisahau
 
Sasa ulipovunjika ikawaje mara baada ya kuduwaa???
 
Aliambiwa aulaze tu juu ya kaburi. Mazishi hayakuwa na kiongozi maalum hivyo ilikuwa ni vurugu tu. Unajua huyu alishakuwa anatuhumiwa sana. Hata kwenye kutoa heshima baadhi ya vijana walitaka kumzuia. Hivyo msalaba kuvunjika ikawa ndio uthibitisho kwa wenye madai yao. Hata kwenye kuweka msalaba pia walitaka kumzuia lakini wazee wenye busara wakaingilia kati

Enhe ikawaje
 
Back
Top Bottom