View attachment 3453929
View attachment 3453932
MONALISA JOSEPH NDALA | 0657299225 | 0741299226 |
ndalamonalisa50@gmail.com
26 Agosti 2025
TAARIFA KWA UMMA
KUHUSU UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSIANA NA MALALAMIKO YANGU DHIDI YA UTEUZI WA BW. LUHAGA JOELSON MPINA KAMA MGOMBEA URAIS WA ACT-WAZALENDO
Mtukumbuke kuwa mimi Monalisa Joseph Ndala niliwasilisha malalamiko Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nikionesha dosari za kikatiba na kikanuni katika mchakato wa uteuzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama chetu cha ACT-Wazalendo.
Ninafuraha kuwaarifu kuwa baada ya majibizano ya kibarua na hatimaye kukutanishwa mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa baina yangu na viongozi wa chama wakiiongozwa na katibu mkuu na mwanasheria mkuu wetu,
Leo Agosti 26, 2025, nimepokea nakala ya barua inayoitoa maamuzi kuhusu malalamiko ambayo kimsingi ofisi ya msajili imekubaliana na hoja zangu kwamba:
1. Kanuni za Uchaguzi za ACT-Wazalendo za mwaka 2024 zinatumika pia katika kuteua wagombea wa nafasi za kiserikali, ikiwemo Urais. (Hivyo mgombea wetu anakosa sifa ya kutokuwa mwanachama siku 7 kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza),
2. Mwisho wa kuchukua fomu za kuomba uteuzi ilikuwa tarehe 25 Mei 2025, kabla ya Bw. Luhaga Joelson Mpina kuwa mwanachama. Hivyo mgombea wetu kuwa nje ya muda wa kimchakato wa kikanuni za kiuchaguzi.
Mtukumbuke kuwa Bw. Mpina alipata uanachama wa ACT-Wazalendo tarehe 5 Agosti 2025, siku 1 kabla ya kutangazwa na Mkutano Mkuu wa chama tarehe 6 Agosti 2025, kinyume na kanuni zetu zinavyotaka. Hakukuw na ushahidi wa kikao chochote cha chama kilichorekebisha ratiba rasmi ya kuchukua na kurejesha fomu.
Kwa msingi huo, Msajili wa Vyama vya Siasa ametamka wazi kwamba uteuzi wa Bw. Luhaga Joelson Mpina ni batili kisheria na hivyo hastahili kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo. (Uteuzi umevunja sheria ya vyama vya siasa sura 258, Katiba ya ACT-WAZALENDO na kanuni za kudumu za uendeshaji wa chama za mwaka 2015 na toleo la mwaka 2024)
Ninapokea uamuzi huu kwa heshima kubwa na ninaona ni ushindi wa kuheshimu Katiba, Kanuni na Sheria za nchi katika kulinda demokrasia ya kweli. Hatua hii imethibitisha kwamba hakuna mtu wala taasisi inayoweza kuwa juu ya sheria.
Natoa wito kwa vyama vyote vya siasa nchini kuhakikisha vinaendesha michakato yake kwa uwazi, uadilifu na kwa mujibu wa taratibu, ili kulinda heshima ya demokrasia na kuimarisha imani ya wananchi.
Pamoja na salamu za CHAMA, "ACT WAZALENDO, Taifa kwanza leo na kesho."
Imetolewa na:
Monalisa Joseph Ndala
Katibu Mwenyekiti, ACT-WAZALENDO (M), DSM.
Naibu Waziri Kivuli, Sanaa, Utamaduni na Michezo
Email:
ndalamonalisa50@gmail.com | Simu: 0657299225
Dar es Salaam
Pia soma GE2025 - Monalisa wa ACT Wazalendo aandika barua kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa kupinga Luhaga Mpina kuteuliwa kama mgombea Urais