GE2025 Msajili wa Vyama vya Siasa: Uteuzi wa Luhaga Mpina ni batili kisheria, hastahili kuwa Mgombea Urais kupitia ACT

GE2025 Msajili wa Vyama vya Siasa: Uteuzi wa Luhaga Mpina ni batili kisheria, hastahili kuwa Mgombea Urais kupitia ACT

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Double standard : Wa CCM aliyejipitisha mwenyewe, kavunja katiba ya CCM waziwazi haguswi hii si sawa; kwani wewe ni msajili wa vyama vingine ila siyo CCM? Maelezo ya kina.
 
Yaani mwanachama anakishtaki chama chake kwa msajili ambaye hawana imani naye ili mgombea wao wa uchaguzi aenguliwe aisee, hilo pingamizi kwa nini halikuanzia ndani hadi mtu anasubiri timing muafaka.Huu si ukachaa kabisa...
Futeni uanachama huyo mama, hakuna chama hapo kwa mwenendo huo, hamjifunzi kwa CCM tu.
Falsafa ya Kaa.
 
MONALISA JOSEPH NDALA | 0657299225 | 0741299226 | ndalamonalisa50@gmail.com
26 Agosti 2025

TAARIFA KWA UMMA

KUHUSU UAMUZI WA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA KUHUSIANA NA MALALAMIKO YANGU DHIDI YA UTEUZI WA BW. LUHAGA JOELSON MPINA KAMA MGOMBEA URAIS WA ACT-WAZALENDO

Mtukumbuke kuwa mimi Monalisa Joseph Ndala niliwasilisha malalamiko Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nikionesha dosari za kikatiba na kikanuni katika mchakato wa uteuzi wa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama chetu cha ACT-Wazalendo.

Ninafuraha kuwaarifu kuwa baada ya majibizano ya kibarua na hatimaye kukutanishwa mbele ya Msajili wa Vyama vya Siasa baina yangu na viongozi wa chama wakiiongozwa na katibu mkuu na mwanasheria mkuu wetu,

Leo Agosti 26, 2025, nimepokea nakala ya barua inayoitoa maamuzi kuhusu malalamiko ambayo kimsingi ofisi ya msajili imekubaliana na hoja zangu kwamba:

1. Kanuni za Uchaguzi za ACT-Wazalendo za mwaka 2024 zinatumika pia katika kuteua wagombea wa nafasi za kiserikali, ikiwemo Urais. (Hivyo mgombea wetu anakosa sifa ya kutokuwa mwanachama siku 7 kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza),

2. Mwisho wa kuchukua fomu za kuomba uteuzi ilikuwa tarehe 25 Mei 2025, kabla ya Bw. Luhaga Joelson Mpina kuwa mwanachama. Hivyo mgombea wetu kuwa nje ya muda wa kimchakato wa kikanuni za kiuchaguzi.

Mtukumbuke kuwa Bw. Mpina alipata uanachama wa ACT-Wazalendo tarehe 5 Agosti 2025, siku 1 kabla ya kutangazwa na Mkutano Mkuu wa chama tarehe 6 Agosti 2025, kinyume na kanuni zetu zinavyotaka. Hakukuw na ushahidi wa kikao chochote cha chama kilichorekebisha ratiba rasmi ya kuchukua na kurejesha fomu.

Kwa msingi huo, Msajili wa Vyama vya Siasa ametamka wazi kwamba uteuzi wa Bw. Luhaga Joelson Mpina ni batili kisheria na hivyo hastahili kuwa Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya ACT-Wazalendo. (Uteuzi umevunja sheria ya vyama vya siasa sura 258, Katiba ya ACT-WAZALENDO na kanuni za kudumu za uendeshaji wa chama za mwaka 2015 na toleo la mwaka 2024)

Ninapokea uamuzi huu kwa heshima kubwa na ninaona ni ushindi wa kuheshimu Katiba, Kanuni na Sheria za nchi katika kulinda demokrasia ya kweli. Hatua hii imethibitisha kwamba hakuna mtu wala taasisi inayoweza kuwa juu ya sheria.

Natoa wito kwa vyama vyote vya siasa nchini kuhakikisha vinaendesha michakato yake kwa uwazi, uadilifu na kwa mujibu wa taratibu, ili kulinda heshima ya demokrasia na kuimarisha imani ya wananchi.

Pamoja na salamu za CHAMA, "ACT WAZALENDO, Taifa kwanza leo na kesho."

Imetolewa na:
Monalisa Joseph Ndala
Katibu Mwenyekiti, ACT-WAZALENDO (M), DSM.
Naibu Waziri Kivuli, Sanaa, Utamaduni na Michezo
Email: ndalamonalisa50@gmail.com | Simu: 0657299225
Dar es Salaam

Pia soma GE2025 - Monalisa wa ACT Wazalendo aandika barua kwa Msajili wa Vyama Vya Siasa kupinga Luhaga Mpina kuteuliwa kama mgombea Urais


=================================

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza alipoulizwa amesema “Ni kweli tumeandika barua kwenda ACT kuwajulisha suala hilo (Mpina kutokuwa na vigezo) na Monalisa amepewa nakala.”

Upande wa Monalisa alipoulizwa kuhusu barua inayosambaa amesema "Ni kweli ni barua yangu. Mimi bado ni Mwanachama wa ACT na nitaishi kwa amani.”

Alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo, Naibu Mwenezi wa ACT Taifa, Shangwe Ayo amesema “Sina hizo taarifa rasmi, nasi tunaziona kwenye mitandao, tukipata taarifa rasmi tutawajulisha."

Majibu ya ACT Wazalendo ~ ACT: Hatutafuata Maelekezo ya Msajili kumtengua Mpina kuwania Urais, tutafunguu kesi Mahakamani
Baada ya kuona Moto wa Mpina kuelekea Ikulu hauzuiliki wameanza kumwekea Zengwe kupitia kwa jike pandikizi Monalisa.
 
Ni katiba ya ACT Wazalendo. Siyo katiba ya nchi.

Swali ni je, Zitto na Masoud ambaye pia aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu Zanzibar hawakulijua hilo?
Huyo msajili kumbuka tu ndie yuleyule aliemrudisha lipumba uenyekiti wa cuf wakati lipumba alishajiuzulu mwenyewe huo uenyekiti
 
Na itawauma mpaka siku mtakabokubali ukweli kuwa CHADEMA ni kubwa kuliko mtu. Yani tushinde halafu ionekane hatujashinda?. Ndio maana mmekimbia wenyewe kwenda CHAUMMA.

Pia Acha kujifariji kwa maneno matamu. Yani hujahudhuria Mkutano umejuaje akidi haikutimia?. Ndio maana tunawaita nyie ni wahuni.
Hapo ndipo mnapojidanganya. Chadema ni kama vyama vingine vya siasa. Vinakua na kupotea vikikosa muelekeo na support. Kenya kulikuwa na KANU, Zambia UNIP na vyote vimepotea. ANC ya Afrika kusini sasa hivi kiko ICU. Zimbabwe MDC kilikuwa mioyoni na tumaini la watu lakini baada ya Tsvangirai na Mutambara kuruhusu ego zao ziwatale nacho basically kimepotea. Mwaka 2008 Tsangirai alipata 47..9 % ya kura ambazo ni zaidi ya alizopata Mugabe katika raundi ya kwanza. Mwaka 2023 mgombea wake alipata 0.65%. Chadema inaeleke huko huko.

Maneno ya kuwa Chadema iko moyoni haisaidii kulipa gharama za kuendesha chama kama watu hawajitolei. Ukimya wenu kuhusu Tone Tone kuna tia wasiwasi. Watu walioshindwa kuchangia gari kwa ajili ya Mwenyekiti wao watatoa wapi pesa za kuendesha chama? Na tunakumbuka ahadi yenu ya kuwa transparent na kutoa taarifa za mapato na matumizi ya chama.

Ingekuwa mnajiamini kuwa mmeshinda msingeanza kampeni ya kutafuta wachawi. Mngeweza kukaa na mliowashinda ili mjenge chama chenu. Badala yake mkaanza vitabia vya udikteta uchwara. Ndio maana wenye busara wakaona isiwe shida wakawaachia chama chenu maana tofauti na mnavyodhani chama cha siasa ni chombo tu. Mtu ukiona hakikufai unakiacha. Hata Mwalimu aliwaambia hivyo CCM.

Kama Mchome alisema uongo, mlishindwaje kutoa daftari la mahudhurio ambalo lingemaliza ubishi? Kusema kuwa tuliwaona hakuna maana yeyote bila ushahidi wa maandishi. Kama mliwaruhusu kuondoka bila kusaini imekula kwenu. Mimi mpaka sasa nashindwa kuelewa mlishindwa nini kuita kikao haraka haraka ambacho kingekuwa na quorum? Au ni ule ujuaji uliowatawala. Kuongoza chama sio kazi rahisi kama mlivyo dhania. jipangeni upya.

Amandla...
 
S

Chanzo cha picha,ACT
Tume huru ya uchaguzi Tanzania (INEC) imeeleza mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina hapaswi kuwania urais Tanzania.
INEC pia imefuta barua yake ya awali iliyohusu urejeshaji wa fomu za uteuzi na kumzuia asifike ofisi ya tume hiyo, huku chama chake kikiri kupokea barua hiyo.
Msajili wa Vyama vya Siasa alitangaza jana kuwa uteuzi wa Mpina kupitia chama chake hicho kipya, haujakidhi matakwa ya kikanuni, kufuatia pingamizi lililowasilishwa na mwanachama wa chama hicho, Monalisa Ndala.
Katika uamuzi uliotolewa Agosti 26, 2025 Msajili alibainisha kuwa Mpina hakutimiza vigezo vya uanachama kwa mujibu wa kanuni za chama, akisema kuwa alijiunga ACT-Wazalendo nje ya muda uliopangwa na hivyo hakustahili kuwania nafasi ya urais kupitia chama hicho.
Kwa mujibu wa malalamiko ya Monalisa aliyoyawasilisha kwa Msajili, mgombea huyo alikiuka sheria ya chama cha ACT Wazalendo kwa kutokuwa mwanachama wa chama hicho siku saba kabla ya mchakato wa uchaguzi kuanza.

Monalisa anasema mwisho wa kuchukua fomu za uteuzi wa mgombea urais ndani ya chama ulikuwa Mei 25, 2025, kabla ya Mpina kuwa mwanachama hivyo mgombea huyo alikuwa nje ya muda kimchakato wa kikanuni za kiuchaguzi.
"Mpina alipata uanachama wa ACT - Wazalendo Agosti 5, 2025, siku moja kabla ya kutangazwa kwenye Mkutano mkuu wa chama hicho wa Agosti 6, 2025, kinyume na kanuni zetu zinavyotaka, hakukuwa na ushahidi wa kikao chochote cha chama kilichorekebisha ratiba rasmi ya kuchukua na kurejesha fomu", ilisema sehemu ya taarifa ya Monalisa kuhusu uamuzi wa Msajili.
Hata hivyo, uongozi wa ACT-Wazalendo kupitia Katibu Mkuu, Ado Shaibu, umetangaza kushtushwa na uamuzi huo na kueleza kuwa tayari wameanza mchakato wa kufungua kesi Mahakama Kuu ili kupinga hatua ya Msajili, wakidai imekiuka taratibu na kuingilia mchakato wa ndani wa chama.
"Chama cha ACT Wazalendo kinaweka msimamo kuwa hakitofuata maelekezo ya Msajili wa Vyama vya siasa juu ya suala hili" inasema taarifa ya ACT na kuongeza kuwa katika kesi itakayofungua itaweka zuio dhidi ya utekelezaji wa uamuzi huu hadi kesi ya msingiisikilizwe.
Kwa mujibu wa taarifa ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), uteuzi rasmi wa wagombea urais umefanyikaa Jumatano August 27, 2025.
Wataalamu wa sheria wameeleza kuwa hata kama Tume itakubaliana na maamuzi ya Msajili, Mgombea huyo bado ana nafasi ya kwenda Mahakamani kuomba zuio la utekelezaji wa uamuzi wa Msajili pamoja na Tume hadi pale shauri la msingi litakaposikilizwa. chanzo BBC
 
Back
Top Bottom