Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
Katibu Mkuu ACT Samson Mwigamba ameibuka na kutoa pongezi rasmi kwa Msajili wa vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi kwa uamuzi wake dhidi ya Chadema.
Mwigamba amesema uamuzi wa Msajili ni Faraja kwake na ni ushindi mkubwa kwani mashtaka hayo aliyapeleka yeye.
Akizungumza jana Mwigamba alisema uamuzi wa msajili kutotambua mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2006 ya Chadema ni wa kuungwa mkono na kila mpenda demokrasia nchini.
Mwigamba ameonya ingawa yuko nje ya Chadema lakini ataendelea kuibua kila udhaifu ndani ya Chadema na anaamini msajili atafanyia kazi kwa maslahi mapana ya demokrasia nchini.Amesema anaamini msajili ataendelea kumpa ushirikiano mpaka pale Chadema watakapokuwa katika mstari.
Souce:UHURU

Wenye mamlaka na Katiba ya CHADEMA ni Chadema wenyewe kupitia vikao hasa Mkutano Mkuu.
Chadema itaendelea kuendeshwa kwa umakini wa kuzingatia misingi ya chama hasa Katiba ya Chama.
Chadema haiwezi kuendeshwa kwa ushauri wala kauli zisizo na msingi wowote kutoka kwa Msajili.
Kama CCM na vibaraka wao wanamuogopa Mwenyekiti Mbowe na Katibu Mkuu Dkt. Slaa, wanastahili pole.
Wenye kujua yupi ana sifa za kugombea na yupi hana, ni wanaCHADEMA kupitia vikao vyao vya Baraza Kuu na Mkutano Mkuu.
Eti kiongozi wa chama kinachojaribu kujionesha kuwa cha upinzani, ananukuliwa kwenye Gazeti la CCM akijivuna kupambana na Chama Kikuu cha Upinzani nchini, kisha mtu huyo huyo na wenzake wakiambiwa wanafanya kazi ya CCM wanang'aka! What a controversy.
Hii nayo ni facts zaidi