Msajili aomba Mwongozo CHADEMA

Msajili aomba Mwongozo CHADEMA

Daima CHADEMA mbele, uasi na uhaini wa Prezzo Matunguri (Zitto) hautupi shida maana dawa ya mchawi ni kumkabidhi mtoto.
 
Ufisadi CHADEMA tukiyajibu haya 2015 asubuhi tunachukua nchi
FREEMAN MBOWE, KIONGOZI ALIYEFANIKIWA KUIFISIDI CHADEMA KWA KUWAAMINISHA WANACHADEMA KUWA MIGOGORO YOTE INAYOTOKEA CHADEMA NI MPANGO WA CCM


Mara zote Mbowe na Slaa wakiulizwa kuhusu migogoro inayoendelea Chadema wao jibu lao ni moja tu “Ni mipango ya CCM kutuvuruga Chadema ni tishio kwao”


Mwanachademe unayejitambua jibu haya:


1. Hivi CCM wanahusikaje na kunyofolewa kinyemela kwa kifungu cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya chadema? (Je Mbowe anatumika pia?)


2. CCM wanahusikaje na suala la Mbowe na Slaa kujikopesha ruzuku?


3. CCM wanahusikaje na kuchagua wabunge wa viti maalum Chadema kwa udugu?


4. CCM inahusikaje na suala la Chadema kutokukaguliwa mahesabu yake?


5. CCM inahusikaje na mradi wa uchangishaji wa M4C kutokuwa na ripoti yoyote / mrejesho wowote kwa wanachama wa chadema?


Hapa utaona kinachofanyika ni viongozi wa juu wa chadema kuitumia CCM kama kichaka cha kuficha ufisadi wao kwani kila anayeonekana kuzungumzia mapungufu na ufisadi wao anaitwa Msaliti/mhaini anatumiwa na CCM.


5. Hamuoni kuwa Mbowe anaitumia CCM kuficha ufisadi wake ndani ya Chadema ?

Wanatusingizia na kutubambikizia kesi ni akina Mbowe? Wanaotulipua na mabomu mikutanoni ni akina Mbowe? Acha ujuha wewe!
 
Duh JF Rocks.....

ben tuishauri chadema imshitaki kapuya kwa kuwa serikali yake inamuogopa tumsaidie yule bint nimeweka thread humu kuishauri cdm kumshitaki kapuya kaiondoa kupitia mods wasio waaminifu cdm ikifanikiwa kwa hili italeta imani kubwa kwa wananchi tuanze kutetea mwananchi mmoja mmoja kupitia jopo letu la wanasheria mahiri
 
Nimeamini kwamba kweli waTanzania mfumo wa 'zidumu fikra za mwenyekiti' unatudumaza sana.Kama kweli CHADEMA wameondoa kipengele cha ukomo wa uongozi katika katiba ya chama hilo ni TATIZO,huwezi kukiweka chama kama taasisi ya watu wachache.Unapokosolewa badilika,CHADEMA tusijifanye MIUNGU watu.
 
Msajili mwenyewe anaitegemea CHADEMA, so Mwiogamba na wasaliti wenzenu kaeni mkaa wa kufukuzwa kama kukuwa kienyeji...
 
Msajili wa Vyama vya siasa Nchini Francis Mutungi amekiomba chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kutoa majibu kuhusiana na madai ya Samson Mwigamba aliyefukuzwa uenyekiti wa chama Arusha.

Akizungumza ofisini kwake Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA Victor Kimesera amesema alipokea barua kutoka kwa Msajili akikiomba chama hicho kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Mwigamba kwamba Katiba ya chama hicho si sahihi hususan suala la Ukomo wa Uongozi.

Kiongozi huyo alisema tayari chama hicho kimemsaidia Msajili kutoa ufafanuzi na vielelezo vyote alivyoomba.

Itakumbukwa kwamba CHADEMA kupitia Kamati Kuu mwezi uliopita kiliwafukuza nyadhifa zote za uongozi Zitto Kabwe,Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwa usaliti na kuhujumu chama.Huku hatima ya uanachama wao ikiwa mikononi mwa Kamati Kuu.


Source: Nipashe.
Inafurahisha pale ambapo wenye taaluma yao wanaitumia vizuri
 
Nimeamini kwamba kweli waTanzania mfumo wa 'zidumu fikra za mwenyekiti' unatudumaza sana.Kama kweli CHADEMA wameondoa kipengele cha ukomo wa uongozi katika katiba ya chama hilo ni TATIZO,huwezi kukiweka chama kama taasisi ya watu wachache.Unapokosolewa badilika,CHADEMA tusijifanye MIUNGU watu.

Wewe Mfuasi wa Lumumba huna hadhi ya kushauri Chadema.
 
Msajili mwenyewe anaitegemea CHADEMA, so Mwiogamba na wasaliti wenzenu kaeni mkaa wa kufukuzwa kama kukuwa kienyeji...

Walitarajia msajili aombe maelekezo Lumumba.
 
Back
Top Bottom