Msajili aomba Mwongozo CHADEMA

Msajili aomba Mwongozo CHADEMA

Molemo

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
14,620
Reaction score
13,361
Msajili wa Vyama vya siasa Nchini Francis Mutungi amekiomba chama cha Demokrasia na Maendeleo - CHADEMA kutoa majibu kuhusiana na madai ya Samson Mwigamba aliyefukuzwa uenyekiti wa chama Arusha.

Akizungumza ofisini kwake Kaimu Katibu Mkuu CHADEMA Victor Kimesera amesema alipokea barua kutoka kwa Msajili akikiomba chama hicho kutoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Mwigamba kwamba Katiba ya chama hicho si sahihi hususan suala la Ukomo wa Uongozi.

Kiongozi huyo alisema tayari chama hicho kimemsaidia Msajili kutoa ufafanuzi na vielelezo vyote alivyoomba.

Itakumbukwa kwamba CHADEMA kupitia Kamati Kuu mwezi uliopita kiliwafukuza nyadhifa zote za uongozi Zitto Kabwe,Kitila Mkumbo na Samson Mwigamba kwa usaliti na kuhujumu chama.Huku hatima ya uanachama wao ikiwa mikononi mwa Kamati Kuu.

Source: Nipashe.
 
Good.........!

Ameanza utekelezaji kwa kufuata taratibu
 
nipashe hawajaweka na ufafanuzi uliotolewa na chadema?manake akina taswira na utaifamwisho hawachelewi kuja kupotosha humu, japo naamini ni ufafanuzi murua.
 
Chadema jibuni hoja kwanini mmechakachua kipengele cha ukomo wa uongozi kwenye katiba

Wameshamjibu Msajili wa vyama.Sasa wataka wakujibu wewe who the hell are you anyway? Nenda kwa office ya Msajili utapata majibu.
 
Wameshamjibu Msajili wa vyama.Sasa wataka wakujibu wewe who the hell are you anyway? Nenda kwa office ya Msajili utapata majibu.
Hoja za mkakati wa mabadiliko hazijajibiwa, au hizo ni kaa la moto?
 
Ni hatua sawi ndugu Msajili. Tunashukuru kwa kuhitaji kuwa na facts ili itimize wajibu wako.

hongera na endelea hivyo hivyo
 
watu type ya willy na wewe kwa kutafuta wanaume wenzenu hamchoki...
Ufisadi CHADEMA tukiyajibu haya 2015 asubuhi tunachukua nchi
FREEMAN MBOWE, KIONGOZI ALIYEFANIKIWA KUIFISIDI CHADEMA KWA KUWAAMINISHA WANACHADEMA KUWA MIGOGORO YOTE INAYOTOKEA CHADEMA NI MPANGO WA CCM

Mara zote Mbowe na Slaa wakiulizwa kuhusu migogoro inayoendelea Chadema wao jibu lao ni moja tu “Ni mipango ya CCM kutuvuruga Chadema ni tishio kwao”

Mwanachademe unayejitambua jibu haya:

1. Hivi CCM wanahusikaje na kunyofolewa kinyemela kwa kifungu cha ukomo wa uongozi kwenye katiba ya chadema? (Je Mbowe anatumika pia?)

2. CCM wanahusikaje na suala la Mbowe na Slaa kujikopesha ruzuku?

3. CCM wanahusikaje na kuchagua wabunge wa viti maalum Chadema kwa udugu?

4. CCM inahusikaje na suala la Chadema kutokukaguliwa mahesabu yake?

5. CCM inahusikaje na mradi wa uchangishaji wa M4C kutokuwa na ripoti yoyote / mrejesho wowote kwa wanachama wa chadema?

Hapa utaona kinachofanyika ni viongozi wa juu wa chadema kuitumia CCM kama kichaka cha kuficha ufisadi wao kwani kila anayeonekana kuzungumzia mapungufu na ufisadi wao anaitwa Msaliti/mhaini anatumiwa na CCM.

5. Hamuoni kuwa Mbowe anaitumia CCM kuficha ufisadi wake ndani ya Chadema ?
 
Back
Top Bottom