Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu CCM bara ajiunga CHADEMA

Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu CCM bara ajiunga CHADEMA

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
MSAIDIZI wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama cha kudhulumu haki za wanachama wake.

Akitangaza uamuzi wake huo leo mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za CHADEMA Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA,huku akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Urais.

Alisema CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.

"Kuna viongozi wakuu wa nchi hii ambao mimi nawaheshimu kama vile Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Makamu wa Rais Mohamed Bila, Edward Lowasa hawakunusha hata tano bora, hiyo sio haki ni dhuluma tu ilifanyika kwa maslahi ya mtu mmoja, kwa hiyo mimi kama kijana nimeona nifanye maamuzi magumu ya kuondoka ndani ya CCM." alisistiza Msunga.

Hata hivyo alisema haina maana kuendele kuwa mwajiriwa wa chama ambacho hakitendi haki na hivyo anaamini kwa kijunga kwake CHADEMA kumempatia faraja kwani anajisikia kuwa huru sasa.

"Vijana wenzangu huu ni wakati wa fungukeni sasa jiungeni na CHADEMA ni chama cha nguvu ya umma na mara zote haki itatendeka huku kwani nimekuwa kiongozi ndani ya CCM toka mwaka 2012 na ni mtumishi hadi leo hii na hata ofisi yao bado sijaikabidhi." alisema.
 
*** Ulipo tupo ****
And why not cuf

Chadema kazi ni kwako
 
Msaidizi wa Naibu katibu mkuu huyu wa sasa au yule mwingine aliyepewa unaibu waziri?
 
Neno baya zaidi wote wanamlaumu "JK kwa kupeleka majina 5 kutoka mfukoni mwake"
 
Kuna maneno kasema uongo, kwamba "...kujiunga kwake CHADEMA kumempatia faraja kwani anajiskia kuwa huru sasa"
Huu ni uongo mkubwa!! Kujiunga leo tu umeshajiona uko huru!!? Ngoja rafu zianze ndo utajua uko huru au la!!
 
Kwani ulikuwa hujui kuwa ccm kimekuwa chama cha riz na babake?
Hata magufuli kapita kwa bahati mbaya, lakini wao walikuwa na chaguo la familia.
 
Huu ni mwanzo tu wengi wanafuata.

mkuu tayari washafuata...walionyeshwa leo kundi la vijana wasiopungua 70 wameenda kwenye ofisi za CHADEMA kinondoni kisha kuchana kadi za CCM hapohapo na kupewa za CHADEMA,wataelewa tu wale magamba.
 
Kwani ulikuwa hujui kuwa ccm kimekuwa chama cha riz na babake?
Hata magufuli kapita kwa bahati mbaya, lakini wao walikuwa na chaguo la familia.

Hahaahaaa!.. mkuu hao dingi na mwanae wamegeuza CCM ni chama cha msoga.
 
chama cha chuki,dhulma,no democracy god help us!!!

sifikiri kama magufuli yupo comfortable enough!!
 
Nenda huna impact yeyote kwenye chama!! Uchu na tamaa za madaraka ndiyo zinawasumbua!! CCM uliikuta na utaiacha na itasonga mbele
Ukiingia mahakamani hapohapo hujikuta ukiwa na tahadhari, ukiingia ktk mazingira hatarishi hujisiikia kutokuwa na amani hapo hapo..na ukiwakuta baadhi ya watu hukufanya huwe huru sana hata wakikuambia tusogee hapa tuongee...NDIVYO UKIWA NA CDM UNAJISIKIA HURU SANA NA HILO LIPO HATA KTK MIKUTANO YA CDM
 
Dotto Mnzava

Mhhh....wala huyo hatusumbui make ameshagundua kwamba uadilifu wake ni mbaya sasa kwa Magufuri hilo hukumu yake ni kuweka busara mbali na hivyo hata nyie wapokeaji kuweni makini,muwekeeni majasusi make anaweza umiza nyie siku sio nyingi,
 
Last edited by a moderator:
Kuna maneno kasema uongo, kwamba "...kujiunga kwake CHADEMA kumempatia faraja kwani anajiskia kuwa huru sasa"
Huu ni uongo mkubwa!! Kujiunga leo tu umeshajiona uko huru!!? Ngoja rafu zianze ndo utajua uko huru au la!!

Usichoamini ni nn ss?
 
Back
Top Bottom