Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu CCM bara ajiunga CHADEMA

Msaidizi wa Naibu Katibu Mkuu CCM bara ajiunga CHADEMA

Ameruka majivu na kukanyaganga moto.
Huko alikoenda ndio kuna madikiteta wa kutisha.
Kama anabisha amuulize zito kama rufaa yake aliyokata iliwahi kusikilizwa.

Rufaa yake sii alikata mahakamani na akapigwa za uso? Au hujui hilo?
 
Sasa hivi ccm ndio magamba watajivua mmoja mmoja tutawajua tu
 
kwa ukatili waliofanyiwa kina lowasa ingekuwa kule kenya wangeshajitoa fasta kwenye hili liccm.
 
Chama kinachodhulumu wanachama wake, ni dhalimu hata kwa Taifa nzima. Wananchi tuamke huu ni wakati muafaka wa kuwakataa kabisa. Candidate wao amepata nafasi hiyo kwa njia za panya. Tukiwapa nafasi nyingine watazidi kutuletea njia zao za panya.
 
mm nashauri cdm yafuatayo
1 kitengo cha intelijensia imfuatilie kila mmoja aliyejiunga ktk chama chao na kuandaa taarifa ya kina
2,. taarifa ijadiliwe ktk vikao na kufikia uamuzi
3. wasipewe majukumu ya chama hadi uchaguzi uishe
4. wacwac isije ikawa system inaandaa watu wa kuhujumu chama

wengine tuongeze
 
MSAIDIZI wa Naibu Katibu Mkuu wa (CCM) Bara, Jumanne Juma Msunga ametangaza rasmi kuhama CCM na kujiunga na CHADEMA, kwa madai kuwa CCM ni chama cha kudhulumu haki za wanachama wake.

Akitangaza uamuzi wake huo leo mbele ya waandishi wa habari kwenye ofisi za CHADEMA Mkoani Singida, Msunga alisema ameamua kujinga na CHADEMA,huku akidai kuwa CCM haikutenda haki katika mchakato mzima wa kumpata Mgombea wa nafasi ya Urais.

Alisema CCM haina shukrani kwani imejaa dhuluma kwani katika mchakato huo baadhi ya Wagombea walikatwa bila kujieleza mbele ya kamati husika.

“Kuna viongozi wakuu wa nchi hii ambao mimi nawaheshimu kama vile Waziri Mkuu, Mizengo Pinda Makamu wa Rais Mohamed Bila, Edward Lowasa hawakunusha hata tano bora, hiyo sio haki ni dhuluma tu ilifanyika kwa maslahi ya mtu mmoja, kwa hiyo mimi kama kijana nimeona nifanye maamuzi magumu ya kuondoka ndani ya CCM.” alisistiza Msunga.

Hata hivyo alisema haina maana kuendele kuwa mwajiriwa wa chama ambacho hakitendi haki na hivyo anaamini kwa kijunga kwake CHADEMA kumempatia faraja kwani anajisikia kuwa huru sasa.

“Vijana wenzangu huu ni wakati wa fungukeni sasa jiungeni na CHADEMA ni chama cha nguvu ya umma na mara zote haki itatendeka huku kwani nimekuwa kiongozi ndani ya CCM toka mwaka 2012 na ni mtumishi hadi leo hii na hata ofisi yao bado sijaikabidhi.” alisema.
cc Juliana Shonza mtela mwampambwa
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom