Msaidizi wa Kampeni wa Edward Lowassa mbaroni

Msaidizi wa Kampeni wa Edward Lowassa mbaroni

Magolyo

JF-Expert Member
Joined
Mar 12, 2012
Posts
1,204
Reaction score
6
Serikali imeendelea kuwashughulikia wafuasi wa UKAWA na Lowassa kwa kutumia nguvu nyingi za Dola tangu walipokamata vijana wa tallying centres wa CHADEMA kuwapa kesi ya human trafficking, na sasa wanasema vijana wale waliingilia mitandao ya Tume ya Uchaguzi ili kuanza kupata matokeo, pamoja na kesi inayoendelea ya vijana hao mahakamani.

Sasa wameanza kukamata watu wote waliokuwa wakiwasiliana na vijana hao, na leo usiku huu amekamatwa mkurugenzi wa zamani wa Stanbic, Bashir Awale katika mazingira ya kutatanisha, lakini kwa tuhuma hizo hizo.

Rashid-11Nov2015.png

Bashir Awale

Mwanamkakati wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bashir Awale, amekamatwa na kuwekwa ndani katika Kituo cha Polisi cha Kati.

Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya timu ya kampeni ya mgombea wa CHADEMA, Edward Lowassa, zinasema kuwa Awale alikamatwa juzi jioni kwenye maeneo ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Taarifa zaidi zinasema kuwa Awale alisimamamishwa na askari, ambao walimchukua kwenye gari lao huku wakilitelekeza gari lake kwenye maeneo hayo.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, aliliambia Nipashe atalizungumzia suala hilo leo pamoja na mambo mengine.

Nimewaagiza vijana wangu waniandalie taarifa juu ya suala hilo. Nitalizungumzia jambo hilo kesho (leo) pamoja na mambo na mengine, alieleza Kamishna Kova, ambaye hakutaka kuingia kwa undani wakati alipohojiwa na gazeti hili kuhusiana na suala hilo.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili unaonyesha kwamba kukamatwa kwa Awale kunahusishwa na masuala ya Uchaguzi Mkuu uliomalizika hivi karibuni kutokana na ukaribu wake na Lowassa.

Lowassa alishindwa kwenye uchaguzi wa urais baada ya kushika nafasi ya pili kwa kupata kura 6,072, 848 sawa na asilimia 39.97 wakati mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk John Magufuli aliibuka mshindi kwa kupata kura 8,882,935 sawa na asilimia 58.46.

Awale alikuwa miongoni mwa viongozi waandamizi kwenye timu ya kampeni ya Lowassa tangu wakati alipokuwa mwanachama wa CCM.

Lowassa alipoachana na CCM na kujiunga na CHADEMA, Julai 28 mwaka huu, Awale alikuwa miongoni mwa watu waliofuatana naye.

Awale alikuwa miongoni mwa watu waliofuatana Lowassa siku anatambulishwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, baada ya kujiunga rasmi na chama hicho.

Kabla ya kuingia kwenye masuala ya siasa, Awale alikuwa Ofisa Mkuu Mtendaji wa Benki ya Stanbic nchini Tanzania kabla ya kuachia ngazi mwaka 2013.

Aliiongoza benki ya Stanbic kuanzia mwaka 2006, lakini kabla ya hapo alikuwa akifanya kazi katika Benki ya Citibank.

Tangu alipoachana na Stanbic, Awale alikuwa miongoni mwa wanamkakati waandamizi wa Lowassa tangu alipokuwa akiwania kugombea urais kwa tiketi ya CCM.

Lowassa alipokatwa jina lake CCM na kujiunga na CHADEMA, Awale alikuwamo kwenye timu ya kampeni akiwa miongoni mwa viongozi waandamizi.

Pamoja na kuwemo kwenye timu ya kampeni, pia ni anachukuliwa kama miongoni mwa wasaidizi na washauri muhimu wa Lowassa.

Kukamatwa kwa Awale kunakuja baada ya hivi karibuni vijana wanane waliokuwa wakisaidia kazi ya kujumlisha kura za Lowassa kwenye kituo cha vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kujumlisha matokeo ya kura za urais katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 25, mwaka huu.

Chanzo:
Nipashe
 
Ifike wakati tuviheshimu vyombo vyetu vya usalama,jambo la usalama linatuhusu watanzania wote likitokea tatizo litatukumba wote halitabagua huyu wa chama gani na huyu si mwanachama
 
Kumteka mkurugenzi wa stanbic hakutosaidia kitu.Kama issue ni Escrow, basi Kubenea ataeleza kila kitu Bungeni kuhusu Escrow kama alivyoahidi kwenye kampeni na hiki ndio kitakuwa kipimo kizuri cha Magufuli na serikali yake kwenye swala zima la ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka.
 
Natamani nikutukane tusi moja baya sana, ila basi tu.

Hao vijana wana makosa kwani walikuwa na lengo la kutuletea machafuko. Hatuna mzaha na mtu yeyote anayetaka kuhatarisha amani ya nchi yetu. Na kila aliyehusika lazima akamatwe na lazima wafungwe!

Bado zamu inakuja kwa mbowe na kundi lake wote, labda akimbie nchi, wewe subiri sasa. Si nyie mlinunua watu mkidhani usalama wa taifa wamelala, waliwaachia tu ili uchaguzi upite, sasa kazi kwenu.

Siku nyingine mjifunze kuwa realistic, siyo mtu unapewa kazi ya kuhatarisha amani na tapeli kama mbowe wewe unakubali tu.
 
Kwa hyo we mleta mada ulivyo kiazi hujaona kosa lililofanywa na hao vijana+lowasa?

Kosa gani limefanywa na vijana wa Lowassa?. Kama mtu amekosea kweli kwanin hawakufuata procedures za kumkamata bali wakamteka?
Inawezekana Ulimboka nae alikua kijana wa Lowassa ndo maana na yeye alipotea kwa style kama hiyo
 
acha Dawa iwaingie wanafikili mkwere Ndio bado madarakani kaingia tinga tinga atawashughurikua democrasia na utawala bora uliisha tarehe 5/11/2015 sasa ni Kazi tuuu acha watekwe.
 
Ukawa mna akili za ovyo ivi mkichukua nchi mutaiongozaje?
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Huyu siwale namjua ni mwizi tapeli kama unakumbuka pale stanbic bank aliiba ndiyo akafukuzwa kazi,

Lakini pia huyo siwale kwanza siyo mtanzania bali ni mkenya hata kukaa kwake nchini siyo halali mda wake ulishaisha lakini anakaa kiujanja tu,

Mbali na hilo siwale amekuwa akitumiwa na makundi ya kihalifu hasa yanayofanya mashambulizi kenya kwa malengo wanayojua wao.

Hata paspoti yake siyo sahihi kwani alipewa kinyume na utaratibu na masha wakati huo akiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi,

kifupi hafai wala usitetee uozo hata kidogo.
 
Huyu siwale namjua ni mwizi tapeli kama unakumbuka pale stanbic bank aliiba ndiyo akafukuzwa kazi,

Lakini pia huyo siwale kwanza siyo mtanzania bali ni mkenya hata kukaa kwake nchini siyo halali mda wake ulishaisha lakini anakaa kiujanja tu,

Mbali na hilo siwale amekuwa akitumiwa na makundi ya kihalifu hasa yanayofanya mashambulizi kenya kwa malengo wanayojua wao.

Hata paspoti yake siyo sahihi kwani alipewa kinyume na utaratibu na masha wakati huo akiwa waziri wa mambo ya ndani ya nchi,

kifupi hafai wala usitetee uozo hata kidogo.

Umechanganga habari.

Aliyekua CEO ni Bashir Awale na sio Siwale.
 
Acha vyombo vya usalama vifanye kazi...
Mtaanza ku politicize kila kitu in the name of upinzani

Mkuu hii sio kazi,hii inaitwa purging~ Ni kitu cha kawaida kwenye nchi zinazoongozwa kidicteta.Hapa tunashabikia vyama vyetu lakini siamini kama unataka Tanzania iwe nchi ya kidicteta.Fikiria tena
 
Back
Top Bottom