Duh hapo ngoma nzito amuulize mumewe kwa taratibuuu ataelewa ni nini
So true...as i said please think abt this guys kabla hamjatoa advice bc as we all know wanaume ni kama watoto they never know what they want....i think she have a right to stand for her married n never let it fall apart bc u as a woman ndo unadicide when to end ur married..if u love your husband please fight for ur married otherwise......the choice is urs end of the day n u have to bare the coinsenqunsys of ur choices
Aaagh eebana eeee hii kali, mama muage mumeo kwa upendo kabisa beba mwanao rudi kwenu kwa wazazi maana huyo akiletwa humo na hivi anapendeka sana na mumeo ujue utaambulia vioja vya ajabu kabisa!
Si una kwenu na hukufukuzwa aga vzr rudi kwenu endelea kumuomba mungu atakusaidia kabisa! Kila jambo linalotokea duniani lina maana yake na huwezi kuijua sasa hv ila utaijua baadaye kabisa. Kumbuka mawazo ya mungu ni tofauti na ya binadamu na yameachana kwa umbali mkubwa mnoooo!
Michango yetu ni msaada mkubwa!
Kama hamna ugomvi muombe mwende mahali patulivu mkishapiga stori zikakolea muulize kwa upole kama kweli anakupenda kwa dhati. Akisema anakupenda mwambie umepata taarifa za uhakika kwamba ana mpango wa kuoa. Atakurupuka kukuuliza nani kakwambia, mwambie unataka kusikia toka kwake. Hapo ndo pa kuanzia.......
Na akisema hakupendi muombe aweke wazi sababu za kutokupenda. Baadae mnaweza kuwashirikisha wazazi kadri ya ugumu wa issue. Pole
Mkwe naomba nikumiss kuanzia leo hadi JumatatuAmbassador hivi akisema hakupendi kuna haja ya kuita ndugu jamaa ama wazazi?
hahaha kama ni mapenzi honey basi yameisha zamani....
funga kwa maombi, Muombe Mungu akuonyeshe njia. Akupe hekima ya maamuzi sahihi, yote yawezekana kwa imani. Muombe Mungu akutendee = = na mapenzi yake. Kilichofungwa na Mungu mwanadamu hawezi kukitenganisha. Huyo mjomba,mumeo, na macho kodo washindwe ktk jina la Yesu.
Maria Roza nitampa true story ya ndugu yangu iwe tu changamoto kwake ingawa kwa huyu ndugu yangu hawezi jenga tena ndoa yenye afya baada ya matatizo makubwa.
Huyu dada alikuwa anaishi kwa amani na upendo na mumewe yaan aseme nini asipewe maisha yalikuwa mazuri kwa kipindi kirefu sana bila kuhisi chochote kwa mumewe.ghafla mume akabadilika akaanza kuchelewa kurudi mara harudi mwisho akatoa kali kumwambia dada sio kwamba yeye sio mzuri au hamuhudumii vizuri ila kapata msichana anaempenda sanaaaa na akamuaga anaondoka pale home akachukua briefcase yake tu yenye docs muhimu akasepa.
Baada ya muda kidogo akabadili na dini akafunga ndoa kiislam huku dada kuchanganyikiwa basi akaingia kusali sanasana maisha yakaendelea tukawa tunapishana tu na shem na mke mpya barabarani magari yote walichukua basi watoto waliozoea magari wakaanza kupanda daladala huku home mke akapangisha nusu ya jumba lao ili ajikimu maana hata ada ilikuwa shida.miaka ilikatikayule jamaa akaanza kuumwa kwa sana mpaka akalala kitandani unajua alichofanya yule mke mpya? Akampigia sister eti njoo umuuguze mumeo mie niko bize sana na majukumu mengi.
Basi mdada mbio kwa sababu ya mapenzi na mumewe uguza na wewe pika michemsho akatafuta na doctor akapata dawa nzuri jamaa akasimama akapata afya.Guess wat????alivyopona kabisa akamwambia dada asije tena pale mke wake atakasirika na kumbuka demu alishasepa kitambo alienda panga nyumba ingine.Basi demu akarudi kwa nyodo nataka hati za nyumba na gari jipya akapewa vyote maisha yakaendelea mdada akawa anajirusha tu na mabwana wengine yule baba akaanza kuwa na mawazo na hivi hapati lishe nzuri na bado anaendelea kufanya lile tendo akadhoofu sana akaumwa mbaya demu akamkimbia tena eeti kapata kazi mkoani.akaondoka kamwacha kitandani dereva wake akamfata sista kumwambia jamaa anakufa kule. dada mbio na makapu ya huduma jamani, hudumia weee akaanza dozi upya mpaka akapona
Hapo akarudi home sasa ndoa tena haikuwa ndoa sista yuko fiti haumwi jamaa ndio hivyo tena. Basi sasa hivi wanalea tu familia na yeye kuhudumiwa sista kapendeza na wala hataki mchumba wala mume mwingine. yule mumewe anaishi mle ndani kwa chumba tofauti.lile demu liko huko mkoani,anaendelea kusambaza na ni msomi ile mbaya. Si kwamba hajarudiana nae sababu anaumwa, anasema mapenzi yaliisha tena akawa anamuhurumia tu.Unaona maisha yalivyo, wanaume wanajidanganya wanapendwa kumbe inapendwa pesa tu hapo wakitetereka mtu anaonyesha makucha yake.
Ushauri wangu huyo dada aendelee na maisha yake asiruhusu kitu kama hicho cause once huyo mume keshapenda mwingine na roho ikipenda hula nyama mbichi asilazimishe kusubiri mpaka yamkute huko aruddi wakati maisha yanaendelea. Bora aishi mwenyewe na mtoto wake awe happy. kuwa na mke mwenza ni kukaribisha maradhi ya moyo ambayo utakufa na mwanao atapata shida. dah sor kwa comment ndefu
Akae chini amwulize mume ni sababu gani zinazomfanya atake kuoa tena? Ikibidi wazee wa pande zote nao wawepo kwenye kikao cha usuluhishi, na huyo pastor aliyewafungisha ndoa ahusishwe ktk hili.
Pole sana dada. Hapo pagumu sana.