Msaidieni Mwanangu tafadhali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msaidieni Mwanangu tafadhali

Discussion in 'JF Doctor' started by rakeyescarl, Oct 11, 2010.

 1. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wana JF,
  Naomba mnisaidie tatizo hili linalonisumbua sana maishani.
  Mwanangu ana umri wa miaka 5 na nusu.Na alizaliwa bila tatizo na kwa njia ya kawaida.
  Ni msichana.
  Tatizo lake kubwa alilonalo ni kutokwa na haja kubwa bila kujijua.
  Tumejaribu wataalamu wengi hapa MWZ/TZ lakini tumeshindwa.
  Kama kuna Hospitali au Dr.popote hapa duniani naomba nijulishwe nitaomba likizo nimfuate bila kujali gharama.
  Tatizo hilo si muda wote lakini najiuliza akianza darasa la kwanza itakuwaje. Ana akili sana na hana tatizo lingine lolote. Kukojoa anakojoa vizuri kabisa na hata kujisaidia,ila hizi incidences za kujisaidia bila kujijua linatusumbua sana kama familia,pamoja na sala tunazoendelea nazo na maombi lakini tunahitaji pia msaada wa utabibu.
  Asante. rakeyescarl@yahoo.ie
   
 2. k

  kisukari JF-Expert Member

  #2
  Oct 12, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  pole sana kwa tatizo la mtoto wako,jaribu ku google maybe utapata information zaidi,kitu kama hicho nimewahi kukisikia ila sina uhakika,kama ni hili tatizo ambalo wataalam wanaliita FECAL INCONTINENCE.
   
 3. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #3
  Oct 13, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45

  Pole sana mkuu. Wahi mapema hospitali kabla ishu haijwa pevu.
  Kama alivyosema mdau hapo juu inawezakana kuna tatizo baina ya ubongo na misuli iliyo katika njia ya haja kubwa, hakuna mawasiliano baina ya misuli na ubongo/mishipa ya fahamu inayomiliki utokaji wa haja kubwa. Muwaishe Muhimbili akapate tiba, atachunguzwa na kufanyiwa upasuaji. Huo ugonjwa una sababu zake zinazoeleweka ambazo ni kwa uchache, kupoteza uwezo wa kuhifadhi choo kwa utumbo mpana, uharibifu wa misuli ya sphinter katika njia ya haja kubwa, uharibifu wa mishipa ya fahamu katika njia ya haja kubwa. Tuombe mungu tatizo hilo lisiwe limesababishwa na kuchakachuliwa (kuingiliwa kinyume na maumbile).
   
 4. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #4
  Oct 13, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  peleka kwa wachungaji wa kilokole wakamwombee, hata mimi kama unataka naweza kumwombea na atapona kabisa. hakuna linaloshindikana kwa Mungu. kwa kawaida, kila tatizo duniani lina chanzo chake, na kama haujakata mzizi/source, tatizo halitakuja kuisha...wengi wakati watoto wanazaliwa wamekuwa wakiwavalisha yale mabegi ya mganga wa jadi, wengine wana mizimu ya kwao, wengine wamemchanja chale wanasema za ulinzi, wengine kipindi cha mimba walienda kwa mganga wa kienyeji either wakitaka kupata mimba wakati wa kumtafuta mtoto au wakati ana mimba akifikiri anailinda mimba ising'ofolewe, kumbe ukimpa shetani nafasi hivyo, anaweka alama kwa mtoto wako, yaani anaweka jini kwenye mtoto wako..ukimpeleka mtoto wako kwa mganga etc, utaweka jini kwake na itafika muda lile jini litafanya litakavyo...simaanishi wewe ndo umefanya, ila jichunguze from a -z afu umwombe Mungu atakusaidia.

  kuna mtu mwezi uliopita, yeye anasali kwetu, mtoto wake amemaliza form five, uyo mama ameolewa na watu wa tanga. sasa wakati wa kuolewa, walichelewa kidogo kupata mtoto, mamamkwe akawaita akawapa kamzizi ili wanywe, wakanywa kamzizi, wakapata mimba ya huyo mtoto ambaye sasa ni form five. sasa mwezi uliopita, mtoto wake alianza kulia akimwita mamake...mamaaa, bibi anataka kunichukua/kunibeba, mamake akasema, we mtoto unaongea nini, bibiyako si yuko tanga, mtoto akasema hapana, bibi huyo hapa...mama akaona kitu cha ajabu...palepale akaanza kukemea kwa Jina la Yesu we wakala wa shetani ushindwe, nakushinda kwa Jina la Yesu, mtoto wangu hatakufa ataishi..basi, akapotea(kwa huyo mtoto)...akambeba mtoto mkukumkuku akampeleka kanisani haraka, kule kawe kwa gwajima, alipofika pale, wakapiga maombi ya nguvu, mtoto akadondoka chali...mashetani yaliyoko ndani yake yakaanza kujisema, yakasema..SISI TULIWEKWA NA BIBI YAKE KIPINDI WALICHOKUNYWA DAWA, NA ILIKUWA AKIFIKA MIAKA KUMI NA NANE TU TUMUUE AKAKAE KWENYE KICHANJA CHA BIBI...wakatandika maombi ya ajabu...mtoto akapona..

  mama akaenda kumweleza babake aliyekuwa kazini, baba akakataa akasema mamangu mimi sio mchawi...basi, yule baba akapiga simu kwa mamake tanga hapohapo, badala ya kupokea salamu ya furaha toka kwa mama, akapokea fujo na matusi...mama kawaka moto anamshambulia yule baba anasea, KWANINI MNANIKATALIA MTOTO, KWANI HUYO MWANAMKE ANAFIKIRI HAO WATOTO NI WATOTO WAKE?SI WATOTO WETU, WANAMHUSU NINI, akamwambia yeye mama anamtaka huyo mtoto...baba hakuamini macho yake, alichofanya, aliwasha gari yake palepale, akawaomba wachungaji kadhaa wa pale kanisani, akawapakiza akakimbia nao hadi tanga kumfuata mamake ili wakamwombee na kumhubiria aokoke..hii kitu imetokea na ni hakika.

  Ole wenu nyie ambao watoto wenu mliwakabidhi kwa waganga wa kienyeji, kuwachanja chale etc....mambo haya ndivyo yalivyo, watoto ni zawadi toka kwa Mungu, hata kama shetani aliyekuwa amefunga akiamua kufungua yeye mwenyewe (afungaye anaweza kufungua), atakapofungua anaweka lock, wakati wowote watoto wenu wanaweza kurudi kwa bibi. amini usiamini.
   
 5. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Tatizo la kutokwa na haja kubwa (wakati mwengine haja ndogo) bila kujitambua tiba pekee inapatikana hospitali na si vinginevyo. Mwache mzazi ampeleke mwanawe hospitali, usimshauri vinginevyo
   
 6. k

  kisukari JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2010
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,753
  Likes Received: 1,038
  Trophy Points: 280
  jamani kuomba si vibaya,lakini hilo tatizo lake ni la kimatibabu zaidi.Akitibiwa atapona
   
 7. Higash

  Higash JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 844
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  hilo linatibika kabisa nenda muhimbili, sikubaliani nawe kua umeenda wataalamu wengi kama unavyosema, labda wa kienyeji bt ungekua muhmbili sasa hv
   
 8. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35

  Yote kheri-lakini unafikiri nayafurahia haya. Maliza kutangaza dini, halafu nitaku PM.
   
 9. l

  lily JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 229
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nenda hospital ya CCBRt iliyoko msasani
   
 10. Baba Mtu

  Baba Mtu JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2010
  Joined: Aug 28, 2008
  Messages: 881
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Achana nae atakupotezea muda, mpeleke mwanao nuhimbili hospitali akapate tiba.
   
 11. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  CCBRT wanadili na hii maneno nadhani. Wanawake waliokwisha jifungua, wenye FISTULA nayo c yafanania hivi? Kwa binti wa umri huo cjui ndo linaitwaje hilo tatizo. Pale CCBRT matibabu kwa matatizo ya nature hii ni bure kama sikosei. Hebu jaribu kuwatafuta, wako vizuri pia.
   
 12. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2010
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Asanteni,
  CCBRT,nilipowaeleza walishauri nifanye X-ray ya uti wa mgongo ambayo ilionyesha kuwa hana matatizo kwa upande huo na wakashauri nitafute hospitali zingione wao hawako competent kwenye jambo hilo.
   
 13. Mpeni sifa Yesu

  Mpeni sifa Yesu JF-Expert Member

  #13
  Oct 18, 2010
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 649
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  inawezekana linatibika. kuna magonjwa mengi sana yanatibika. pamoja na yote, kuna magonjwa mengine yanayotibika kabisa lakini watu wametembea mahspitali yote bila kupona, hao utasemaje? nimehudumu kanisani muda mwingi. nimekuwa karibu na watu wenye matatizo muda mwingi. kuna watu wanaleta watoto wao wamezaliwa vizuri tu, lakini kwasababu ya madawa ya kienyeji, wamejikuta watoto wanabadilika wanakuwa mazuzu/tahira hivihivi kabisa, kwasababu walimkabidhi kwa shetani. asilimia 80% ya watu wa pwani haya mambo wanayafanya sana, hasa kupitia mashehe na waganga akina manyaunyau...hili halifichiki, nenda magomeni, temeke yote, Tanga yote, manzese etc angalia kati ya watoto chini ya miaka mitatu wangapi hawana begi jeusi kiuononi, na wamama wangapi kipindi cha ujauzito au kipindi cha kunyonyesha hawakunywa dawa ya kienyeji, utashangaa karibia wote wako hivyo...

  nimepokea wamama wengi sana, mwingine anakwambia mimi nilikaa miaka miwili bila mtoto, nikaenda kigamboni kwa mganga, alipokunywa dawa akapata. Mtoto ikifika saa nne analia sana sana, afu anyamaza, ikifika saa kumi au tisa hivi usiku analia sanaaaa, kumbe yule mganga anakuja kumchukua saa nne usiku na anamrudisha saa kumi hivi...cha kuelewa ni kwamba, SHETANI HANA WATOTO WA KUMPATIA MWANADAMU, watoto ni zawadi toka kwa Mungu..ila, shetani anao uwezo kumfunga mtu asipata mtoto, na pia anao uwezo kufungua kile ambacho yeye mwenyewe shetani alikifunga either kupitia mawakala wake etc..afungaye aweza kufungua pia..this is obvious....cha ajabu sasa, anapokufanyia chochote inamaana kuwa unaingie kwenye mkataba naye, mkataba wa kumtumikia yeye maisha yako yote..mfano, kama ulitupiwa jini alafu ukawa hauzai, jini kubwa linaweza kutupwa kwako kulizidi lile la ndani yako na ukazaa lakini yule mtoto na kizazi chake chote hawatapata mtoto hadi waje waende kwa mganga kama walivyopatikana...upo hapo?

  wanawake wengi hawapati watoto si kwasababu Mungu hapendi wapate, bali, wazazi wao walipokuwa wanawapata waliingia mkataba na shetani bila kujijua hivyo maisha yao yote na kizazi chao chote watakuwa watu wa kutozaa bila kunywa dawa ya kienyeji, na wakifanya hivyo, shetani anaweka antena kwa watoto watakaowazaa. ndio maana kama mtu hajanywa midawa hiyo, kama hajaokoka utakuta anapata kifafa cha mimba etc, hasira kumchukia mtu fulani na mambo mengi ya ajabu, kile kifafa cha mimba (hata kama madaktari watasema lolote), kule kuzimu huwa wanakuwa wanamchukua mtoto na kwenda kumkwangua nyota kwanza (kila mtu huzaliwa na nyota)..

  na watu wote waliozaliwa kwa wazazi wao kunywa madawa madawa hayo, huwa hawana hata akili hata darasani..amini usiamini na mara zote huwa hawafanikiwi kwasababu shetani aliwakwangua wangali wadogo au wangali tumboni (alikwangua nyota za mafanikio yao)...kila mtu huzaliwa na nyota yake toka kwa Mungu...hata Yesu alizaliwa na nyota ya kifalme ambayo mamajusi waliiona walipokuwa wanataka kuiba kama anavyofanya shehe yahya, wakaishindwa wakaamua kufunga safari tu waende kumsujudia kwasababu mtu huyo ni mkuu sana ambaye wameshindwa kumng'ofoa nyota...hao kina shehe yahya wanao uwezo wa kuangalia usiku kwenye ulimwengu wa giza nani ana nyota ipi, wanampiga usingizi afu wanaichukua/iiiba, wanawauzia hao viongozi, wafanya biashara etc...huu ndio ulimwengu uliojaa dhambi...

  ndugu zangu, dunia hii imejaa uchafu wa ajabu, cha ajabu ni kwamba, watu wanaishi humu bila kuijua hii dunia. KAMA KUNA WATU WAMEFANYA SANA HAYO MAMBO, KIMBILIO NI KWA YESU TU. ushauri wangu ndo huo...kama hamuamini, subirini timbwilitimbwili lianze, ndo mtaanza kutafutana...
   
 14. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #14
  Oct 18, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,549
  Likes Received: 611
  Trophy Points: 280
  Lakini huyu mtoa mada amesema anafanya maombi , lakini ameona pia atafute njia za kitabibu.. nadhani ni wazo zuri na lenye akili ndugu!
   
 15. MNDEE

  MNDEE JF-Expert Member

  #15
  Oct 19, 2010
  Joined: Jul 10, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 0
  Mkuu kutoka na maelezo yako inaonekana uko tayari kupeleka mtoto popote, nakushauri waone Lion Club upate connection za madaktari au hospital za India au google. Option nyingine ni South Africa, mara nyingi hizi hospitali za nje watakuagiza vipimo wafanya uchunguzi wao kabla hawajaamua cha kufanya.
   
 16. K

  Kasungura Member

  #16
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 12, 2007
  Messages: 72
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Pole sana mzazi kwa yanayomkumba mwanao. Najua atapona kama atapata tiba sahihi.
  Maombi ni sahihi but zingatia na tiba za kitaalam.
  Plz ni PM. kama hautajali.
   
 17. r

  rakeyescarl JF-Expert Member

  #17
  Oct 19, 2010
  Joined: Dec 9, 2007
  Messages: 408
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nawashukuru nyote mlionijibu na mnaoendelea kunijibu,sijapata ufumbuzi lakini wana JF wengi walionitumia PM naona kuna mwanga mkubwa.
  Ila kwa ufupi, Muhimbili,Aghakhan,kote niliishafika ila sasa nimepata consulation ambayo naona mwanga mkubwa. Nawashukuru sana x 1000.
   
 18. KakaKiiza

  KakaKiiza JF-Expert Member

  #18
  Oct 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 10,541
  Likes Received: 2,237
  Trophy Points: 280
  Mpeni sifa yesu umenikwaza sana!!!Nitatizo sijji kabila lako ninge kudefine hoe u're!!huwezikusema maneno mazito kama nayo kwa mtu anayeuguliwa na mtoto wake!!hata yesu aliwambia nini anayeweza kumnyoshea kidole huyu binti kwamba yehe nikahaba??kama yeye nimsafi na hakjna aliyejitokeza!!! Iweje wewe hadharani umwambie maneno yakumtia simanzi mwenzio kama wese siyo mzazi au hautakuwa mzazi? Tuyaache hayo ila jifunze kutokana na makosa leo kwangu kesho kwako.......NAKUOMBA RAKEYESCARL Nenda hapo CCBRT nirahisi kukupa ushahuri au kukupatiba pole najisikia uzuni kama mzazi!!!
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  Oct 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Pole sana,ukishafanikiwa kutibu hilo tatizo,please tupe feedback,itaweza kumsaidia mtu mwingine akigoogle tatizo kama hilo
   
Loading...