Msafara wa Dkt. Slaa wazuiwa kwa muda Iringa jioni hii

Status
Not open for further replies.
Kwasasa ni dhahiri kusema cdm ina wananchi wakat ccm ikiwa na dola. Kilichobaki sasa cdm anzeni hotuba za nguvu zenye mashiko mazito kuvielimisha vyombo vya dola kuhusu aina ya mabadiliko yatarajiwayo ili navyo vikombolewe kifikra.

Asante Mungu....
 
IMG_0968.JPG

FFU wakiwa wameuzuia msafara wa viongozi wa Chadema Taifa eneo la Miyomboni mjini Iringa jioni hii ,msafara huo ulikuwa ukitokea Morogoro kuja Iringa

Msafara wa Chadema ukiwa umepigwa Stop eneo la Miyomboni jioni hii

Jeshi la Polisi mkoani Iringa limeuzuia kwa muda msafara wa viongozi wa kitaifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambao walikuwa wakiingia mjini Iringa wakitokea mkoani Morogoro.

Askari polisi hao wakiongozwa na askari wa FFU zaidi ya 100 waliuzuia msafara huo eneo la Zebra katika barabara kuu ya Iringa – Dodoma baada ya jeshi hilo awali kuzuia maandamano ya Chadema na vyama vyote kwa maelekezo ya msajili wa vyama vya siasa.

Hata hivyo kutokana na umati mkubwa wa wananchi mkufika eneo hilo viongozi wa Chadema na polisi waliweza kukubaliana msafara huo kuendelea na safari yake kuelekea nyumbani kwa mbunge Msigwa eneo la Kihesa.

Katika tukio hilo jeshi la polisi halijaweza kutumia mabomu wala nguvu zaidi katika kuwatawanya wananchi kama ilivyo kuwa mkoani Morogoro jana.

Habari zaidi utaendelea kuzipata

Siku Dr Slaa atakapokuwa anaapishwa kuwa Rais 2015 maaskari watakuwa wanamlinda kama wanavyoonekana kwenye picha...
 
Bora Rpc na Ocd wa Iringa ni waelewa na hawakuleta maafa kama jana kwa Shilogille na O.c.d wake ambae hata kuandika official letter kwake ni ....
 
Ndugu zangu wa chama changu, Huwezi kuzuia maji ya mto kwa kiganja. Matumizi ya nguvu kuzuia harakati za wapinzani hawa, haziwezekani. Huwezi kuzuia nguvu ya umma kwa kufungia magazeti, kuua raia wasio na hatia wala kuwakataza wasifike kwa wananchi. Cha msingi, ni kuruhusu waseme, na sisi twende tukaeneze sera. Dawa ya moto ni moto. kuendelea kufanya haya tunayofanya, ni kuua chama chetu, na kuongeza umaarufu kwa wapinzani.
"HAKUNA NGUVU INAYOSHINDA WAKATI" wakati umefika, wananchi wametuchoka!!!! turudi, TUJISAHIHISHE.
 
183503302.jpg

May be this is a failure to you. Na CCM Iringa mtakiona cha mtemakuni.

Tunangojea press conference. Hii inatupa tabu kidogo.
Ni wazi kabisa ccm hawakushinda kiuhalali uchaguzi uliopita.Haiwezekani na wala kuingia akilini kwamba walishinda.UONGOZI ULIPATA RIDHAA YA WANANCHI GANI?Mbona huwa sioni mambo kama haya kwa ccm kama kilishinda?hao wanachama wake ni hewa?
 
karibu raisi wetu iringa! hapa sasa ndio kitaileweka,na usisahau kwenda!Isimani,pawaga,mafinga,watu huko wanakuhitaji sana! hatulali mpaka walale wao! kama mbwai na iwe mbwai! tumechooooookaaaaaaaa!
 
Mbona sababu za kuzuia maandamano zinazotolewa na hawa watu wa liwalo na liwe ni nyepesi, eti barabara za morogoro ni nyembamba by Emmanuel Nchimbi,kuna uhusiano gani kati ya wembamba wa barabara na kuzuia maandamano, tatizo ndugu zetu ccm hawajui nchi hii imebadilika sana, propaganda za akina Hiza Tambwe na Shigela sasa hivi ni upumbavu mkubwa, wananchi wa sasa wanajua nchi hii inaliwa na wachache na ukombozi ni lazima,ccm kuweni makin meli yenu inazama.
 
Hawawezi kuzuia mvua kunyesha....,kama walivyomsikia rais wa ukweli dr slaa.inyeshe mvua liwake jua tutaandamana baada ya sensa
 
Ni kazi kuzuia mabadiliko ya fikra, kila jambo na wakati wake, this is a right time for changes....NO ONE CAN DARE TO PREVENT.....!!!!
 
Najivunia kukipenda Chama Cha Demokrasia na Maendeleo_CHADEMA.
MUNGU aendelee kuwaongezea kudra za uhai mpaka uhuru kamili utimie, naamini kwa mapenzi yake MOLA tutafika tuendako.
 
FFU wakiwa wameuzuia msafara wa viongozi wa Chadema Taifa eneo la Miyomboni mjini Iringa jioni hii ,msafara huo ulikuwa ukitokea Morogoro kuja Iringa

Msafara wa Chadema ukiwa umepigwa Stop eneo la Miyomboni jioni hii

Jeshi la Polisi mkoani Iringa limeuzuia kwa muda msafara wa viongozi wa kitaifa wa chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema) ambao walikuwa wakiingia mjini Iringa wakitokea mkoani Morogoro.

Askari polisi hao wakiongozwa na askari wa FFU zaidi ya 100 waliuzuia msafara huo eneo la Zebra katika barabara kuu ya Iringa – Dodoma baada ya jeshi hilo awali kuzuia maandamano ya Chadema na vyama vyote kwa maelekezo ya msajili wa vyama vya siasa.

Hata hivyo kutokana na umati mkubwa wa wananchi mkufika eneo hilo viongozi wa Chadema na polisi waliweza kukubaliana msafara huo kuendelea na safari yake kuelekea nyumbani kwa mbunge Msigwa eneo la Kihesa.

Katika tukio hilo jeshi la polisi halijaweza kutumia mabomu wala nguvu zaidi katika kuwatawanya wananchi kama ilivyo kuwa mkoani Morogoro jana.

Habari zaidi utaendelea kuzipata

yaani RPC wa Iringa ana busara kuliko wa Mlogolo?
 
IMG_0964.JPG

Huyu askari ni kama anasema, ... akishuka tu Dr Slaa mpandishe defender bila hata ya kushika bomba
 
Bora Rpc na Ocd wa Iringa ni waelewa na hawakuleta maafa kama jana kwa Shilogille na O.c.d wake ambae hata kuandika official letter kwake ni ....
Mkuu ipo thread inasema Dr kaahirisha M4C kwa siku ngapi cjui,nilidhani pia watabaki kwenye mazishi ya marehemu Ally,huu msafara wa Iringa tena ni wa nani? mikutano itakuwepo?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom