jamani mimi nitakuwa tofauti na wengi humu,siipendi ccm na wala sitaipenda daima ila kwa kuwapiga bado sikubaliani,hawa watu ni wezi wanamiliki hela nyingi wana hasira hawataki kuachia nchi kwa sababu wanajua kitakacho wapata pindi watakapoingia waadilifu madarakani.
wanaweza kununua silaha wakatuletea vita.
naamini mwisho wa siku haki ndiyo itashinda.
yuko wapi mikhail chausesko,yupo wapi noriega,yupo wapi ben ali,yupo wapi sadam husen,yupo wapi mobutu seseseko kuku wa zabanga,yupo wapi idd amin dada?
saa inkuja na si mbali watanzania maskini wanaoibiwa utu kwa pilao na kofia watapata mkombozi.
hakuna haja ya kupiga mawe hao ni wenzetu tuliowapa dhamana wakatugeuka,wamesomea hela zetu,ni wasaliti hawa.
mungu hukaa upande wa wanyonge daima.