Msaada wenu watalaamu

May 9, 2017
9
0
Habari zenu wakuu, ninashida wakuu,

Inanitatiza bado sijapata suluhisho mpaka mda huu na jambo lenyewe nakaribia kulifanya. Bila ya kuwachosha nianze na jambo langu ninalotaka msaada.

Ninataka kujiajiri katika kitu fulani lakini mpaka mda huu sijajua nafanya kwa utaratibu gani tupo wawili ila mhusika mkuu ni mimi, mimi nimesomea mambo ya ELECTRICAL INSTALLATION na huyo mwenzangu kasomea CCTV CAMERA & SATELITE DISH sasa swali lipo hapa tunataka kufungua workshop hatujajua tufungue kama kampuni, biashara au vipi tukitaka kufungua workshop tusajili kama aina gani?

Mfano kama tunatafuta jina la hii office yetu kwa mfano redmoon, uku mbele tunamalizia vipi redmoon company, technology service, solution au vipi swali langu lipo hapo? Msaada wenu wakuu mana hii issue tulipanga tufanye mda tu ila kwa sasa tuna asilimia 80% ya jambo letu kufanikisha ila issue ipo hapa natumai nitapata msaada mana humu kila kitu kinapatikana.
 
Back
Top Bottom