Msaada: Ndugu yangu ni dereva wa lori ana kesi ya kugonga (traffic case)

MGODOLO

JF-Expert Member
Oct 23, 2020
209
172
Habari zenu ndugu zangu wana JF, Nina ndugu yangu ambaye ni dereva wa lori, Alimgonga kijana wake kwa nyuma kwa bahati mbaya kwakua hakumuona (kwa bahati mbaya alifariki)

Ndugu yangu alikamatwa na kuwekwa Lockup siku kadhaa, Lakini kwa sasa yupo nje kwa dhamana, mpaka leo hii ana siku ya 15 anakwenda kuripoti tu na kuambiwa faili lipo kwa mwana sheria kwa lengo la kwenda mahakamani, Leseni yake ipo hukohuko.

SWALI LA KWANZA

Naomba kuuliza, Je, hali hii ya kwenda kuripoti kila siku, itamchukua muda gani mana kwasasa hawezi kufanya kazi kwakua jembe lake lipo polisi.

SWALI LA PILI

Je, Kuna uwezekano kweli akapelekwa mahakamani? Au ataishia kuripoti na kuachana naye, Mana kuhusu ndugu wa marehemu hawafuatilii tena

MSAADA NINAOTAKA

Endapo atapelekwa mahakamani Je? Ajiandae na yapi, Kuhusu maswali atakayoulizwa ajibu vipi, AKUBALI AU AKATAE... mana watu wengine wanasema akiwa mahakamani akubali, wengine wanasema akatae, Sasa mimi kama ndugu nimebaki njia panda ili asije akakosea kujibu mwisho akafungwa.

Naombeni msaada wenu kama kuna aliekutwa na hilo swala na ilikuaje,

Msaada wenu tafadhali ndigu zangu

Nawasilisha. Asanteni
 
Kwanza Pole Kwa wafiwa, kama kesi Imeshafika kwa Pilato hamna namna.

Cha Kwanza Mambo ya Jembe lake liko huko huko achana nayo kbs, ujue hapo uhai wa mtu umetoka. usije kuwatibua wafiwa.
Hao Wafiwa kuwa Karibu nao ili huyo mwanasheria akiuliza unasema nimeshawaona na pole nimewapa!

Ukifanya hivyo unawarahisishia Kazi Mwendesha Mashtaka na Bw.Pilato. Kaa nao Vizuri Mwanasheria na Bw. Pilato, Sijui Ushanfahamu hapo.? haitakiwi kutoa detail sana kwenye ushauri. Mambo ya Akatae au Akubali watafundishana mbele kwa mbele.
 
Habari zenu ndugu zangu wana Jf, Nina ndugu yangu ambaye ni dereva wa lori, Alimgonga kijana wake kwa nyuma kwa bahati mbaya kwakua hakumuona (kwa bahati mbaya alifariki)

Ndugu yangu alikamatwa na kuwekwa Lockup siku kadhaa, Lakini kwa sasa yupo nje kwa dhamana, mpaka leo hii ana siku ya 15 anakwenda kuripoti tu na kuambiwa faili lipo kwa mwana sheria kwa lengo la kwenda mahakamani, Leseni yake ipo hukohuko.

SWALI LA KWANZA
Naomba kuuliza, Je? Hali hii ya kwenda kuripoti kila siku, itamchukua muda gani mana kwasasa hawezi kufanya kazi kwakua jembe lake lipo polisi.

SWALI LA PILI
Je, Kuna uwezekano kweli akapelekwa mahakamani? Au ataishia kuripoti na kuachana naye, Mana kuhusu ndugu wa marehemu hawafuatilii tena

MSAADA NINAOTAKA
Endapo atapelekwa mahakamani Je? Ajiandae na yapi, Kuhusu maswali atakayoulizwa ajibu vipi, AKUBALI AU AKATAE... mana watu wengine wanasema akiwa mahakamani akubali, wengine wanasema akatae,... Sasa mimi kama ndugu nimebaki njia panda ili asije akakosea kujibu mwisho akafungwa.

Naombeni msaada wenu kama kuna aliekutwa na hilo swala na ilikuaje,

Msaada wenu tafadhali ndigu zangu

Nawasilisha, Asanteni
 
Polee kwa wafiwa na kwa ndugu yako!

Familia ya wafiwa, wakikuelewa na hasa baada ya wewe kuweka ubinadamu mbele, polisi hawana haja ya kupeleka kesi mahakamani! Omba kuripoti angalau mara moja kwa wiki ili uweze kuendelea na mapambano ya kimaisha!

Kuhusu jembe, sahau kuhusu hilo, askari wetu wanataka pesa kwa kila chochote, hawatakurudishia bila chochote ng'o!
 
Poleni Sana Mwambie asiogope Hiyo traffic case inaenda mahakamani ataulizwa tu Kama ni kweli atajibu kwa kawaida kwa kua akukusudia inabidi alipe faini ambayo hua ni elfu 56000 Kama sijakosea na jalada hua linafungwa

Tafuta mwanasheria mpeni elfu 10 atawaelezea vizuri
 
Ajali haina kinga pia ajitahidi awe karibu na ndugu za marehemu hata kama sio yeye atafute mtu wa niaba yake. Akiweza aubebe msiba, japo airudishi uhai but inapunguza ulipaji visasi.
 
Habari zenu ndugu zangu wana JF, Nina ndugu yangu ambaye ni dereva wa lori, Alimgonga kijana wake kwa nyuma kwa bahati mbaya kwakua hakumuona (kwa bahati mbaya alifariki)...
Jambo la msingi hakikisha ile familia ya mfiwa haina neno nanyi, usiseme wapo kimya tu lazima ujue kwa undani mioyo yao ipo safi!?

Baada ya hapo muone hakimu au askar anayehusika na hiyo kesi kujua muafaka.

Kukataa kesi ni ujinga akati kweli umefanya na ni suala la kawaida haya mambo.
 
Sasa atakataa vipi hali yeye ndo alikabidhiwa gari.
Kukataa mahakamani hakumaanishi kutokutenda kosa, lah hasha.

Kusomewa shitaka na kukataa kosa ni utamaduni wa kimahakama ili kukufanya wewe mshitakiwa uweze kuwasiliana na mawakili wako ama washauri wako wa kisheria.

Hata kama umetenda kosa na unatamani kukiri, kamwe usije kukurupuka siku ya kwanza ya kusomewa mashitaka kukubali.

Ukishasomewa mashitaka na kukubali, huwa mahakama haina haja ya kuendelea na process zingine za kimahakama bali ni hukumu inafuata hapo hapo.

Utakwenda na maji kabla haujajiandaa, hata kama una point za kukuokoa kifungoni ama kukupunguzia makali ya hukumu.
 
Sheria unasemaje?Acheni kuleta mambo kwa fikra zenu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kukataa mahakamani hakumaanishi kutokutenda kosa, lah hasha.

Kusomewa shitaka na kukataa kosa ni utamaduni wa kimahakama ili kukufanya wewe mshitakiwa uweze kuwasiliana na mawakili wako ama washauri wako wa kisheria.

Hata kama umetenda kosa na unatamani kukiri, kamwe usije kukurupuka siku ya kwanza ya kusomewa mashitaka kukubali.

Ukishasomewa mashitaka na kukubali, huwa mahakama haina haja ya kuendelea na process zingine za kimahakama bali ni hukumu inafuata hapo hapo.

Utakwenda na maji kabla haujajiandaa, hata kama una point za kukuokoa kifungoni ama kukupunguzia makali ya hukumu.
Kulingan na kesi, mfano ya ajali sidhn kama kuna haja ya kukataa.

Mi ninekupiga wewe leo ngumi halafu ukanishtak, nikiitwa mahskamani nakubar fasta ila naeleza mazingira ya kurusha ngumi.

Mwisho utasikia amekubar bira kuisumbua mahakama anahukumiwa miazi 3 jera au faini elfu 50.!!!

Nachan wallet mambo yameisha, mara nyibgi kesi huwa inasikilizwa na kutolewa maamuzi kabla ya kusimama kizimban!!!
 
Hapo hakuna kesi ya kuwaza ila tu ni sheria kesi ifike mahakamani kwa mujibu wa sheria na kitakachofua ni faini na kurudishiwa kila kitu chake
 
Kulingan na kesi, mfano ya ajali sidhn kama kuna haja ya kukataa.

Mi ninekupiga wewe leo ngumi halafu ukanishtak, nikiitwa mahskamani nakubar fasta ila naeleza mazingira ya kurusha ngumi.

Mwisho utasikia amekubar bira kuisumbua mahakama anahukumiwa miazi 3 jera au faini elfu 50.!!!

Nachan wallet mambo yameisha, mara nyibgi kesi huwa inasikilizwa na kutolewa maamuzi kabla ya kusimama kizimban!!!
Ushukuliwe kaka
 
Back
Top Bottom