Msaada, wazee wa DSM ni akina nani

Kaudunde Kautwange

JF-Expert Member
Nov 15, 2011
1,625
1,619
Habari wanajukwaa..

Nimekuwa nikijiuliza kila siku, hivi hawa wazee wa DSM ni akina nani zaidi!??

Wana mahusiano gani na serikali, maana nimesikia kuwa mh. Dk. JPM naye atazungumza nao.

Na kama ni wazee wa kawaida tuu kama walivyo wazee wengine, sasa kwa nini iwe wazee wa DSM tuu!?

Kwa nini kusiwe pia na vikao na wazee wa mikoa mingine!?

Ahsante, karibuni tuelimishane...
 
Hao ni wazee wanao ishi dar
Sio lazima wawe ccm pekee
Na unapo sema wazee hapo wanalengwa wale wenye busara
Usuje mleta yule mamvi Fisadi No
 
Huku kwetu kisiwani tuna wazee wengi na wenye kuelewa mambo lakini hawajawahi kuitwa hata na mbunge wetu kuwasilikiza. Sasa hao wa Dar es Salaam pamoja na upendeleo wote wanaopewa nchi imefikia kiwango cha kulea majipu yote haya yanayotishia uhai wa taifa bila hata ya kumuonya au kumstua JK/awamu ya nne pamoja na kuongea nao kila kukicha!
 
Habari wanajukwaa..

Nimekuwa nikijiuliza kila siku, hivi hawa wazee wa DSM ni akina nani zaidi!??

Wana mahusiano gani na serikali, maana nimesikia kuwa mh. Dk. JPM naye atazungumza nao.

Na kama ni wazee wa kawaida tuu kama walivyo wazee wengine, sasa kwa nini iwe wazee wa DSM tuu!?

Kwa nini kusiwe pia na vikao na wazee wa mikoa mingine!?

Ahsante, karibuni tuelimishane...
Kwa akili zako

Ni vile vizee vishindia kahawa na kashata pale Lumumba
 
unapozungumzia chimbuko la wazee wa DSM unaanzia hapa kwa wazee hawa
c7f8f7799560be4cb366911d602ed835.jpg

waliokuwa chimbuko la vuguvugu la kuwania uhuru na utaratibu huu wa kuzungumza nao aliuazisha MWALIMU NYERERE akaurithisha kwa maraisi wengne waliomfatia

Kutoka kulia waliosimama. 1. Abdallah Shomari
(Tandamti no. 3 )2. Nassoro kalumbanya (simba
str.) 3. Said Chamwenyewe (Aggrey/Congo str.)
4. Mtoro Ally (Muhonda str.) 5. John Rupia
(Misheni kota) 6. Julius Nyerere( Pugu
Sekondari ) 7. Said Chaurembo (Congo/
Mkunguni str.) 8. Jumbe Tambaza( Upanga ) 9.
Sheikh Suleiman Takadir (Mafia /Swahili) 10.
Dossa Aziz ( Mbaruku /Somali kipande ) 11.
Mshume Kiyate (Tandamti) 12. Juma Sultan
(Kitchwele karibu na kanisa dogo ) 13. Maalim
Shubeti (Masasi/...

nadhani hapo utapata picha wazee wa dsm ni watu gani na wana heshima ipi ktk serikari ya TANGANYIKA(sio tanzania mana tanzania ishakufa kitambo)
 
Ni wataalum wa Dsm huingii pale Magogoni bila ridhaa, yao.Hata Jerry Muro afisa taaluma wa Dar Young Africans anawaheshimu wakati wanasubiri mechi yao na mtaani wa jadi Simba.Ushirikina mtupu!!!
 
Dar ndio Tanzania kubali au ukatae!!! Hata kijijini huwezi kufanya vitu bila kuonana na wazee wa kijiji..Kabla ya uhuru wakati Nyerere anakuja Dar kuanza harakati za uhuru hawa wazee ndio waliompokea nakumtambulisha kwa kina sykes wakampokea na wao ndio waliochochea mafanikio ya TANU..Tamaduni imeendelea mpaka leo kila rais lazima akutane nakushauriana na wazee wa mjii
 
Back
Top Bottom